Kama kweli Heche alishughulikiwa hati yake na usalama wa taifa, basi Heche ndio wakumtilia shaka.
Anatakiwa Heche personally aje kujibu tuhuma dhidi yake, sio ajibiwe na wafuasi mitandaoni.
Hata kama kuwa na urafiki na watu serikalini sio kosa, lakini urafiki wao usivuke mipaka.
Kumchukia Lema kwa sababu anasema anachokiamini ni ujinga, Heche sio bubu au kiziwi, anajua kusoma na kuandika.
Asitumie kivuli cha kupigiwa kelele na wafuasi mitandaoni kujifichia humo, ajitokeze ajibu tuhuma dhidi yake.
Hizi negativities zinazoendelea ndani ya Chadema ni wazi watu hawaaminiani mule ndani, kuna urafiki wa mashaka kati yao.
Mpaka Lissu aje kutoka gerezani akae na hawa watu waongee face to face, huu urafiki wao wa mashaka walionao sasa hivi unazidi kukigawa chama, hata kama hawataki ionekane hivyo.