Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Kumbe haya mawe yote tunayo mpondaga humu hua yanampata.....[emoji15] [emoji45]
 

Alieombewa kufa ni nani huyo..? Maana naona umekazana tu hapa, kaombea watu kifo.. Hebu mtaje huyo alieombewa kifo na Lema..
 
Lema alikuwa anamuombea Rais kifo miezi michache iliyopita, tena kwa mbwembwe na kejeli unamuombea binadamu mwenzio asifikishe 2020, leo kwa unafiki anajidai kuhubiri upendo, huu unafiki Godbless J Lema unautoa wapi ?

Acha kujitoa ufahamu, unaweza kumuombea mtu kifo ana akafa? Kuna binadamu mwenye nguvu ya kumuombea mwingine kifo ana akafa kweli? Ungeniambia alimpiga risasi akapona ningekuelewa.
 
Mnahangaika na huyo raisi...
Kauli zake za kijinga jinga ndio zitumike dhidi yake next time.
Watanzania wanatakiwa wajue walichagua mtu wa aina gani.
Haina haja ya kuomboleza na kumsihi mtu ambaye yupo doomed.
 
Kwa sisi Wakatoliki tupo kwenye mwezi wa toba Kwaresma, imani yetu inatufundisha kusamehe hata walio adui zetu kwa kipindi hiki, na mtukufu Rais nj mkatoliki mwenzangu.

Bahati mbaya tuna Askofu mnafki kama Pengo mambo haya anveyafanya Kikwete kwa sababu ya uislamu wake basi ungesikia matamko mazito ya TEC na Kardinali mwenyewe na waraka wake wa kichungaji.

Kwakuwa wewe una chanel nyingi za kusikilizwa kwa wadhifa wako, nashauri copy ya waraka huu imfikie Kardinali Pengo, Tec, na ile kamati ya viongozi wa dini ya amani.

Kamwe usitalajie Sheikh mnafiki kama sheikh mkuu wa mkoa Darisalama kuinuwa mdomo wake kukemea hili, Bakwata ndio kabisa GSM wanawajengea ghorofa.

Wacha niishie hapa maana Watanzania wote wameufyata kwa mtu mmoja, ngoja na miye nikapapalie migomba yangu.
 

Ila Lema nawe uache unafiki.

Uwe unachunga kauli zako.

 
Lema fanya yako..Jimboni hakuna maji ya uhakika wala umeme!Miundo mbinu ya shida na vijana wengi hawana ajira!Ila kila siku una deal unarukia yasiyokuhusu..Fanya yako na shughulikia kero za wananchi wako!Period
Acha siasa zako rahisi wewe. Wewe ndio unajua kero za wananchi? Hopeless propaganda in the making.
 
Alieombewa kufa ni nani huyo..? Maana naona umekazana tu hapa, kaombea watu kifo.. Hebu mtaje huyo alieombewa kifo na Lema..
Acha unafiki, haujui Lema amekaa Kisongo kwa kesi ipi ?
Yeye yuko radhi kumuombea Rais afe ila analia lia hapa kuhusu kusalimiwa tu, kweli Nabii Lema ana nyumbu wengi.
 
Lema fanya yako..Jimboni hakuna maji ya uhakika wala umeme!Miundo mbinu ya shida na vijana wengi hawana ajira!Ila kila siku una deal unarukia yasiyokuhusu..Fanya yako na shughulikia kero za wananchi wako!Period
Siyo kazi ya mbunge kutafutia vijana ajira wewe, muulize Rais wako tangu ameingia madarakani ametoa ajira ngapi zaidi ya watu kupoteza ajira?
 
Acha kujitoa ufahamu, unaweza kumuombea mtu kifo ana akafa? Kuna binadamu mwenye nguvu ya kumuombea mwingine kifo ana akafa kweli? Ungeniambia alimpiga risasi akapona ningekuelewa.
Hayo muulize Nabii Lema, yeye ndio alikuwa anasema kwa mbwembwe na kejeli kuwa Rais atakufa kabla ya 2020, leo analia lia kwa sababu ya kuto kusalimiwa tu. Unafiki utamuumiza Lema.
 
Mna wakati mgumu sana upinzani safari hii msipo simama pamoja na kuweka tofauti zenu pembeni sijui hali itakuwaje
Watanzania ndio wanawakati mgumu siyo wapinzani huko ni kujitia tu upofu wa kisiasa. Taifa linapokuwa la chuki, visasi n.k. tutaumia wote hatasalia mtu hata asiyekuwa na chama.
 
kwahiyo unataka kutueleza Rais yuko sahihi?
 
Asante sana kwa ujumbe wenye busara na hekima Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema .
Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini ,ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa , ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa Nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…