Swali la 1. majini ni nini?
Kwanza kabisa yatupasa kuelewa nini maana ya neno jini, Neno jini linatokana na neno la kiarabu Jinn (djinn au Jinnee). Na lina maana ya kitu kisichoonekana au kilichofichika. (Mapepo).
Tafsiri kutoka kamusi za kiingereza zinaeleza hivi maana ya neno jini:
A: a spirit, often appearing in human form, that when summoned by a person carries out the wishes of the summoner.
B: any spirit; demon or ghost.
C: any of a class of spirits, lower than the angels, capable of appearing in human and animal forms and influencing humankind for either good or evil.
D: A supernatural creature who does one's bidding when summoned.
kwa hali hiyo basi, Majini ni miongoni mwa viumbe alivyo viumba M'Mungu kama tulivyoumbwa Binadam, Malaika, Wanyama na viumbe vingine tusivyo vijuwa, wakiwemo wadudu wa aina mbali mbali.
Matumaini kuwa mpaka hapo dada yetu pamoja na wasomaji wengine wa makala haya watakuwa wamelewa nini maana ya neno jini.
Swali la 2. Majini na waislam wana uhusiano gani katika ulimwengu wa roho?
Jibu:
Kwenye ulimwengu wa kiroho si kwa waislamu tu ambao wanahusishwa na kuwepo kwa majini,
Tukiangalia vitabu vya ulimwengu wa Dini, kama vile Uhindu (Vedas, Puranas), Ukristo (Bible),
Uyahudi (Talmud) nk. Tukichungulia Biblia ya wakristo tunakuta bwana yesu akiyakemea mapepo yaliyokuwa yakikaa ndani ya vichwa vya watu.
Haya ni majini ambayo yanasumbuwa watu na kufanya ukorofi kama walivyo baadhi ya binadamu wenye tabia chafu za kukaa vichochoroni na kukaba watu nyakati za usiku na wakati mwingine mchana kweupe.
Kwenye Biblia Majini au Mapepo asili yao ni Malaika. Baada ya kuasi amri ya M'Mungu wakafukuzwa wao pamoja na kiongozi wao Lucifer (Ibilisi). Kwa Jinsi hiyo Malaika wabaya huitwa kwa jina la Pepo.
Angalia baadhi ya aya kutoka kwenye Biblia:
Genesis 6 :2&4
...that the sons of God saw the daughters of men that they were fair; and they took them wives of all that they chose...The Nephilim were in the earth in those days, and also after that, when the sons of God came unto the daughters of men, and they bare children to them: the same were the mighty men that were of old, the men of renown.American Standard Version that the sons of God, looking at the women, saw how beautiful they were and married as many of them as they chose....The Nephilim were on earth in those days (and even afterwards), when the sons of God resorted to the women, and had children by them. These were the heroes of the days gone by, men of renown
From Jerusalem Bible (catholic).
some of supernatural beings* saw that these girls were beauutiful, so they took the ones they liked... In those days and even later, there were giants on the earth who were descendants of human women and the supernatural beings. They were the great heroes and famous men of long ago.*supernatural beings; or son of gods; or sons of God
From the Good News Bible
the sons of God saw that the doughters of men were beautiful, and they married any of them they chose....The Nephilim were on earth in those days -and also afterward- when the sons of God went to the doughters of men, and had children by them. These were the heroes of the old, men of renown
From King James Version
Pia waweza kupitia kwenye kitabu cha… Isaiah 14:12-15, Job 1: 6 and 2:1 kumb 18:10-11
Kuna majina mengi tu yanayo tumika kumaanisha neno jini, mfano mapepo (pepo), demons, Lucifer, Ghost na jamaa zangu wa kule Commoro visiwa vya ngazija wao wanawajuwa kwa jina la Kibuki.
Wamasai wao wanawajuwa kwa jina tofauti. Wapo baadhi ya watu wanawaita kimakosa kwa jina la shetani.
Wanashindwa kuelewa kuwa neno shetani ni sifa mbaya, sifa ambayo hata binadamu anapoonekana kuwa ni mwenye kufanya vitendo viovu huitwa kwa jina la shetani.
Angalia pia Mark 16:9 Pia rejea Genesis 6:2&4, Job 1: 6 na Job 2:1 kumb 18:10-11
Kwa mujibu wa biblia bwana yesu anawaagiza wanafunzi wake watawanyike ulimwenguni wakahubiri Injili kwa viumbe wote. Kwa matumaini kwamba na mapepo wamo, maana nao ni viumbe. Mark16:15-16
Kwenye ulimwengu wa imani ya kuamini dini, majini nayo yana imani tofauti tofauti kama vile tulivyo sisi binadamu. Kuna majini yenye kuamini Uislam, Ukristo, Uhindu, Upagani, na hata dini ambazo tunaziita za jadi.
Na kuna yale majini yasioamini kuwepo kwa M'Mungu.