permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 11,682
- 14,241
Hapa tutakuwa tunatoa documents (nyaraka) mbalimbali za kisheria ambazo mtu atahitaji kama vile case laws, legislations, law books n.k.
Binafsi nina e-library kubwa sana ya hivi vitu na sitokuwa mchoyo kwa lolote, isipokuwa kuna baadhi ya vitabu vina kopyright so sitoweka hapa kwenye public itabidi nikutumie kwa email adress au vinginevyo.
Pia mjadala wowote wa kisheria (kwa wanasheria tu) ni vizuri ukawekwa hapa ili tuwekane sawa, lakini masuali ya darasani (academic questioins) yawekwe kwenye jukwaa la sheria generally.
Wanasheria karibuni sana
Mkuu nashukuru kwa usaidizi huu, nianze kwa maswali machache, naomba nijue hizi sheria kama bado zinatumika, nazo ni
Rent Restriction Act
Land Acquisition Act
Land Regulations of 1948.
Naomba kuuliza kama unavyo vitabu hivi please naviomba,
Sarkar on Evidence
Mullar's Code of Civil procedure
Treitel on Contract Law
Schmithoff on International trade and finance.
Natanguliza shukrani.