Leila Sheikh mwanahabari na mtetezi wa haki za wanawake, wakati akishiriki mjadala wa waandishi wa habari uliotayarishwa na radio DW Kiswahili leo mchana ametoa matamko ambayo hata NEC wala viongozi wa CCM hawawezi kutamka moja kwa moja kuishambulia Marekani kwa kuitaja kwa jina zaidi ya kuishia kutaja mabeberu.
Leila akichagia mjadala huo uliohusu waandishi wanavyouona uchaguzi wa Tanzania alionekana kutofautiana na waandishi wenzake kutoka mataifa ya nje kwa jinsi alivyokuwa akiitetea NEC na Rais Magufuli kwa kudai kuwa uchaguzi unaendeshwa kidemokrasia na kuongeza kuwashambulia wapinzani wanaotishia kupeleka wananchi barabarani kama watashindwa.
Alikanusha kutokuwepo uhuru wa habari kipindi hiki cha uchaguzi.