macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Mkuu kama ni aina ya transaction ilichopitishwa na benki basi inatakiwa iwe safe features zote na namna ya kufuatilia matukio kama haya. I mean kama wanaona wateja wengi wanapigwa kwa njia hii, basi waiondoe.Hela yako utapata bila wasiwasi Ila usipendee kutoa hela Kwa wakala tumia zaidi sm banking
Pesa imetoka baada ya kama lisaa kimoja na nusu baada ya Mimi kuondoka Kwa wakalaMkuu, utathibitishaje sasa kuwa hukupewa hiyo 1m?
AnashindajeNenda polisi haraka sanaaa! Hiyo kesi wakala anashinda mchana kweupee ukizembea.
Atadhibitisha kwa kuonyesha kuchelewa kwa msg ya kutoa pesa kuingia kwenye simu yake.Mkuu, utathibitishaje sasa kuwa hukupewa hiyo 1m?
Utathibitishaje kuwa uliondoka hilo saa moja na nusu ndipo pesa ikatoka?? Yaani utathibitishaje kuwa hukuwepo hapo wakati pesa inatoka?Pesa imetoka baada ya kama lisaa kimoja na nusu baada ya Mimi kuondoka Kwa wakala
Wewe ndiye uliweka namba ya siri kudhibitisha muamala☺️Anashindaje
Wenyewe wamethibitisha kua kweli kulikua na shida ya mtandao, kuna miamala ilitoka badae, sasa wewe unabishana na CRDB wenyewe? Au hujasoma ukaelewaUtathibitishaje kuwa uliondoka hilo saa moja na nusu ndipo pesa ikatoka?? Yaani utathibitishaje kuwa hukuwepo hapo wakati pesa inatoka?
🤣🤣🤣🤣🤣 Ushawahi kutoa pesa Kwa wakala? ndio niliweka na lazima uweke, inawezekana hata hujawah kutumia hizo huduma hujui hata nini kinazungumzwa hapaWewe ndiye uliweka namba ya siri kudhibitisha muamala☺️
mpaka sasa hajapata meseji ya kuonesha kuwa ametoa Tshs. 1,000,000/=Atadhibitisha kwa kuonyesha kuchelewa kwa msg ya kutoa pesa kuingia kwenye simu yake.
Inaeleweka wakala hatoi pesa mpaka msg irudi.
Pia kuwasilisha malalamiko yake CRDB Itamsaidia.
Akizembea iitakula kwake lakini.
Wewe subiri Jumatatu uone kama watafungua. Ukienda polisi sasa hivi utapoteza muda bure.Yani sielewi maana nmewapigia CRDB wakaniambia labda kwakua ni weekend ndio mana wamefunga, niende jumatatu kama sijafanikiwa niwajulishe, maana wanasema account ya huyo wakala IPO vizuri tuu na ni MTU anafanya miamala
Anashindaje
Wakala nikampa Kadi akauliza kiasi, nikamwambia atoe laki1, akanipa mashine nikaweka namba ya siri
Nimesoma na kuelewa vizuri, mimi nakuuliza wewe maswali ili utetee vyema hoja yako.Wenyewe wamethibitisha kua kweli kulikua na shida ya mtandao, kuna miamala ilitoka badae, sasa wewe unabishana na CRDB wenyewe? Au hujasoma ukaelewa
Ndio maana umetapeliwa sababu haupo makini, unashindwa kung'amua kua haya maswali hata huko polisi utaulizwa na sisi tupo hapa kukuchallenge ili ujiandae na majibu utakayoulizwa huko.🤣🤣🤣🤣🤣 Ushawahi kutoa pesa Kwa wakala? ndio niliweka na lazima uweke, inawezekana hata hujawah kutumia hizo huduma hujui hata nini kinazungumzwa hapa
Huyu jamaa ni m'bishi sana.Nimesoma na kuelewa vizuri, mimi nakuuliza wewe maswali ili utetee vyema hoja yako.
Hapa suala la kuwahi au kuchelewa kwa muamala sio ishu, maana mfano ungesubiri mpaka huo muda fedha imetoka, si ungeichukua, je kungekuwa na mgogoro wowote?? Jibu ni hapana
Sasa kwa kuwa hukuichukua, hoja ni namna ya kuthibitisha kuwa hukuichukua. Kama kungekuwa na camera ingekua rahisi sana ila kama hakuna camera, ni kipi kitakufanya wewe uaminike na sio wakala, incase akisema kuwa fedha ilivyotoka ulikuwepo na alikukabidhi!!
Nahuyu namsubiria, labda asifungue na Kesho naenda POLISI, watu kama nyie ndio napenda maoni yenu maana mnajua ninachokiongelea, wengine hawaelewi kituHuyo dogo tu anataka kukupiga.
Iliwahi nitokea hiyo kwa wakala wa nmb,mbona alinipa pesa yangu tu bila shida
Mkuu pengine hujaelewa sajo anachojaribu kusema. Nadhani anasema kama huyo wakala atasema ulisubiri mpaka muamala ukakamilika na akakupa fedha zako ukaondoka, unaweza kuthibitishaje kuwa hukupewa? Na mbaya zaidi anaweza kuweka na shahidi wa uongo. Ni nadharia ya mtu kukukana kwa kitu cha ukweli. Kwa mfano mimi niliwahi kumlipa mtu fedha ya kibarua alichofanya kwa siku moja. Kesho yake akakana macho makavu na akasema hukunipa na kama ulinipa lete ushahidi. Nlikwama kwa sababu sikuandika popote ili asaini na pia hakukuwa na shahidi. Anyway, japo jambo kama hili ni nadra kutokea lakini ni vizuri kupanua mjadala.Wenyewe wamethibitisha kua kweli kulikua na shida ya mtandao, kuna miamala ilitoka badae, sasa wewe unabishana na CRDB wenyewe? Au hujasoma ukaelewa