Haya mambo yanaanzishwa na wanaharakati mitandaoni, wakijibiwa ndio inaonekana viongozi wanajibizana.Hivi hili swala la hati ya kusafiria ndio muhimu zaidi wakati huu; na kama hili halitoshi, hata zile pesa alizochukuwa Heche bado halijafahamika ilikuwaje!
Sasa kweli tuseme hapa kuwa Lema hana jambo na Heche?
Hili swala la passport lina umuhimu gani katikati ya kupambania kesi inayomkabili Mwenyekiti?
Haya mapambano ya Lema haya kweli yatawaacha CHADEMA salama?
Inabidi Lema ajitokeze na aeleze waziwazi tatizo lake kuhusu Makamu Mwenyekiti.Binafsi Lema huwa simuamini kitambo sana! Anyway itakuwa ni chuki zangu tuu, binafsi. 😊
Hawa "wanaharakati" wanao uhusiano wowote na Heche?Haya mambo yanaanzishwa na wanaharakati mitandaoni, wakijibiwa ndio inaonekana viongozi wanajibizana.
Lema ni mfuasi mtiifu wa Mbowe, huko kwa lisu amejichomeka tu baada ya kuona lisu anaungwa mkono na wengiUnapoanza kuona uchokonozi kama huu anaofanya Lema sasa hivi, na hasa wakati mgumu kwa chama kama ulivyo sasa; haihitaji akili kubwa kujuwa tatizo lipo wapi.
Huyu Lema analo jambo, siyo bure.
Maneno haya ningeyaamini zaidi kama yangesemwa na mtu mwingine kuliko wewe.Lema ni mfuasi mtiifu wa Mbowe, huko kwa lisu amejichomeka tu baada ya kuona lisu anaungwa mkono na wengi
Hapa siwezi kujua internally kama huwa wana mawasiliano kati yao.Hawa "wanaharakati" wanao uhusiano wowote na Heche?
Hiki ulichoandika hapa ndio kitamaliza hili tatizo, sio watu kujitokeza huko pembeni kujigeuza wasemaji wa Heche kama vile yeye hana mdomo wa kujibu.Inabidi Lema ajitokeze na aeleze waziwazi tatizo lake kuhusu Makamu Mwenyekiti.
Kuna 'pattern' inayoonyesha dhahiri kuwa kuna jambo linalomsumbua Lema kumhusu John Heche.
Kama hao wanaomvuruga akili huko mitandaoni wanatumwa na John Heche kufanya hivyo, inabidi atoke na aeleze hilo.
Hapa siyo 'issue' ya "kumwamini au chuki", ni jambo lililo dhahiri kwamba Lema analo jambo na Heche. Ni vyema atoke ajieleze shida ilipo, na kama Heche anawatumia watu kumchokoza Lema, pia itafahamika.
Na haya si lazima yafanyike kupitia mitandaoni. Ni swala linalohitaji kushughulikiwa huko ndani ya chama.
Umesema hujui mawasiliano yao huko, lakini kutokana na majibu ya Lema yanayomlenga Heche ni kama Lema anajuwa hao wanaomchokonoa wanao uhusiano na Heche; kwa hiyo yeye analenga moja kwa moja kwa mhusika anayewatuma hao wanaharakati kumchokonoa Lema!Hapa siwezi kujua internqllly kama huwa wana mawasiliano kati yao.
What i know, kila mara likianza jambo kumhusu Heche, Lema akiongea badala ya kujibiwa na Heche, atajibiwa na wanaharakati, na ndio maana hizi kelele haziishi.
Hakuna sababu ya Heche kujitokeza hadharani kujibu chochote, hilo ndilo tatizo ninalomlaumu Lema juu yake.Hiki ulichoandika hapa ndio kitamaliza hili tatizo, sio watu kujitokeza huko pembeni kujigeuza wasemaji wa Heche kama vile yeye hana mdomo wa kujibu.
Hata kama hawezi kujibu hadharani, basi wakae vikao vya ndani waongee mambo yao wayamalize.
Lemma katika hili amekosea big time, hakutakiwa kumjibu mpuuzi kama Sativa, angempotezea tu ona sasa jibu lake lilivyoleta taharuki kwani watesi wamelitafsiri kwa maslahi yao.Hakuna sababu ya Heche kujitokeza hadharani kujibu chochote, hilo ndilo tatizo ninalomlaumu Lema juu yake.
Mambo ya chama hayawezi kumalizwa kwa kupakana matope kwenye mitandao.
Nakubaliana na wewe kwa hiki ulichoandika hapa.Umesema hujui mawasiliano yao huko, lakini kutokana na majibu ya Lema yanayomlenga Heche ni kama Lema anajuwa hao wanaomchokonoa wanao uhusiano na Heche; kwa hiyo yeye analenga moja kwa moja kwa mhusika anayewatuma hao wanaharakati kumchokonoa Lema!
At least inaonesha hivyo kutokana na 'reaction' ya Lema.
... muhimu wayamalize haya mambo hata ndani ya chama, wakiendelea kunyanaza sitashangaa mbele ya safari yakiibuka tena.Hakuna sababu ya Heche kujitokeza hadharani kujibu chochote, hilo ndilo tatizo ninalomlaumu Lema juu yake.
Mambo ya chama hayawezi kumalizwa kwa kupakana matope kwenye mitandao.
Lema ameibuka na jambo la passport from nowhere akimtuhumu mtu ambaye hakuwepo katika wanao mshambulia.Kama kweli Heche alishughulikiwa hati yake na usalama wa taifa, basi Heche ndio wakumtilia shaka.
Anatakiwa Heche personally aje kujibu tuhuma dhidi yake, sio ajibiwe na wafuasi mitandaoni.
Hata kama kuwa na urafiki na watu serikalini sio kosa, lakini urafiki wao usivuke mipaka.
Kumchukia Lema kwa sababu anasema anachokiamini ni ujinga, Heche sio bubu au kiziwi, anajua kusoma na kuandika.
Asitumie kivuli cha kupigiwa kelele na wafuasi mitandaoni kujifichia humo, ajitokeze ajibu tuhuma dhidi yake.
Hizi negativities zinazoendelea ndani ya Chadema ni wazi watu hawaaminiani mule ndani, kuna urafiki wa mashaka kati yao.
Mpaka Lissu aje kutoka gerezani akae na hawa watu waongee face to face, huu urafiki wao wa mashaka walionao sasa hivi unazidi kukigawa chama, hata kama hawataki ionekane hivyo.
Kama unakubali passport ya Brenda haijapatikana na Golugwa pia, lakini ya Heche ilipatikana kwa msaada wa DG wa TISS huoni kuna tatizo hapo?Lema ameibuka na jambo la passport from nowhere akimtuhumu mtu ambaye hakuwepo katika wanao mshambulia.
Zaidi kuonyesha amejiandaa akapandisha nyaraka juu ya namna yeye alivyoipata passport yake kama ushahidi, halafu akamtuhumu Heche bila ya ushahidi. Ni jukumu la Lema kuthibitisha tuhuma zake juu ya Heche.
Ilivyosemwa kuwa kuna kikundi ndani ya CHADEMA kinajipanga dhidi ya Makamu Mwenyekiti, sasa imeanza kujidhihirisha.
Mwenendo wa Lema una mashaka mengi sana siku za hivi karibuni, na imekua rahisi sana kumstukia sababu unafiki siyo maisha yake, hivyo amekuwa kama mlevi au mvuta bhangi mpya, lazima tu atastukiwa. Lema ndiyo Mwanasiada pekee ndani ya CHADEMA ambaye amekuwa huru sana kwenda na kurudi Canada atakavyo, ndiye pekee ndani ya CHADEMA ambaye anaibexpose na kuitangaza familia yake mitandaoni walipokuwa nchini, kinyume kabisa ma hali iliyopo ya wapinzani kuwindwa. Hata mke wa Tundu Lissu ameshindwa kuingia Tanzania kumtembelea mume wake sababu ya hofu za kiusalama, but Lema anajiachia atakavyo.
Susla la kuipata passport yake kupitia Wakili wa Chama thats not an issue, sababu wote tunajua, wakiamua hauipati hata uende na nani. Brenda Rupia ya kwake hadi leo hajaipata wala Amani Golugwa pia assport yake hajaipata na Mawakili wa Chama wapo.
Hata zile milioni 310 wakizolipishwa kipindi kile wanafungwa wakati wa Magufuli hawakuwahi kurudishiwa na Mawakili wa Chama wapo.
Kwa nini atolee mfano wa Heche na asimjibu SATIVA hii ni kutafuta uchafuzi kwa kiongozi wake ni kama anamvizia kila kukicha. Lema rudisha hadhi yako kwa kujibu hoja kwa aliyeitoaKama kweli Heche alishughulikiwa hati yake na usalama wa taifa, basi Heche ndio wakumtilia shaka.
Anatakiwa Heche personally aje kujibu tuhuma dhidi yake, sio ajibiwe na wafuasi mitandaoni.
Hata kama kuwa na urafiki na watu serikalini sio kosa, lakini urafiki wao usivuke mipaka.
Kumchukia Lema kwa sababu anasema anachokiamini ni ujinga, Heche sio bubu au kiziwi, anajua kusoma na kuandika.
Asitumie kivuli cha kupigiwa kelele na wafuasi mitandaoni kujifichia humo, ajitokeze ajibu tuhuma dhidi yake.
Hizi negativities zinazoendelea ndani ya Chadema ni wazi watu hawaaminiani mule ndani, kuna urafiki wa mashaka kati yao.
Mpaka Lissu aje kutoka gerezani akae na hawa watu waongee face to face, huu urafiki wao wa mashaka walionao sasa hivi unazidi kukigawa chama, hata kama hawataki ionekane hivyo.
Huelewi concept. Wamekuwa wakizungumzia passport ndio Lema akagusia ya Heche, hajakosea popote.Kwa nini atolee mfano wa Heche na asimjibu SATIVA hii ni kutafuta uchafuzi kwa kiongozi wake ni kama anamvizia kila kukicha. Lema rudisha hadhi yako kwa kujibu hoja kwa aliyeitoa