Nimekuelewa Mkuu isipokuwa bado hujaweka aya na reference za maneno yako.
Hakuna aya yoyote katika Biblia inayosema kwamba Yesu ni mungu, kinyume kabisa na baadhi ya Wakristo wanaoamini kwamba Yesu ni mungu.
Tunaposoma Biblia tunakuta aya kadhaa zinazoeleza kwamba Yesu ni mwana wa Adamu. Basi mwana wa Adamu hawezi kuwa mungu wala mwana wa Mungu. Biblia inasema:
1. Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, wakasema mlafi huyu na mlevi. (Mathayo 11:19).
2. Kwani kama vile Yona alivyokuwa mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo, Mwana wa Adamu atakavyokuwa kwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. (Mathayo 12:40).
3. Yesu akamwambia, mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake. (Mathayo 8: 20). Tunaposoma Biblia tunakuta mara nyingi sana Yesu anaitwa Mwana
wa Adamu. Kwa mfano: Mathayo 8:20, 9:6, 12:40, 14:28, 16:27, 17:22, 24:30 na 26:45. Marko 2:10, 9:31 na 14:21-40. Luka 9:44. Yohana 5:27 na Matendo 7:56.
Kama Mwana wa Kondoo ni kondoo – Mwana wa mbuzi huwa ni mbuzi vile vile Mwana wa Adamu ni binadamu. Haieleweki ni kwa sheria na kanuni gani Mwana wa Adamu anapachikwe jina la Mungu au Mwana wa Mungu?
4. Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, Mwana wa Daudi, Mwana wa Ibrahim. (Mathayo 1:1)
Umeniambia namhitaji Roho mtakatifu,
Swali :
Hivi Roho Mtakatifu wa kanisa lipi ndiye sahihi ?? kwani kila kanisa linasema linaongozwa na Roho mtakatifu na kila moja linadai ndilo liko sahihi ??
Unatakiwa kwanza umkiri Yesu kristo kama BWANA na mwokozi wa maisha Yako ndipo uombe kumpokea Roho MTAKATIFU.
Unaquote bible verses kimwili na humjui YESU ni nani, so kusema habari za Yesu na humwamini au mumjua Yeye ni nani unakua ANTI CHRIST kama wayahudi ndomana walimwua. Usidiriki kusambaza habari za Yesu usiyemjua utapata ADHABU kubwa sana.
Umeniuliza Roho MTAKATIFU wa KANISA lipi yupo sahihi?
Nami ntakuuliza Kanisa ni nini?
KANISA.
KANISA ni mtu, Roho mtakatifu Hakai kwenye majengo unayoyaita makanisa. ROHO MTAKATIFU anakaa ndani ya mtu mmoja mmoja amwaminiye Yesu kama Mungu na njia pekee ya Mbinguni.
USHAURI.
Funga Kwa siku Saba, omba Yesu ajifunue kwako Kwa UPYA!!
Muulize akufunulie kwann Anaitwa mwana wa Mungu, hapo hapo anajiita mwana wa daudi, tena anajiita mwana wa Adamu,
Muulize why anasema tena kabla Daudi hajazaliwa Yeye Yesu alikuwapo, Muulize tena kwann alisema ana mamlaka ya kusamehe dhambi na wakati mamlaka hayo ni ya Mungu pekee?
Muulize why, Nabii Isaya alisema tazama bikra atachukua mimba na kuzaa mwana, ataitwa Immanuel yaani Mungu pamoja na WANADAMU, Immanuel Yuko wapi na ni nani?
Muulize kwann Yohana alisema Yesu ndiye Neno aliyekuwa Kwa Mungu na alikuwapo Kwa Mungu na alikuwa Mungu,
Muulize kwann aliwaambia makutano kuwa ukiniona Mimi Yesu, umemwona Mungu, na akamwambia Mungu Yu ndani yangu, na Mimi Yesu ni ndani ya Mungu,
Muulize pia kwann aliwaambia wayahudi kuwa hayupo mwenye Uwezo wa kuniua, au kuutoa uhai wangu, Bali Mimi Yesu Nina mamlaka ya kuutoa uhai wangu Kisha nikaurudisha tena KTK MWILI!!!!!!!
Muulize kwann Yesu ulipopaa Mbinguni uliwaaambia wanafunzi kuwa utamtuma Roho wako MTAKATIFU na Roho huyo atamshuhudia Yesu na akisema tofauti na aliyofundisha Yesu huyo ni ROHO wa UWONGO?
Muulize Yesu kwann Mary alipata ujauzito Kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU na hapohapo aseme BAADAYE atamtuma Roho wake, yaani awe tena sawa na Roho aliyesaidia kuingia ndani ya tumbo la Mariam?
Muulize pia why amkane Mary na ndugu zake ambao wayahudi walijua kuwa ndo mama yake Kwa kusema " Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani, ??Mama yangu na ndugu zangu ni Hawa wanaolisikiza neno la Mungu".
Muulize kwann Mungu hashuki mwenyewe kuuhukumu Ulimwengu ktk ufunuo juu ya siku ya mwisho? Anakuja Yesu Badala ya Mungu na Kila goti Mbinguni na duniani anapigiwa YESU hujiulizi Yesu ni nani?
Hujiulizi why mapepo hayatoki Kwa Jina la Mungu, yanatolewa Kwa Jina la YESU? Yesu angekuwa Si Mungu Pepo wangetii vp wanapofukuzwa Kwa Jina lake Yesu?
Mungu zamani amejifunua Kwa majina ya KAZI zake, by Jina lake lilikuwa limefichika, bt limefunuliwa ktk agano jipya.
Muulize aliyeandikwa ameketi mkono wa kiume wa Mungu ni nani? Nini maana ya kuketi mkono wa kuume wa Mungu? Je Pana mtu anaweza kuketi ktk mkono wa kuume wa Mungu?
In spirit ukibahatika Kumuona aliyeketi ktk KITI Cha enzi utakuta ndiye huyo huyo YESU aliyekuja kama mtu akasulubiwa, akautoa uhai wake, na kujifufua na kurudi tena ktk uhalisia na uungu enzi yake.
Niliwahi kuwa na maswali kama Yako na nilitaka kuchanganyikiwa, bt nilipomruhusu Roho mtakatifu anifundishe, nilielewa.
Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.
Amen.