Yesu mwenyewe anawambia wanafunzi wake.
(Mathew 28:19.)
Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho mtakatifu.
(Mark 16:15).
Akawaambia enendeni ULIMWENGUNI mwote mkaihubiri INJILI Kwa Kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa.
Ndugu GAVANA, unaendeshwa na Roho ya Mpinga kristo.
TUBU, usipotubu utahukumiwa.
Amen
Encyclopaedia Brittanica, nakla ya 11, jalada 17, sahifa 730, yasema ya kuwa kipande chote hicho kiliongezwa baadae, yamkini mwanzo mwanzo wa karne ya pili, kuchukua maneno yaliyopotea, au yaliyoonekana kuwa ni mapungufu.
William Neil akiandika katika tafsiri ya Biblia iitwayo
Harper's Bible Commentary anasema:
"Kama lipo jambo lolote katika uchunguzi wa Injili ambalo juu yake wataalamu wamekubaliana, ni kuwa kufika hapa (yaani Marko 16.8) Injili ya Marko inakoma.
Sehemu iliyobaki ya sura (yaani 16.9-20) ndio hiyo iitwayo "Kimalizio kirefu" cha Injili.
Kimalizio hicho hakionekani katika nakla za miswada ya zamani, na ambacho ni nyongeza iliyopachikwa katika karne ya pili kutokana na maongezo ya Mathayo, Luka na Matendo...ushahidi wa kale kabisa ulioandikwa juu ya Kufufuka (Yesu) haumo katika Injili bali katika barua ya kwanza ya Paulo kuwapelekea Wakorintho 15.3-8."
Maneno hayo ya Paulo aliyowaandikia Wakorintho na ndio mara ya kwanza kutajwa kufufuka kwa Yesu ni haya:
Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maaandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; badaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.
1 Wakorintho 15.3-8
Ikiwa kipande chote tangu mstari 9 mpaka mstari 20 katika sura 16 ya Injili ya Marko, kimepachikwa, basi kisa chote cha kufufuka Yesu kimebuniwa.
Mwenye kubuni kisa hichi ni Mtakatifu Paulo.
Hivyo ndivyo tunavyoweza kuagua kutokana na kuisoma Biblia, kwani maandishi ya kwanza hayamo katika Injili bali yamo katika barua ya Paulo kwa Wakorintho.
Amesema Craveri katika Maisha ya Yesu(The Life of Jesus )
"Paulo alijihakikishia mwenyewe kuwa ijapokuwa Yesu ni kweli alikufa, lazima awe amefufuka, akiuwacha mwili wake wa kidunia nyuma ili avae mwili wa 'kiroho'.
Paulo alichanganya mawazo yake mwenyewe ya kikafiri kafiri na ya Yesu kuwa na maisha mapya kwamba ni malipo yake kwa mema yake, pamoja na imani ya Kiyahudi ya kuwajibika mapatano na Yehova (Mungu) na agano la pili.
Kwa hivyo Paulo akafunza kuwa ndiyo haya khasa yaliyokuwa ni kazi ya Yesu, na hicho ndicho cheo chake machoni mwa Mungu: kafara ya nafsi yake kwa utakatifu wake na kutokuwa na dhambi kwake ili afutie kwa pamoja makosa ya wote."
Ikiwa basi msingi wa hadithi nzima ya kufufuka Yesu hadi ya ubora wake ni kuwa ni ya shaka shaka - licha ya kuwa ni wazi kuwa ni ya uwongo - hapana njia ya kuamini ya Kuwa Yesu wakati wo wote katika historia aliwahi kuamrisha watu "
Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu," kwa sababu haya hakuyasema ila baada ya huko kunakoambiwa ni kufufuka.
Katika Biblia ya Kiswahili iliyo mbele yangu iliyotangazwa na
The British and Foreign Bible Society 1950 kifungu cha Marko 16 tangu mstari wa 9 mpaka mwisho yaani mstari wa 20 kimetiwa katika mipinde miwili hivi ( ) kuonyesha kuwa maneno hayo hayakuwamo katika maandiko ya asili.
Ilivyokuwa imethibitika kuwa hayo ya Marko si madhubuti, basi yaliyonukuliwa na Mathayo na Luka juu ya mambo hayo ya kufufuka, na kuamrisha kwenda kuhubiria watu wa ulimwengu, na kuutaja Utatu, yote hayo ni baatili.
Kwa mukhtasari tunaona kuwa Biblia inashuhudia kuwa Yesu alikuwa ni Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa Waisraili waliopotea njia.
Hadithi ya kuwa aliamrisha mafunzo yake yakatangazwe kwa watu wote "kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu" imebuniwa na kuongezwa mwishoni mwa Injili tatu za Mathayo, Marko na Luka.
Kadhaalika kuwa Yesu alifufuka kutoka wafu kwa njia ya kimiujiza imeongezwa, na kauli ya Utatu basi ya kuwa mafunzo yakatangazwe "kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu" pia nayo imebuniwa na wala haina asili yo yote ya kweli.