Yesu ni Mungu, soma hapa;
(Isaya:9:6).
Maana Kwa ajili yetu, mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto Mwanaume, na Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake,
Naye ataitwa Jina lake, MSHAURI WA AJABU, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, MFALME WA AMANI.
(Isaya 7:14, Mathayo 1:23).
Tazama bikra atachukua mimba, naye atazaa mtoto wa kiume, nao watamwita Immanuel, maana yake, MUNGU pamoja na nasi.
Pia Kuna swali unalikwepa, Mmetoa wapi ruhusa kujumuika na MAJINI kwenye nyumba zenu za IBADA?
YESU SI MUNGU:
KWA SABABU HANA SIFA ZA MUNGU
Mwenyezi Mungu Anazo sifa zifuatazo ambazo Yesu hanazo hata sifa moja wapo. Mwenyezi Mungu ndiye muumba wetu ambaye ni mmoja. Anajulikana na anatambulikana kwa sifa zake. Biblia inatuelezea sifa hizo.
Hapa chini nitaeleza baadhi ya sifa za Mwenyezi Mungu zinazotajwa katika Biblia. Vilevile nitaeleza kwamba Bwana Yesu Kristo hana hata sifa moja sawa na Biblia.
1. MUNGU HAJARIBIWI
Biblia inasema kwamba:
“Mtu ajaribiwapo, asiseme, ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala mwenyewe hamjaribu mtu,” (Yakobo 1:13).
Sasa tuone hali ya Bwana Yesu Kristo kwamba yeye anayo sifa hii au ni kinyume chake.
Biblia inasema kwamba:
“ Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi,” (Mathayo 4:1). Mungu hajaribiwi lakini Yesu alijaribiwa na Iblisi, kwahiyo hawezi kuwa mungu, kwa sababu ya kukosa sifa hii ya Mungu.
2. MUNGU ANAJUA KILA KITU
Ni sifa ya Mwenyezi Mungu kujua kila kitu cha dhahiri na cha siri. Kitu chochote hakiwezi kufichika kwake. Kama Biblia inavyosema kwamba:
“Basi usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukampe kila mtu kwa kadri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote.” (1Wafalme 8:39).
Sasa tuone kiwango cha Bwana Yesu cha kujua mambo. Biblia inasema kwamba:
“Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.”
(Mathayo 21:18-19).
Mtu ambaye hajui kwamba msimu huu mti fulani haupatikani matunda ilhali hata watoto wadogo wanajua misimu ya matunda mbalimbali, hawezi kuwa Mungu.
Tena aya hii inaonesha tabia ya Bwana Yesu kwamba mwenyewe alikosea kujua msimu wa matunda ya mtini na kisha akaulaani mti bure.
Pia Bw. Yesu anakiri mwenyewe kwamba hajui chochote kuhusu habari za saa ile (Mathayo 24:36).
3. MUNGU HACHOKI
Mwenyezi Mungu hana kasoro ya udhaifu wowote. Sifa zote njema zinamhusu yeye. Biblia inasema kwamba:
Je, wewe hukujua? hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana muumba miisho ya dunia, hasinzii wala hachoki, akili zake hazichunguziki.” (Isaya 40:28).
Sasa tuone hali ya Yesu. Je, yeye anayo sifa hii ya Mungu? Kama hana, basi hawezi kuwa Mungu. Biblia inasema:
“Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, Basi Yesu kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo yapata saa sita.” (Yohana 4:6). Basi mwenye kuchoka hawezi kuwa Mungu.
4 . MUNGU HASINZII WALA HALALI
Mwenyezi Mungu ni mwenye uwezo wa aina zote ambaye hahitaji kupumzika wala kusinzia. Biblia inasema kwamba:
“Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, yeye aliye mlinzi wa Israeli.” (Zaburi 121:4).
Sasa Mungu hahitaji kusinzia wala kulala lakini Bwana Yesu alikuwa akilala sana. Kwahiyo hawezi kuwa Mungu.
Biblia inasema kwamba:
Ilitokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. Naye mwenyewe alikuwapo
katika shetri, amelala juu ya mto, wakamwamsha, wakamwambia, mwalimu, si kitu kwako kama tunaangamia? (Marko 4:37-38; Mathayo 8:23-25)
Bwana Yesu anasema:
. ....Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawambie, ninapaa kwenda kwa baba yangu naye ni baba yenu,
kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. (Yohana 20:17).