Yote alivyosema Yesu ni sahihi.
Yote alivyosema Paulo na mitume wengine ni sahihi na Kweli.
Uelewa wako ndio finyu. BIBLIA ni Moja, kuanzia mwanzo Hadi ufunuo ni NENO la Mungu na limethibitika na halipingani.
Yesu alikuja na kufufuka na alipaa Mbinguni alikokuwako mwanzo kabla ya kuvaa mwili.
Hayupo mwanadamu, Pepo au masonry wa kupunguza Wala kuliongeza neno la Mungu.
Andikeni kitabu chenu Cha kishetani Kwa USHETANI wenu lakini NENO la Mungu litabaki vile vile.
Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.
Amen.
Matoleo ya Biblia ya Kingereza
Katika utangulizi wa toleo la Biblia linalotumika sana, la Revised Standard Version, mtunzi ameandika yafuatayo:
"Biblia ya Revised Standard Version, ni marekebisho yaliyoidhinishwa ya toleo la American Standard Version, lilochapwa 1901, na ambalo nalo pia lilikuwa ni marekebisho ya toleo la King James Version, lilochapwa 1611...
Toleo la King James Version lililazimika kushindana na Biblia ya Geneva Bible (1560) juu ya kutumiwa na watu wengi; lakini hatimaye lilienea, na kwa zaidi ya karne mbili na nusu hakuna tafsiri ya Biblia kwa Kingereza iliyoandikwa na kuidhinishwa.
Toleo la King James Version likawa ndilo "toleo lililoidhinishwa" kwa wanaoongea Kingereza...
Ndio, Toleo la King James Version lina dosari kubwa mno.
Kufikia katikati ya karne ya kumi na tisa, maendeleo ya tafiti za Kibiblia vilevile kugunduliwa kwa miswada mingi ambayo ni ya kale zaidi kuliko ile iliyotegemewa na Toleo la King James Version, yamefanya toleo hilo
kuwa ni wazi kuwa lina dosari nyingi na mbaya mno na kusababisha kuitishwa kufanyika marekebisho ya tafsiri ya kingereza.
Kazi ikafanywa, kwa idhini ya Kanisa la Uingereza, mwaka 1870.
Toleo la Biblia la English Revised Version lilichapwa mwaka 1881 – 1885; na Toleo la American Standard Version, lahaja zake zimejiingiza katika upendeleo wa wanazuoni wa Kimarekani walioshiriki katika kazi hiyo, nalo
lilichapishwa mwaka 1901."
Katika Toleo la Biblia la Revised Standard Version, idadi kubwa ya mistari muhimu kutoka katika Toleo la King James Version ya Agano la Kale na Jipya, ambayo wasomi waliiona kuwa imeongezwa katika karne za baadaye, iliondoshwa kutoka katika matini na kuwekwa katika tanbihi.
Kwa mfano, kifungu maarufu sana katika Injili ya Yohana 8:7 kinachohusu mzinzi aliyetakiwa kupigwa mawe.
Inasemakana Yesu amesema: "Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe."
Tanbihi za Toleo la King Jemes (1952) zinaeleza "Mamlaka za kale mno zinaondosha aya za 7:53 – 8:11"
Kwa kuwa mswada namba 1209 wa Vatikani na mswada wa Sinaitic ya tangu karne ya nne haina aya kumi na
mbili hizo, wasomi wa Biblia wamefikia uamuzi wa kuwa maneno hayo hayatoki kwa Yesu.
Mfano mwingine ni kifungu kinachohusishwa na Yesu na kinachotumika kama ushahidi wa rejeo la Utatu katika Maandiko matakatifu.
Katika 1 Yohana 5:7, Inasemakana Yesu amesema: "Kuna watatu wanaoshuhudia huko mbinguni, Baba, Neno na Roho Mtakatifu: na watatu hawa ni mmoja"
Msomi maarufu sana wa Biblia, Benjamin Wilson, anaandika kuwa; maandiko haya yanayohusu "ushahidi wa mbinguni" hayamo katika mswada wowote wa Kigiriki ulioandikwa kabla ya karne ya kumi na tano! Kwa hiyo, katika Toleo la Biblia la Revised Standard Version, mstari huu umefutwa na kutolewa katika matini tena bila ya kuwekewa tanbihi.
Hata hivyo, ili kuwe na idadi ya mistari iliyosawa baina ya Toleo la Biblia la Revised Standard Version, na ile ya Toleo la Biblia la King James Version, warejeaji wameugawa mstari wa sita na kuwa mistari miwili.
REFERENCE;
The Holy Bible: Rivised Standard Version, p. iii-iv.
Ibid, p. iv.
Ibid, p. vi.
The Holy Bible: Rivised Standard Version, p. 96.
The Holy Bible: (King Jems Version