Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Kama hayo maneno ya Lema ni kweli ya kwake bac binafsi nampuuza na kumuona hana maana maana anahubiri kile asichokiamini wala kukiishi.

Hivi utadumishaje umoja wa kitaifa kama unatabiria wenzako vifo?, hivi mwenzio akikutabiria kwamba utakufa siku fulan tena kwa chuki unadhan utampenda?, ndugu zake je?, rafiki zake je? Hao wote watajisikiaje kama unamtabiria kifo mpendwa wao. Huko si ndio kuhimiza utengano, chuki, dharau na uchochezi?.

Mm si mwanachama wa chama chochote hivyo sikubalian na wanasiasa wanafki wasiotenda wanayoyahubiri majukwaan ili wajipatie umaarufu usio na maana wakati huo huo wakipelekea tafran ama mgawanyiko wa kijamii
Amesema ameona MAONO, you must be out oof your senses!
 
Mapadrii wapi hao wa kumwambia yule mtu bado sijaona atakayeweza nyanyua mdomo wamseme
Njaa mbaya sana,ndo maana mi muda mwingine naona kwenda kanisan mizinguo tu viongoz wa dini wako kimaslahi sana
 
Halafu hichi ni kipindi cha kwaresma na jamaa anajiita mroman. Jaman mapdri acheni unafiki mwambieni ukwel

Kitu ambacho huwa hakisemwi na hao viongozi wa Dini pamoja na Wanaharakati ni kuwa "AMANI ni TUNDA la HAKI" hilo linapaswa kusemwa bila kumumunya maneno wala kupepesa macho! Unataka kudunisha amani wape Watu zilizo haki zao kwa wakati!
 
Tatizo Watanzani tumekuwa na uchama hadi myoyoni tunasahau ubinadam.
Hilo ni tatizo lililojengwa na viongozi wasio na nia ya uongozi bali wapo hapo kwa mambo yao binafsi binafsi. Kiongozi mzuri ni yule anayemuandaa mrithi wake ambaye ni kijana anayechipukia. Lakini kama ukiwajaza vijana chuki ukategenea, usitegeme viongozi bora siku za usoni,
 
Wewe hujui unalolitetea, huyu ni Rais wa nchi analolisema ni maagizo kwa viongozi na umma !!

Hawa jamaa wamejaa chuki ajabu , Mimi binafsi nimewahi kupenya kwenye vikao vyao ngazi ya wilaya fulani nilishuhudia mshereheshaji wao akiwaambia uchaguzi si jambo la huruma na kucheka ikibidi kuua ua mradi chama kishinde. Sasa haya yanatokea kwa mheshimiwa inaakisi maagizo toka juu kwa watendaji ,jambo ambalo si fair
Ndio sababu kaamua kuwateua MaRas MaDas na MaDed wa Chama tawala ili wakwamishe maendeleo majimbo ya Upinzani
 
Mna wakati mgumu sana upinzani safari hii msipo simama pamoja na kuweka tofauti zenu pembeni sijui hali itakuwaje
Utakuta jitu kama hili linanuka shida na dhiki. Hapa alipo yupo kituo cha feli kuvizia WiF ya coke ya bure
 
Kwa ubanguzi ulivyo kwa sasa kuna haja ya Mikoa minne kupata uhuru wake , ambayo ni KILIMANJARO ,MARA , MANYARA NA ARUSHA KWANI WANA PATO LA KUTOSHA NA AMBAZO HAZIISHI , KAMA VILE MILIMA MARU NA KILIMANJARO , MBUNGA NZURI NGORONGORO, MANYARA , SERENGETI , MADINI MENGI ,KM TANZANITE N.K
 
Lakini nasikia kuna chama kilitangaza kutoshirikiana na watu wote wa CCM, tena kilitangaza hadharani
 
Anataka yeye na yeye tu afanye wengine wote ni wasaliti mara zote yeye anasema anawatumilia wote lakini wengine wakiwatumikia wote hao ni wasaliti nakumbuka yule aliyesema hayo ni uhalisia wa tabia yake anajifunua kwa uma wake c umesikia siku hizi wanamsemo mpya CHAMA CHETU
 
Siku zote namlaumu aliyeteua hili jina sijui alikuwa akimkomoa nani kwa kweli kwanini aliwaacha watu na busara zao ma akili zao leo hii tulitakiwa tuwe tunaongozwa na Mark Mwandosya, Akina Mzee Pinda sasa hili janga hili sijui tutalibeba mbeleko gani kwa kweli...

Mungu tunusuru tunakoelekea siko kabisa

Na ndo anazidi kupandikiza chuki miongoni mwetu...

Alafu urafiki wake na Kagame huenda ndo chanzo cha yote haya....Atakuwa ametumwa kulivuruga Taifa hili.
 
Mh Rais Magufuli nakusalimu.

Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia, Wachungaji, Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali, sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.

Mh Rais, nimeogopa sana kwa kauli hii yako, je Taifa linakwenda wapi, hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? Kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu, basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .

Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini, ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa, ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuhimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa nchi hii.

Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu, ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako.

Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako, je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako?

Mh Rais neno la Mungu linasema, Wapendeni maadui zenu, waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu.

Mungu akubariki sana, natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi.


Godbless J Lema (MB)
Kamanda nitampa jina mtoto wangu jina lako liishi ....bravo
 
Kwa kauli za mkulu kwa kweli lema yabidi aombwe radhi manake sio kwa kauli hii.Lema alipokuwa gerezani aliitaji faraja ya kila alieona anaweza kumfariji bila kujali itikadi udini ukabila au hata umri so watu kutishiwa na kuitwa usaliti hii si sawa nitaipinga daima nikiwa na pumzi.
 
Back
Top Bottom