Lema: Unapokuwa na viongozi mawazo yao ni uchaguzi na sio kizazi kinachokuja figo zenu zitasainiwa kuuzwa China

Lema: Unapokuwa na viongozi mawazo yao ni uchaguzi na sio kizazi kinachokuja figo zenu zitasainiwa kuuzwa China

Lema ameyasema hayo katika Mkutano wa kupinga Mkataba wa Bandari unaofanyika leo tar 23/7/2023 Temeke, ambapo amesema, Waarabu wanaangalia miaka 100 - 200 mbele wajukuu zao wataishije wabunge wenu wanaangalia 2025 watapata wapi pesa ya uchaguzi.

Huku akiendelea kuwa, Unapokuwa na viongozi mawazo yao ni uchaguzi na sio kizazi kinachokuja bado kidogo figo zenu zitasainiwa kuuza china.

Lema ameongeza kuwa Waarabu wanaona uchumi wao unakwenda mwisho waanza kutafuta uchumi duniani kwaajili ya vizazi vinavyokuja mbunge wako anaiba kura akaingie bungeni badala ya kufanya tathimini ya miaka 100 mbele anakuja kumfanya muarabu wewe kuwa mbadala wa uchumi wake na mtoto wako aendelee kuwa dereva bodaboda.
Lema yupo sahihi ✔️ nakubaliana nae!!
 
Poleni kwa mikutano wa Temeke kudorora

Moshi nao wanahitaji mikutano na maandamano kama maeneo mengine

Waambieni Vingozi wenu wajitoe kwny Vikao vya maridhiano …unafanyaje vikao na mtu anaeuza Bandari kwa Waarabu kama sio usaliti ni nini ?
 
Lema ameyasema hayo katika Mkutano wa kupinga Mkataba wa Bandari unaofanyika leo tar 23/7/2023 Temeke, ambapo amesema, Waarabu wanaangalia miaka 100 - 200 mbele wajukuu zao wataishije wabunge wenu wanaangalia 2025 watapata wapi pesa ya uchaguzi.

Huku akiendelea kuwa, Unapokuwa na viongozi mawazo yao ni uchaguzi na sio kizazi kinachokuja bado kidogo figo zenu zitasainiwa kuuza china.

Lema ameongeza kuwa Waarabu wanaona uchumi wao unakwenda mwisho waanza kutafuta uchumi duniani kwaajili ya vizazi vinavyokuja mbunge wako anaiba kura akaingie bungeni badala ya kufanya tathimini ya miaka 100 mbele anakuja kumfanya muarabu wewe kuwa mbadala wa uchumi wake na mtoto wako aendelee kuwa dereva bodaboda.
lema ameongea ukweli mtupo though ni mchungu. wanasisiemu huwa wanachukua koti la dini wanaliweka mbele, ukitaka kuongea wanasema usipaze sauti tusije kugawanyika kwa dini, kwa mgongo huo wao wanapitiapo wanapiga hela. wamewaruhusu wanzanzibar wapo na rais wao na serikali yao na wao siku zote huwa wanaongea waziwazi juu ya nchi yao, ila watanganyika hawatakiwi kuongea kabisa juu ya Tanganyika, sasa zanzibar iliungana na hewa? kwanini tusiongelee tanganyika? hawa wazanzibar wamejipanga sana, kuanzia mama yao, mbarawa, na wazili wa mambo ya ndano, wote wamewekwa strategically ili kuchuma na kuuza mali za tanganyika wakati za kwao zinabaki salama. HAKUNA MTU ATAKAYEKUJA MWENYE UCHUNGU NA TANGANYIKA, ILA MTANGANYIKA MWENYEWE. mzanzibar hata siku moja hawezi kuwa na uchungu na nchi hii zaidi sana ataona bora auze tu manake anapo kwengine kwa kwenda, ana kwao, ila sisi hatuna kwetu hapa ndio kwetu tunatakiwa tuitambue na kuthamini nchi yetu.
 
To be honest wanasiasa aina ya Lema na Lissu nawapenda sana... yaani wanapeleka ujumbe kwa wahusika bila kupepesa wala kupamba pamba kauli safi sana....

Hizi nondo zinazopelekwa kwa Samia sidhani kama atapaka hina leo!!
Mkuu ongezea jembe Mwambukuzi, yile jamaa ni moto
 
Maisha na maendeleo ya Mtanganyika hawaijali, katiba imewapa ulaji kuleni mnenepe mkajenge magorofa, walimu waendelee kuishi kama mashetani ni wajinga sana, hivi inakuaje wasomi tena level ya degree hawajitambui wala hawajui haki zao?

Ukiwa mwalimu Tanganyika nakupa maua yako....... pokea tu aise! walimu ni wajinga nchi hii, kuna kada zingine Tanganyika ni mabomu tu ndio wamejazana huko aise.
Mpwayungu Village yuko sahihi sana, walimu wengi nchi hii ni janga
 
Serikali haina mamlaka yakuniuza mimi maana ni mwili wangu labda niwape kwa mkataba fulani unadhani maisha nikuwezwa tu . Serikali imewekwa viongozi kuisimamia serikali sio watu umeona , akija kwangu hana haki ujue hilo
Acha kubwabwaja kwani hauna ubavu huo, wakikutaka wanakuchukua wakati wowote hata saa sita mchana, kwani Ben na Azory walichukuliwa saa ngapi.
 
Back
Top Bottom