Lema asema hakubali mtu kuuawa kwa kuwa ni shoga

Atakuwa hana malinda huyo unadhani walimpeleka Canada bure
 
Kwanini unawaza mhindu kua mkrito na sio mkrito kua mhindu?
 
What is the meaning of Leviticus 20 15?

If a man has sexual intercourse with an animal, he must be put to death; you are also to kill the animal. NLT 'If a man has sex with an animal, he must be put to death, and the animal must be killed.
Ssija
Wakristo wengi sana wamekuwa sana Wivu kusoma vitabu

Hivyo vyote vimekatanzwa acheni Unafiki Wenu mkubwa huko
Sijaona mahali alipoukubali ushoga
 
Yesu hakuzaliwa na dhambi ya kurithi. Anaitwa mwana wa Adamu sababu tu alivaa mwili,

Bt Damu yake haikutokana na mapenzi ya mwanadamu, Bali Kuvaa mwili.

MUNGU ni Mmoja na YESU ndilo JINA lake.

Amen
 
Majini unayohudhuria nayo IBADA ukiamini ni mapenzi ya Mungu majini kuchangamana na WANADAMU, hayawezi kukuruhusu uamini juu ya Yesu.

Bt nakuombea, Mungu akubadilishe Ili upate kumwamini Yesu na uokoke.

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
 
Manake ni kwamba kama ule moto wa sodoma na gomora ulishindwa kumaliza ushoga na mashoga,je kuwafunga na kuwauwa ndio tutamaliza tatizo hilo,hili ni tatizo la kiroho zaidi,kumbuka vita yetu si juu ya damu ama nyama bali ni dhidi ya ufalme wa giza.
Mashoga wa wakati ule walimalizwa waliokuja baadaye ndio wakaekewa sheria ya kuuawa
 
Yesu hakuzaliwa na dhambi ya kurithi. Anaitwa mwana wa Adamu sababu tu alivaa mwili,

Bt Damu yake haikutokana na mapenzi ya mwanadamu, Bali Kuvaa mwili.

MUNGU ni Mmoja na YESU ndilo JINA lake.

Amen

Lete ushahidi wa uliyoyasema
 
Lete ushahidi wa uliyoyasema
Yesu ni Mungu, soma hapa;

(Isaya:9:6).

Maana Kwa ajili yetu, mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto Mwanaume, na Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake,

Naye ataitwa Jina lake, MSHAURI WA AJABU, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, MFALME WA AMANI.

(Isaya 7:14, Mathayo 1:23).

Tazama bikra atachukua mimba, naye atazaa mtoto wa kiume, nao watamwita Immanuel, maana yake, MUNGU pamoja na nasi.

Pia Kuna swali unalikwepa, Mmetoa wapi ruhusa kujumuika na MAJINI kwenye nyumba zenu za IBADA?
 

Tuanzie na Isaya 7: 14


Isaya 7:14 …Tazama bikira atachukuwa mimba, atazaa mototo mwanamume naye ATAMWITA jina lake Imanueli.


Ukisoma kuanzia Isaya 7:10, utagunduwa kuwa utabiri ulikuwa unamuhusu Mfalme Ahazi au Isaya mwenyewe kuwa mkewe ndio atakaye zaa mtoto na ndio maana ukiendelea mbele mpaka kufikia Isaya 9:6, utakutana na maneno haya:

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.

Isaya 9:6

Mstari huu, umeandikwa kwa present past tense, yaani tukio ambalo limekwisha tokea, ila utokeaji wake si wa muda mrefu. Ndio maana ikaandikwa "...Tumepewa mtoto mwanamume..." Kuonyesha kuwa tendo limekwisha tendeka, si kuwa litatendeka kwa wakati ujao.

Hapa nanukuu kitabu kimojawapo ambacho ni mwongozo kwa walimu wa theologia (Teacher’s guides to religions education series) uliokubaliwa na Wanatheologia wote (Agreed Sylabases).

Kitabu hiki kinaitwa "The Rise of the Prophets" Senior lessons – Volume Six cha Norman J. Bull, M.A – Champlain and lecturer in Divinity Saint Luke’s College.

Mfululizo wa miongozo hii imetayarishwa na The Religious Education Press Ltd. Wallington Survey (1961) katika ukurasa wa 156 kikizungumzia "Imanuel"

Kinasema

Hicho ndicho wanachofundishwa Makadinali, Maaskofu, Mapadre n.k. kuwa huyo mwanamke hakuwa bikira (not a virgin) na tayari alikuwa na mtoto (was with child) na wala sio Maria bali mke wa Nabii Isaya au mfalme Ahazi. Na wanasisitiziwa kuwa hakuna utabiri wa uzazi wa mwanamke bikira hapo " there is no Prophecy here of a virgin birth".

Vilevile ukisoma Biblia ya Revised Standard Version (RSV) kuhusiana na Isaiah 7:14, wao wamelitafasiri neno la Kihebrania (עַלְמָה) 'almāh{al-maw'} kuwa ni "young woman" Mwanamke Kijana au kwa Kiswahili cha kawaida twaweza kusema Msichana (Kigori) na si kama wanavyotafasiri kwenye biblia zingine kuwa neno ilo lina maana ya "virgin" yaani Bikra au Bikira.

Neno Bikira au Bikra kwa Kihibrania ni [בְּתוּלָה (bəṯūlāh)] limetumika mara 50 kwenye Septuagint.

Hapa chini kuna tafasiri mbalimbali kutoka baadhi ya Biblia

Revised Standard Version (American; RSV)
Therefore the Lord himself will give you a sign. Behold, a young woman[a] shall conceive and bear a son, and shall call his name Imman'u-el
---


Tafasiri Nyingine:​

The Jerusalem Bible (Koren Publishing; JBK).
Therefore the Lord himself shall give you a sign: a maiden is with child and she will bear a son, and will call his name Immanuel.
---

New Jerusalem Bible (Catholic; NJB)
The Lord will give you a sign in any case: It is this: the young woman is with child and will give birth to a son whom she will call Immanuel
---

New English Bible (NEB)
Therefore the Lord himself shall give you a sign: A young woman is with child, and she will bear a son, and will call him Immanuel.
---

New English Translation Bible (NET)
For this reason the sovereign master himself will give you a confirming sign. Look, this young woman is about to conceive and will give birth to a son. You, will name him Immanuel.
 
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

1 Korinth 13:2
 
Yesu ni meana wa Mungu kama hata wewe na mimi ni Wana wa Mungu. Yesu si Mungu.
 


YESU SI MUNGU:

KWA SABABU HANA SIFA ZA MUNGU

Mwenyezi Mungu Anazo sifa zifuatazo ambazo Yesu hanazo hata sifa moja wapo. Mwenyezi Mungu ndiye muumba wetu ambaye ni mmoja. Anajulikana na anatambulikana kwa sifa zake. Biblia inatuelezea sifa hizo.

Hapa chini nitaeleza baadhi ya sifa za Mwenyezi Mungu zinazotajwa katika Biblia. Vilevile nitaeleza kwamba Bwana Yesu Kristo hana hata sifa moja sawa na Biblia.

1. MUNGU HAJARIBIWI

Biblia inasema kwamba:

“Mtu ajaribiwapo, asiseme, ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala mwenyewe hamjaribu mtu,” (Yakobo 1:13).

Sasa tuone hali ya Bwana Yesu Kristo kwamba yeye anayo sifa hii au ni kinyume chake.

Biblia inasema kwamba:

“ Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi,” (Mathayo 4:1). Mungu hajaribiwi lakini Yesu alijaribiwa na Iblisi, kwahiyo hawezi kuwa mungu, kwa sababu ya kukosa sifa hii ya Mungu.

2. MUNGU ANAJUA KILA KITU

Ni sifa ya Mwenyezi Mungu kujua kila kitu cha dhahiri na cha siri. Kitu chochote hakiwezi kufichika kwake. Kama Biblia inavyosema kwamba:

“Basi usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukampe kila mtu kwa kadri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote.” (1Wafalme 8:39).

Sasa tuone kiwango cha Bwana Yesu cha kujua mambo. Biblia inasema kwamba:

“Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.”
(Mathayo 21:18-19).

Mtu ambaye hajui kwamba msimu huu mti fulani haupatikani matunda ilhali hata watoto wadogo wanajua misimu ya matunda mbalimbali, hawezi kuwa Mungu.

Tena aya hii inaonesha tabia ya Bwana Yesu kwamba mwenyewe alikosea kujua msimu wa matunda ya mtini na kisha akaulaani mti bure.

Pia Bw. Yesu anakiri mwenyewe kwamba hajui chochote kuhusu habari za saa ile (Mathayo 24:36).

3. MUNGU HACHOKI

Mwenyezi Mungu hana kasoro ya udhaifu wowote. Sifa zote njema zinamhusu yeye. Biblia inasema kwamba:

Je, wewe hukujua? hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana muumba miisho ya dunia, hasinzii wala hachoki, akili zake hazichunguziki.” (Isaya 40:28).

Sasa tuone hali ya Yesu. Je, yeye anayo sifa hii ya Mungu? Kama hana, basi hawezi kuwa Mungu. Biblia inasema:

“Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, Basi Yesu kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo yapata saa sita.” (Yohana 4:6). Basi mwenye kuchoka hawezi kuwa Mungu.


4 . MUNGU HASINZII WALA HALALI

Mwenyezi Mungu ni mwenye uwezo wa aina zote ambaye hahitaji kupumzika wala kusinzia. Biblia inasema kwamba:

“Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, yeye aliye mlinzi wa Israeli.” (Zaburi 121:4).

Sasa Mungu hahitaji kusinzia wala kulala lakini Bwana Yesu alikuwa akilala sana. Kwahiyo hawezi kuwa Mungu.

Biblia inasema kwamba:

Ilitokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. Naye mwenyewe alikuwapo
katika shetri, amelala juu ya mto, wakamwamsha, wakamwambia, mwalimu, si kitu kwako kama tunaangamia? (Marko 4:37-38; Mathayo 8:23-25)

Bwana Yesu anasema:

. ....Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawambie, ninapaa kwenda kwa baba yangu naye ni baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. (Yohana 20:17).
 

Kamwe , Yesu Hajiiti Mungu​


Biblia (licha ya kubadilishwa na kupotoshwa kwa muda) ina mistari mingi ambayo Yesu anazungumza juu ya Mungu kama mtu tofauti kwake mwenyewe. Hii tu ni baadhi yao:

Mtu mmoja alipomwita Yesu “Mwalimu Mwema,” alijibu “Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu mmoja.’’ [Marko 10:18]

K
atika kisa kingine anasema: “Siwezi kufanya lolote peke yangu. Chochote ninachosikia, Ninahukumu na hukumu yangu ni ya haki. sitafuti mapenzi yangu mwenyewe bali mapenzi yake aliyenituma.” [Yohana 5:30]

Yesu anazungumza juu ya Mungu kama kiumbe tofauti kwake mwenyewe: Ninapanda kwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu. [Yohana 20:17]

Katika mstari huu anathibitisha kwamba alitumwa na Mungu: Huu ndio uzima wa milele: Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. [Yohana 17:3]

Iwapo Yesu angekuwa Mungu angewaambia watu wamwabudu, lakini alifanya kinyume na akakataa yeyote anayemwabudu: Nao wanani abudu bure [Mathayo 15:9].

Ikiwa Yesu alidai kuwa Mungu kungekuwa na mamia ya mistari katika Biblia ambayo ingeitaja. Lakini hakuna mstari hata mmoja katika Biblia nzima ambao Yesu anasema mimi ni Mungu, niabudu.
 
Ni Kweli Neno ulivyoquote maandiko.

Mungu hachoki, hasinzii, hajaribiwi nk.

Uliokuwa unajaribiwa ni mwili alovaa, mwili ndo Uliona njaa, na majaribu ulijaribiwa mwili alovaa.

Aliwalisha watu 5000 chakula Kutoka Mbinguni, ndo Mungu huyo.

Nimekueleza mara Kwa mara na kurudia, Mungu amewahi kuja ktk mwili wa mwanadamu na kula chakula alipomjia Ibrahimu kabla ya kuwatuma Malaika kuangamiza Sodoma na gomora.

MAJINI unayojumuika nayo ktk swala, kamwe hayawezi kukuruhusu kuelewa UKWELI huu.
 
Hivi tunavyoongea Yesu amekaa katika KITI Cha enzi Mbinguni.

Amini utaokoka, usipoamini, umekwisha kuhukumiwa.

Nakuuliza, Nani aliwapa ruhusa kuwakaribisha na kujumuika na MAJINI ktk swala zenu?
 
Wewe Mpinga kristo, Mfalme hakuzaa mtoto wa kiume Kwa Jina la Imanuel.

Pia mfalme ahazi asingeweza kumzaa mtoto mwenye sifa za Immanuel ambazo ni :

1. Mfalme wa Amani.

2.Mungu mwenye nguvu.

3. Baba wa milele.

Isaya alikuwa Nabii, alipokuwa anaongea na mfalme ndipo akatabiri juu ya Yesu,

Sifa za Yesu ndizo,

1. Mfalme wa Amani.

2. Mungu mwenye nguvu.

3. Baba wa Milele, ambaye ufalme wake hauna mwisho.

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen.
 


@ Rabbon

Kama kulisha watu wengi hata Elisha alilisha watu wengi, 1 Wafalme 4:44 , mbona humuiti Mungu ???

Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake

John 1:18

No one has seen God at any time ......................... Wanafunzi wa Yesu walikuwa vipofu na viziwi ???



1. Exodus 33:20

But He said, “You cannot see My face, for no man can see Me and live!”


2 John 5:37

And the Father who sent Me, He has testified of Me. You have neither heard His voice at any time nor seen His form.

3. 1 John 4:12


No one has seen God at any time; if we love one another, God abides in us, and His love is perfected in us.



Katika Matendo 2:22, Paulo anandika: “Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…