Lengai Ole Sabaya aachiwa Huru kwa sharti la kutofanya kosa la Jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ambaye amekuwa akikabiliwa mashtaka saba ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu leo Aprili 05, 2023 ameachiliwa huru.

Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa baadae.

Chanzo: Jambo TV

===

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, leo April 5, 2023 ameachiliwa huru na mahakama baada ya kufutiwa mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu.

Mahakama imetoa uamuzi wa Lengai Ole Sabaya kulipa kiasi cha shilingi milioni 5 kama fidia kwa mwathirika na hapaswi kufanya kosa lolote la jinai kwa muda wa mwaka mmoja.

Sabaya ambaye mapema asubuhi ya leo alifika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi, kabla uamuzi wa kuachiwa haujatangazwa, kupitia Kifungu cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 91 kifungu cha 1A, kesi yake ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022 ilifanyiwa marejeo kama upande wa mshtakiwa ulivyoomba.

Mawakili upande wa Jamhuri waliiomba mahakama kubadilisha mashtaka ya Lengai Ole Sabaya kutoka kuwa ya kesi ya Uhujumu Uchumi na kufungua kesi yenye Mashtaka ya Makosa ya Jinai baada ya Lengai Ole Sabaya kuomba kufanya mazungumzo nje ya mahakama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ombi hilo la Sabaya lilikubaliwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Salome Mshasha baada ya Mawakili wa Lengai Ole Sabaya kuridhia na kufutwa kwa kesi yake namba 2 ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022.

Baada ya kuridhia hilo, kesi mpya aliyofunguliwa Sabaya ni kesi kesi ya Jinai Namba 31/2023 ambayo ndani yake kulikuwa na mashtaka mawili mapya dhidi yake, kosa la kwanza likiwa ni kuchukua madaraka ambayo siyo yake.

Imeelezwa kuwa Lengai Ole Sabaya na wenzake, Januari 19, 2021 katika eneo la Masama Mbosho wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, bila kibali walivamia duka la Alex Evarest SwaI na kuchukua mali na kuzizuia na kujipatia kaisi cha fedha shilingi milioni 50.

Kosa la pili ni kuzuia upatikanaji wa haki ambapo Januari 19, 2021 katika maeneo tofautitofauti katika Wilaya ya Hai na Tulia jijini Arusha na maeneo tofauti ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama za kumfanya Alex Swai kuwa ametenda kosa la kukwepa kodi.

Baada ya kusomewa mashtaka, Sabaya alikiri kufanya makosa yote hayo mawili mbele ya hakimu Salome Mshasha.
Mbona kuna source nyingine inasema huyo nyang'au hajaachiwa huru?
 
Mtu muovu anasamehewa ? Tunataka na watanzania wengine wenye kesi wakili makosa na kuachiwa mara moja tuache upendeleo hakika ccm wameriaribu taifa letu tunahitaji katiba mpya sasa inatosha
 
Hongera sana Sabaya Mungu ni mkubwa sana sasa upo mtaani waliokufitini wataona aibu kubwa sana

USSR Usiishie tuu kumpongeza, pia msihi ajifunze jinsi ya kuwa raia mwema, kutenda haki na kumuogopa Mungu..
 
Kama anayo hekima japo ya kizibo cha soda, aende kwa aliowapigilia misumari na kuwakata masikio, akawaombe msamaha.

Halafu afanye tafakari kwa nini shetani alifanya makao katika nafsi yake. Aliweka mazingira gani hata yakawa kichocheo cha kuona kwenye nafsi yake ndipo mahali salama pa kuishi.

Matendo ya Sabaya, ni vigumu kuamini kama yanaweza kufanywa na binadamu halisi. Yalikuwa ni matendo ya kinyama yanayoweza kufanywa na shetani pekee. Na ili shetani akutumie kwa kiwango kikubwa kama ilivyokuwa kwa Sabaya, ni lazima uwe umemtengenezea mazingira mazuri ya pekee.
Hili povu
 
Ameachiwa kwenye Makosa ya Uhujumu Uchumi, baada ya kukiri

Sabaya bado ana kesi ya Matumizi ya Silaha ambayo Serikali ilikata Rufaa
 
Sasa anaenda kuishi maporini maana akipita Bomang'ombe bila ulinzi atafanywa ng'ombe.
Makonda kafanywa nini mpaka leo licha ya kuwa mnamtuhumu kwa mengi?

Jifunzini kutambua nafasi zenu kwenye hii nchi, so kujifanya mashujaa nyuma ya Keyboard.
 
Mkiweka ligi ya kuwindana kitaa, amini kwamba kuna wengi aliowakosea ambao hawana uwezo wa match naye kijasusi na kiuchumi, hapo mnakuwa mnatengezeza kitu inaitwa "mwenye nguvu ammalize asiyenazo..
Kwahiyo unataka kusema kwamba Jambazi Sabaya alikuwa anapora na kuibia maskini? Unataka kusema rushwa ya million 90 aliyolazimisha kutoka kwa mtu anayeitwa Mrosso kama ilivyosomeka kwenye hati ya mashtaka ni pesa ya kutolewa na mtu asiye na nguvu ya pesa?

Sabaya alikuwa na nguvu kutoka kwa mtu ambaye hayupo tena. Tuombe hao aliowanyanyasa wasiamua kupanga njama za kuhangaika nae huko mitaani.
 
Back
Top Bottom