Wadau kama alivyozungumza JJ Mnyika kwamba tujitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura. Jambo la kwanza ni kwamba kura hazitopigwa kama mawakala wa vyama vya upinzani "MAKINI"(Nasema upinzani makini maana kuna wapinzani kina TLP, NCCR, UDP ambao ni CCM-A,B na C) hawatoruhusiwa kuingia kwenye vituo vya kura, tujiandae kwa nguvu ya umma, najua Hai, Mbeya, Iringa, Arusha, Misungwi na kanda maalumu huko hakuna shida "FITA ni FITA" kule mapema asubuhi wanakiwasha wakiletewa utopolo, ila sehemu nyingine makatibu na wenyeviti wa majimbo CHADEMA sisitizeni kwamba mwaka huu ni mwisho kuonewa; hawawezi kufanya chochote polisi maana uchaguzi huu unaaangaliwa na dunia nzima,wakivuruga uchaguzi hakika ICC itawahusu.