Lema: Mchungaji Msigwa nimeumia sana, natamani niendelee Kufanya Kazi na wewe kwenye Chama Bora CHADEMA

Lema: Mchungaji Msigwa nimeumia sana, natamani niendelee Kufanya Kazi na wewe kwenye Chama Bora CHADEMA

Nimefurahi kuona Lema hajawa mnafiki kwenye hili
 
CCM wametumia kila njia kisiki Mbowe aondoke ili CDM ilainike ila imeshindikana kabisa.
Sasa mbowe ataondoka vp wakati yeye ndio mwenye mali, yn n sawa na mwenye nyumba kulipa kodi
 
Kwenye hii ziara ya Mbowe ambayo anaambatana na lema. nauona uso wa lema ukiwa hauna furaha.
 
chama cha mbowe kile hata wakubali wakatae huo ndio ukweli, chama kilikuwa cuf ingawa lipumba alikibomoa , now chama bora chenye kubeba sura ya wananchi ni ccm tu ikifuatiwa na act
Hata Marekani ukikorofishana na kumkejeli kiongozi wa chama ujue hautadumu. Wale wote waliompinga Trump hawapo tena katika nafasi za uongozi. Msigwa alikuwa na haki ya kulalamikia matokeo ya uchaguzi lakini hakupaswa kumuita mwenzake hadharani kuwa mlamba viatu vya Mwenyekiti wake! Kosa lingine ni kutoka upinzani kwenda kwenye chama tawala ambacho sera na misimamo yake ni tofauti kabisa na alikokuwa. Hataweza kudai Katiba Mpya kwa nguvu zile zile. Hataweza kutoa shutuma za ufisadi za serikali ya chama chake kipya. Hawezi kukemea uonevu wowote ambao utafanywa na watu wa chama chake kipya. Credibility yake kama principled mpinzani imetoka. Bora kama angeacha siasa au angehamia chama kingine cha upinzani.

Amandla...
 
Wasikae nyuma na kuumizwa ila warekebishe walipo kosea, wasizidi kupoteza watu makini na walio jenga chama.
 
Mara moja moja uwe unachanganya na zako. Unajua kabisa Msigwa na Magufuli (rip shujaa) ni familia; familia zao wameoleana, kwa hiyo ulitaka Magu asisaidie kumtoa Sanzi yake toka gerezani? Nyie nyumbu wakati mwingine mna matatizo makubwa sana ya kutumia mbongo zenu kufikiri kwa ufanisi!
Yaani Magufuli aharibu uchaguzi kisha awabambikie kesi, ndio useme ni familia? Au unadhani kila mtu ni ndezi wa sampuli yako?
 
Tatizo kubwa la Chadema ni Mbowe, chama ni mali binafsi yake wala sio ccm wala sio kusema wana nunuliwa, chama kimekuwa kwa ajiri ya familia ya mtu mmoja halafu mnakuja na kauli za kufarijiana hapa eti wana nunuliwa, tatizo ni King mswati wa chadema.

Haiwezekani wote wanaotoka ni wabovu au wamenunuliwa, King Mswati yeye yupo kwa ajiri ya maslahi binafsi, mkisubiri mageuzi ndani KIng Mswati ni kupoteza muda, mtaishia kusema ohh wananunuliwa, ohh kura tunaibiwa, ohh tuandamane, ohh tulikubaliana na Rahisi hakuna zama za giza tena ohh story ohh story oh story miaka ina songa mwenzenu anapiga pesa, ohh nakuposha chama, ohh bila mimi chama hakiendi, ohh nakidai chama, ohh bila mimi chama kina hujumiwa, hizo zote ni usanii tu wa kupiga pesa na kuendelea kumiliki chama.

Actually mnao msikiliza nawapa pole, hizo elimu zenu zote mnasikiliza JIBA?
 
Back
Top Bottom