Lema: Mchungaji Msigwa nimeumia sana, natamani niendelee Kufanya Kazi na wewe kwenye Chama Bora CHADEMA

Lema: Mchungaji Msigwa nimeumia sana, natamani niendelee Kufanya Kazi na wewe kwenye Chama Bora CHADEMA

Chadema ni TAASISI wengi wameondoka kuanzia Kaburu,Kafulila,Kitila,Gekur, Pendo, Zitto etc.....lakini kinadunda tu,ni chuo kizuri cha kupika wana siasa kwa karne hii
CCM wametumia kila njia kisiki Mbowe aondoke ili CDM ilainike ila imeshindikana kabisa.
 
Mimi nimesikitishwa sana siku ya leo.
Mimi sijashangaa kabisa, kauli za Msigwa toka alipotaka kulipiwk na dhalimu magu ili atoke gerezani, zilionyesha yuko cdm kwa kwa kuhofia kusimangwa. Baada ya kushindwa uchaguzi alikubali kushindwa kishingo upande, lakini siku chache mbele akazua zogo ili kujitengenezea njia ya kuondoka. Na yeye ndio alikuwa anampa mama Samia mambo ya ndani ya cdm. Rejea kauli ya Samia kuwa ndani ya cdm kunawaka moto.
 
Mimi sijashangaa kabisa, kauli za Msigwa toka alipotaka kulipiwk na dhalimu magu ili atoke gerezani, zilionyesha yuko cdm kwa kwa kuhofia kusimangwa.
Mara moja moja uwe unachanganya na zako. Unajua kabisa Msigwa na Magufuli (rip shujaa) ni familia; familia zao wameoleana, kwa hiyo ulitaka Magu asisaidie kumtoa Sanzi yake toka gerezani? Nyie nyumbu wakati mwingine mna matatizo makubwa sana ya kutumia mbongo zenu kufikiri kwa ufanisi!
 
Watu makini walioondoka CDM. Zitto, Dr Slaa, Halima Mdee, Ester Bulaya, Mchungaji Msigwa. Wote hawa wasaliti?
1. Halima na Bulaya hawajaondoka chadema
2. Umetusahau mimi, Professor Mkumbo, na wengine, tulioondoka wakati mfalme mbowe alipokodisha chama kwa Lowassa.
Wote tulioondoka siyo wasaliti. Tumeondoka kwa sababu chadema kuna ugonjwa wa kufisha.
 
Back
Top Bottom