Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,281
Ninachojua ni kwamba kila nafsi itaonja mauti, either kwa kutabiriwa au bila kutabiriwa. Kwanini unakamata wanaotoa unabii? Yeye kaoneshwa mambo katika ulimwengu wa roho, kwamba uache kiburi cha uzima, majigambo, na kudhani wewe ni Mungu, vinginevyo utakufa kabla ya muda wako. Kama hutaki kufa kabla ya muda wako fanyia kazi hayo yaliyoelezwa. Jishushe, acha kiburi cha uzima, heshimu kila mtu, acha kujitwika mamlaka ya kiungu, usinyanyase wasio na hatia, usitafute sifa kwa kusema uongo, boresha maisha ya kiuchumi ya watu wako. Nabii hawa hauawi. Yeye kashatoa unabii wake. Kumfunga au kutomfunga haibadilishi unabii huo.!