Lengai Ole Sabaya aachiwa Huru kwa sharti la kutofanya kosa la Jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja
Kajifunza sanatenasana. Usisahau Mbowe alikuwa amekodisha komandoo matatu kwenda kumuua? Kwa bahati mbaya (nzuri kwake) makomandoo hayo (Bwire, Ling'wenya, na Adamoo) yakaamua kutembelea soko la Rau kunywa mbege na wa6hudumu, ndipo yakakamatwa na Afande Jumanne wakiongozwa na Kamanda Kindai kwa sting operation ya Afande "Homeboy" Urio. La sivyo angekufa kama ilivyoelezwa ushahidi na Lawyer wa tigopesa. Ila ile kesi ya mbowe ya ugaidi DPP akaona bora aifute kwa vile huyo ole Sabaya hakuzurika tena.
Hivi unadhani hata uandikeje unaweza kumshusha aliyebarikiwa na vijembe vya kwenye vijiwe vya kahawa mbowe ni level nyingine kikubwa tupambaniye vipaji vyetu yeye katuacha mbali ni kati ya viongozi wakuu wanchi anatambulika je wewe na Mimi tumejificha Huku kwenye ID fake anatujua nani?
 
Mungu siyo Mbowe kiasi kwamba awe katiri kiasi hiko
Sasa kama kweli una ubongo kichwani mbowe kaingiaje hapo je sabaya alishitakiwa na mbowe au chadema au mahakama ilikuwa ya chadema mfanyabiashara aliye mshitaki sabaya ni Allex swai na ni mfanyabiashara itakiweje umwiingize mbowe hapa pili tukio la kuvamia kwa mfanyabiashara Allex sabaya alijirekodi na lipo YouTube Sasa why
 
Haki kweli imeshinda maana kama amekiri Makosa yake hatimae justice has been served.

If justice were to be served, Sabaya could be serving a prison sentence!! Hii ni dhahiri kuwa taasisi zetu hasa Mahakama Sio huru bali hufanya Kazi kwa maelekezo ya executive!! Serikali ya Samia ndio imeiamrisha Mahakama imuachie Sabaya kama vile wanavyocheza na kesi ya wakina Halima Mdee na wenzie ambao kufuatana na katiba yetu hawatakiwi kuwa wabunge!!
 
Ni sawa akisema ameshinda hii ndio aibu ambayo serikali ilikuwa inaitaka kwa kuanzisha kesi kwa kufuata mihemko na hisia za watu wenye chuki.
Inamaana sio huyu aliyeonekana ameshika mtutu kama jambazi kwenye cctv camera!??
Chuki ipi tena??
Tutumie ubongo kutafakari mambo na sio uccm na uchadema.
Tunashukur katoka kama binadamu tunatarajia amejutia kwa Mungu na sio kuona kama alionewa.
Kwa kufanya hivyo atakua mtu mwema kwa muumba wake na wanadamu, ila Akianza kuinua vimabega ataamsha hisia za watu aliowatendea unyama halafu yawe mengine tena.
 
Mfanyabiasha Alex Swai kaporwa shilingi milioni 50, mahakama inaamuru mshitakiwa amlipe mfanyabiashara Elibariki Swai shilingi milioni 5!!!
Mauzauza hoyee!!
Hapo na mimi huyu hakimu kaniacha hoi!! Hawa majambazi walipora milloni 50 halafu hakimu anasema warudishe milloni 5!! Hii hukumu ya wapi? Kweli mauza uza.
 
Hana sifa ya kuwa kiongozi wa Serikali na hata kwenye Taasisi za Umma.

..mbona Deo Mwanyika alitoka kwa plea bargain halafu Magufuli akampitisha kugombea ubunge kwa tiketi ya Ccm?

..hatima ya kisiasa ya Sabaya, kama atateuliwa tena ktk nafasi za uongozi, inategemea utashi wa Mwenyekiti wa Ccm, Rais Ssh.
 
Mfanyabiasha Alex Swai kaporwa shilingi milioni 50, mahakama inaamuru mshitakiwa amlipe mfanyabiashara Elibariki Swai shilingi milioni 5!!!
Mauzauza hoyee!!
Hili linafikirisha sana, bora hata angemlipa hiyohiyo 50 bila ya fidia. At least that would've been sensible smh.
 
Back
Top Bottom