Lengai Ole Sabaya aachiwa Huru kwa sharti la kutofanya kosa la Jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja
Mahakama imemwachia huru Sabaya ambaye ametufanyia uovu mkubwa ikiwapo kutunyang’anya fedha kwa mabilioni. Hatujaridhika na uamuzi huu na tutamhukumu Sabaya kwa sheria zetu katika mahakama zetu zilizotapakaa nchi nzima.
Aisee
 
Aliyewahi Kuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amehukumiwa Kifungo cha Nje cha Mwaka mmoja baada ya kukiri makosa na kuomba mahakama imwangalie kwa jicho la huruma.

=======
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, imemtia hatiani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya mara baada ya kukiri kosa na kumfunga kifungo cha mwaka mmoja nje bila kufanya kosa lolote la jinai.

Sabaya amekiri kosa hilo kwa njia ya ‘Plea Bargaining, ambao ni mchakato wa makubaliano / maridhiano maalumu katika kesi ya jinai kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka kupitia Mwendesha mashtaka na mshtakiwa ambapo mshatikiwa anaweza kukiri kosa moja au zaidi ili aweze kupata nafuu katika kesi inayomkabili.

Sabaya ambaye alisalia kwenye kesi namba 2 ya mwaka 2022 baada ya wenzake Sylvester Nyegu, Nathan Msuya, John Aweyo na Antero Asey ambao septemba 7, 2022 waliachiwa baada ya kufanya makubaliano mahakama na mwendesha mashtaka Mkuu wa serikali.

Msingi wa kesi hiyo kwa Mujibu ya hati ya mashtaka inadaiwa Mnamo Februari 21. 2021 Sabaya na waliokuwa wenzake hao walijipatia kitita cha Tsh Milioni 50 Kutoka kwa mfanyabiashara Alex Swai wakimtisha kutoa taarifa zake za ukwepaji kodi.

Ikumbukwe pia tangu kesi hiyo kuanza kwake Juni Mosi, 2022 haikuwai kusikilizwa kutokana na sababu mbalimbali za kisheria.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Salome Mshasha leo Aprili 05, 2023 ilifika Mahakamani kwa ajili ya kutajwa lakini upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili Mwandamizi wa Serikali Verediana Mlenza akadai mshtakiwa ameomba makubaliano nje ya Mahakama na Mwendesha mashtaka Mkuu wa serikali.

Maombi ambayo Mahakama iliyaridhia na kumuachia huru Mshtakiwa huyo Lengai ole Sabaya kwa shart la kifungo cha nje kwa muda wa mwaka Mmoja, na kumtaka amlipe fidia ya Tsh Milioni Tano mfanyabiashara Elbariki Swai ambaye ni Muathirika wa tukio hilo.


Source: ITV Habari

Pia soma: Lengai Ole Sabaya aachiwa Huru
Hopefully amenyooka kisawaswa, hawez jiingiza kweny uvunjaji wa sheria tena!!!
 
Mahakama imemwachia huru Sabaya ambaye ametufanyia uovu mkubwa ikiwapo kutunyang’anya fedha kwa mabilioni. Hatujaridhika na uamuzi huu na tutamhukumu Sabaya kwa sheria zetu katika mahakama zetu zilizotapakaa nchi nzima.
Nyie ni watu mliokia mnakwepa Kodi, mkataka afatane na ninyi kuwaibia wananchi wanyonge, mkashindwa mkamtengenezea chain ya RUSHWA kwenye kuhakikisha mnamkomesha, leo yupo free ktk namna ambayo hamkutegemea, kumbukeni mwanasiasa na yeye hiyo ndiyo kazi na tegemeeni Kuna siku atarejea kwenye system tena yamkini ktk mamlaka makubwa tu, mtakimbilia wapi? Kesi yake mliibumba
 
Hizo mahakama za mitandaoni sidhani kama zitaweza kumletea athari yeyote ni za kujifurahisha tu, huko mtaani watu wanahukumiana hata kwa kuiba kuiba buku tu ila sio kutoa hukumu kwa mafisadi au waharibu wakubwa.
 
Katiba mpya sio suluhisho, suluhisho is mind your own business, lea watoto, mche Mungu, ngoja siku ziishe uende kwa Baba.
Hata mm Nina hiyo mentality lkni at the end of the day watakufuata tu hata kama umejitenga nao.government overreach is all encompassing,as long you live in the same country,they will come for you if not affect the way you live.
 
Sabaya siyo muhaini mkuu, uhaini ni moja ya capital offences nchini, kosa ambalo adhabu zake ni nzito kwelikweli, na kesi ya mtuhumiwa wa makosa ya namna hii huwa inaendeshwa kwa umakini wa hali ya juu.

Labda useme tu kwamba Sabaya hastahili kugombea nafasi za uongozi kwasababu ana criminal record (rekodi ya kihalifu) ambayo huwa inam-disqualify mtu kugombea nafasi kadha wa kadha, ingawa Sabaya kupitia kwa Mawakili wake anaweza kukata rufaa Ili Mahakama ya juu itazame kwa upya kama kweli alikuwa na hatia na alistahili adhabu hiyo, Mahakama ya rufaa (ya juu) ikitengua kosa na adhabu basi Sabaya anaweza ku-qualify tena. The same was done by Sugu.

Kwa sasa ni hayo tu.
Ok
 
Hata mm Nina hiyo mentality lkni at the end of the day watakufuata tu hata kama umejitenga nao.government overreach is all encompassing,as long you live in the same country,they will come for you if not affect the way you live.

Solution yake: "Mche Mungu, the only powerful organ over any oppression is God himself" - solution tayari, achana na unafki wa hawa watu kabisa.
 
Walisema wanamuweka ndani kwaajili ya usalama wake.

Na wameamua kumtoa nje?🤔
 
Hakuwa na hatia au kumbukumbu zako zipo makalioni!
Makalio ya Sugu alipokuwa Jela

Kumbe hata huelewi Rufaa ilisikilizwa na kuamliwa lini

Nyie Bavicha ni weupe saba ndio sababu Nondo ya ACT Wazalendo inawasugueni Kweli kweli
 
For any one who believes kuna mahakama huru Tanzania, anapaswa akapimwe.this country is rotten to the core...I am not here to argue kama Ole Sabaya ana hatia au la,lakini ebu imagine kuishi kwenye nchi ambayo unaweza ukafungwa muda wowote kwa kosa lolote na wenye mamlaka.. Au mamlaka ikamwaachia mfungwa yoyote mwenye kosa lolote akarudi uraiani.

Yani so called 'child predators' waliopewa kifungo cha maisha waliachiwa awamu iliyopita, 'waporaji/majambazi' kama Sabaya wanafungwa vifungo vya nje, 'magaidi' kama kina Mbowe wanafunguliwa kesi na kusamehewa na kurudi kwenye majukwaa ya siasa kimasikhara, 'mafisadi' wanapewa adhabu za kufagia hospitali baada ya kusamehe Kodi za serikali Bil. 12,huku wezi wa Kuku wakifungwa miaka 3+...what is what?

Hawa jamaa wanatengeneza narrative Kila siku wakijua zile za nyuma tushasahau..alafu mijitu inasema katiba mpya ndio suluhisho..Suluhisho Gani wakati itaendelea kusimamiwa na judicial system ileile.
Tuendelee kuimba bia tamu..anyway silaumu Sana ,our average iq is 71
Huyu kaachiwa ili kuzima mvumo wa moto wa ripoti ya CAG...Sidhani kama ni coincidence

Ila yote unayoyasema ni kweli tupu. The whole country is rotten to the core...hakuna mfumo au taasisi hata moja inayoendeshwa kwa weledi, haki na uhuru!
 
Back
Top Bottom