Leo ilipaswa kuwa mwaka 2031, Error katika upangaji wa Calender imetufanya tuwe 2024

Kwanza kabisa, vitu haviko perfect. Watu wanazeeka, wanaumwa, wanakufa.Wanajamba, wanakunya, wanapata njaa. Vitu vinaoza. Hiyo si perfection.

Pili, vitu kuwa perfect si uthibitisho kwamba Mungu yupo, ni uthibitisho kwamba vitu viko perfect. Ukimuingiza Mungu hapo ni non sequitur logical fallacy.

Tatu, kama vitu kuwa na complexity ni ushahidi kuwa vimeumbwa, huyo Mungu naye ni complex, yeye naye kaumbwa ?

Hiyo hoja yako inathibitisha Mungu hayupo, haithibitishi Mungu yupo.
 
Sasa kuziba pua kunathibitishaje Mungu yupo?

Ukiziba pua hivyo utakufa.

Kifo ni uthibitisho kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Hoja yako ni uthibitisho kwamba Mungu hayupi, si uthibitisho kwamba Mungu yupo.
 
Kwa nini tuanze kuhesabu miaka tangu alipozaliwa Yesu?
Roma Locuta, Causa Finita
Kwa vyovyote kwa kuwa wote tupo katika sayari moja na ulimwengu mmoja, ilikuwa ni lazima kutafuta standard moja. Wenye akili zao wakapanga standard za kutumika, wasio na akili wakalazimika kufuata standard hizo
 
Kwa hiyo umekubali kwamba hii ni mipango ya watu tu, na hizo habari za Mungu kuwapo ni sehemu ya habari hiyo hiyo ya kutaka kuwapangia watu wote wafuate standard moja tu?
 
Kwa hiyo umekubali kwamba hii ni mipango ya watu tu, na hizo habari za Mungu kuwapo ni sehemu ya habari hiyo hiyo ya kutaka kuwapangia watu wote wafuate standard moja tu?
upangaji wa calender hauna uwezo wowote wa kuonyesha kwamba Mungu yupo au Hayupo,
Yaani hakuna uhisiano kabisa. hata ingekwepo calender moja,
 
Kwa hiyo umekubali kwamba hii ni mipango ya watu tu, na hizo habari za Mungu kuwapo ni sehemu ya habari hiyo hiyo ya kutaka kuwapangia watu wote wafuate standard moja tu?
Tuliumbwa na Mungu kuwa na utashi wa kuyatawala mazingira yetu

Mwanzo 1:27-28
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
 
upangaji wa calender hauna uwezo wowote wa kuonyesha kwamba Mungu yupo au Hayupo,
Yaani hakuna uhisiano kabisa. hata ingekwepo calender moja,
Kwa sababu Mungu mjuzi wa yote mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwapo, kusingekuwa hata na haja na kuonesha Mungu yupo.

Kwa sababu kila mtu angejua Mungu yupo bila utata, kufundishwa wala mjadala.
 
Hatujaumbwa na Mungu na hatuyatawala mazingira yetu.

Na hiyo Biblia unayoinukuu ni kitabu kimeandikwa na watu tu, kina uongo mwingi sana. Nikikuwekea msururu wa contradictions zilizo ndani ya Biblia huwezi kuzimaliza kuzitatua.

Bisha.
 
Sasa kuziba pua kunathibitishaje Mungu yupo?

Ukiziba pua hivyo utakufa.

Kifo ni uthibitisho kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Hoja yako ni uthibitisho kwamba Mungu hayupi, si uthibitisho kwamba Mungu yupo.
Bado hujafanya nilichokuambia fanya kwanza halafu urudi tena
 
Bado hujafanya nilichokuambia fanya kwanza halafu urudi tena
Wewe huwezi kufanya fikra dhahania.

Hata nikifanya hicho ulichoniambia, hakitathibitisha Mungu yupo, kitathibitisha Mungu hayupo.

Unaelewa hilo?
 
Wewe huwezi kufanya fikra dhahania.

Hata nikifanya hicho ulichoniambia, hakitathibitisha Mungu yupo, kitathibitisha Mungu hayupo.

Unaelewa hilo?
Nakuapia ukifanya lazima utapata jibu hiyo ni practical based evidence ya kujua kama kweli kuna Mungu au hakuna fanya uone
 
Hatujaumbwa na Mungu na hatuyatawali mazingira yetu.
Na hiyo Biblia unayoinukuu ni kitabu kimeandikwa na watu tu, kina uongo mwingi sana. Nikikuwekea msururu wa contradictions zilizo ndani ya Biblia huwezi kuzimaliza kuzitatua.
Bisha.
Sihitahi kubishana. Endelea tu kupinga uamuzi wa kuhesabu miaka kwa utaratibu wa BC na AD. Mimi kwa elimu yangu ya hesabu, unapozungumzia magnitude ya fundamental quantities of physics, ni lazima uwe na reference point. Mass, Time na Length huwezi kuziexpress bila reference. Hawa walioamua kupima miaka (Time), waliona reference yao iwe ni mwaka wa kuzaliwa Kristu. Unaruhusiwa pia kutafuta namna tofauti ya kuelezea hilo, lakini fundamental quantities za physics zitabaki kuwa ni Mass, Time na Length. Ni sawa tu na convention ya boiling point ya maji kuwa 100 oC, au density ya maji kuwa 1g/cc
 
Kwa sababu Mungu mjuzi wa yote mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwapo, kusingekuwa hata na haja na kuonesha Mungu yupo.

Kwa sababu kila mtu angejua Mungu yupo bila utata, kufundishwa wala mjadala.
mimi nikichogundua, ni kua wewe unahitaji kuona vitu fulani kama hivyo unavyosema ndo uamini yupo, ila sasa Mungu yeye ana namna yake nyingine kabisa ambayo wewe kwa ulivyotaka iwe ndo haiendani,

hata hivyo akili ya binadamu japo unaweza kuona umefikiria kwa kina hadi mwisho, kumbe ndo inapoweza kuishia lakini vitu vingine vinahitaji ufikiri beyond and beyond ambapo pia kwa capacity ya ubongo wa binadamu haiwezekani

ndo maana wanasayansi kuna mambo mengi hawawezi kuyaelezea na hawajui mechanisim yake,

hawawezi hata kuzuia mtu asizeeke, hawawezi kutengeneza hata seli moja ikafanya kazi,

ukishindanisha ufahamu wako na kuweka conclusion hivo ni kama kushindanisha maji ya kwenye kikombe au bakuli na bahari

Mwanadamu amepewa akili ili aweze kuyatawala mazingira yake, ila pia ina limit yake sanasana inafanya vitu kutokana na experience na memory,

ila vitu ambavyo hawezi kugi experience physically kama uwepo wa Mungu,
ndo hapo kunakua na ubishani.
 
CHAI
 
Kitu cha msingi kabisa ni kwamba, napinga uwepo wa Mungu si kwa sababu mimi nataka kuona vitu fulani.

Hili si suala langu mimi binafsi, hizi ni hoja zilizokuwepo maelfu na maelfu ya miaka kabla mimi sijazaliwa.

Ni suala la logical consistency. Unaelewa logical consistency ni nini?

Yani imeandikwa Mungu yupo, mtaona cha bluu, halafu mnaona chekundu, hamuoni cha bluu. Mnahoji, mbona tuliambiwa tutaona cha bluu halafu tunaona chekundu, huyo Mungu yupo kweli?

Hapo nikihoji, si suala langu tu, ni suala la logical consistency.

Mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo.
 
Hata habari ya reference ya mwaka wa kuzaliwa Kristu wamekosea.

Ndiyo point ya uzi huu.

Na wamekosea kwa sababu hizi ni habari za watu tu, Mungu hayupo. Angekuwapo, angewaongoza wasikosee tangu mwanzo.
 
ahaa kumbe wewe umeamua tu kuamini hayupo kwasababu ya logic

kuna vitu vingi sayansi haina Majibu

hili ni mojawapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…