mibichama tunapoteza watu makini so sad
Kwa yale Yanayoendelea Kenya ni uthinitisho tosha kuwa Dunia chini ya mwavuli wa Demokrasia inatawaliwa niKikundi cha wahalifu na watu waovu ,wabinafsi wasiojali Maumivu ya wengine.
mfano tu Msiggwa katika harakati zake za kisiasa mpaka akapata jina kuna watu wengi wameumizwa na CCM na watawala wake na hata kupoteza maisha kwa sababu ya kuwa Chadema .
Lakini nadhani amegundua kuwa dunia inatawaliwa na watu waovu na wanafiki wasiojali maisha na maumivu ya wengine . Anataka aungane na wenzake wanaonekana mdomoni kuwatetea watu lakini mioyoni mwao wanawaza fedha na mali kama Husein Bashe na Doto Bireko . Bora Mwigulu Nchemba yeye yuko wazi kabisa anawaambia watu wazi wanaopata shida Tanzania wahame waende Burundi mana watapata tabu sana mana Anaamini Rasilimali wakati zinaumbwa na Mungu na yeye alimsaidia Mungu akiwa na CCM .
Msigwa Damu umeungana na Chama kilichomwaga damu za watu wasio na Hatia. Na kesho kutwa kwenye uchaguzi hawatashinda wala wewe hutashinda bila kumwaga damu za wanyonge na kupora kura zao.
Ole wako masna mali za dhulma zimefikia mwisho Afrika imeshavuka nusu ya Jubilee ni lazima mabadiliko yatokee kwa mujibu wa kalenda za kiroho. Hukusoma Nyajati.
Kilwa ilikua ni Himaya kubwa sana ya Kiarabu lakini ilipotea kabisa duniani na haitarudi kamwe.
Zanzibar ya sultani haitarudi kamwe.
Ukoloni wa Mjerumani hautarudi kamwe.
Ukoloni wa Mwingereza hautarudi kamwe.
Kilichobaki ni wazi kuwa ni utawala wa mawakala wa ukoloni . Ni wazi nao wataondolewa kwa damu na hawatarudi kamwe. Msigwa umeenda kuungana na chama kilichopo kwenye list ya kuondoka milele. na hakitarudi kamwe . Wanafikiri kuwa watantania wamelala lakini wamesahau kuwa Mungu ndiye aliyewaweka katika usingizi wao kwa makusudi yake na atawapigania yeye Nwenyewe. Mungu aliwapa uhuru Watanganyika bila kumwaga damu lakini aliuongiza nchi hii Mwalimu akataifisha mali zote za Wazungu bila kumwaga damu pia mali zote wakapewa Wananchi ambao hawakumwaga damu . Ni jambo kubwa na la nguvu za Mungu pekee. Kibinadamu na nguvu za vita haingewezekana kamwe .
Msigwa amejidanganya akidhani kuwa atawaimarisha mafisadi wa CCM Ukanda wa Nyasa akidhani kuwa yeye ndiye anayemiliki watu na roho zao bila kujua kuwa kuna Mungu na anafanya mambo yake kwa majira yake . Asijiulize tu ni kwa nini CCM haitaki kuruhusu Chama kingine kianzishwe kwa sasa . Wanajua CCM haina watu wanaoitaka hata ndani yake.
Msigwa Subiri uteuzi wa Muda na sio Ubunge kwa sababu katiba mpya ikija teuzi zitakua ngumu sana. Na ubunge hata CCM ikikuachia Jimbo huwezi kushinda kwa sababu wananchi ndio wanaochagua na hawapo tayari kuichagua CCM wanaoshindana kuuza nchi yao ili wapate pesa za kuhonga wabaki madarakani.