Ndugu zangu Watanzania,
Leo Tarehe 7 October Ndio siku aliyozaliwa Jabali na Nguli wa siasa Za ndani na nje ya Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete.Ni mwamba kweli kweli wa siasa,Ni fundi wa siasa aliyekulia katika siasa na anayezijuwa siasa. Ni mwanamikakati mzuri sana na mwenye mipango ya ushindi na ushawishi katika siasa. Ni mwenye historia ya kuvutia kisiasa inayotufundisha vijana subiri na uvumilivu katika safari yoyote ile kisiasa. Ni kiongozi wa mfano Barani Afrika Na Dunia nzima kwa ujumla.
Ni waziri wa mambo ya nje aliyehuduma kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa sana kwa Taifa letu,Ni wakati wake ambapo vijana wengi sana walipenda na kujiingiza katika siasa,ni wakati wake ambapo demokrasia ilichanua katia Taifa letu,Ni wakati wake ambapo Taifa letu lilipokea viongozi wote wakubwa katika ulimwengu huu,na kwa wakati fulani tumewahi kupokea kwa wakati mmoja Rais aliyepo madarakani na aliyestaafu kutoka Taifa la Marekani, ni wakati wake Elimu ya chuo kikuu vijana wengi sana waliipata bila kikwazo,ni wakati wake ajira watu walikuwa wanachagua waende private au serikalini,ni wakati wake ambapo miundombinu ya barabara ilijengwa kila kona ya Taifa letu na ni wakati wake mtu akipangiwa ajira kijijini haendi kwa kuwa private alikuwa na uhakika wa kupata ajira.
Ni wakati wake shule za kata zilijengwa sana na kutoa nafasi kwa wanafunzi wengi sana kupata na kutimiza ndoto ya kupata Elimu ya sekondari,ni wakati wake huduma za afya zilisogezwa karibu ya watanzania,Ni wakati wake Biashara zilishamiri sana nchini,ni wakati wake vijana wengi sana walipata nafasi ya kuaminiwa kushika nafasi kubwa serikalini na hata katika mashirika ya umma na Taasisi mbalimbali,Ni wakati wake na kwa ushawishi wake Tulishuhudia mh Dr Asha Rose migiro akiwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa chini ya Ban kin moon aliyekuwa Rafiki yake na mh Kikwete.
Ni kupitia yeye viongozi mbalimbali aliwakuza ambao mpaka leo wapo serikalini na wanaendelea kulitumikia Taifa letu katika nyadhifa mbalimbali. Alikuwa fundi wa kuibua vipaji vya vijana ,hakuwa na hiyana katika kuwapatia nafasi vijana. Leo viongozi wengi ni kazi ya mikono yake na macho yake ya kuwaona na kuwapatia nafasi ya uongozi.
Ni Dr Jakaya Mrisho Kikwete aliyenishawishi kuipenda siasa na chama cha Mapinduzi mwaka 2005 mkoani Rukwa katika mji mdogo wa Laela wilaya ya sumbawanga vijijini alipokuja katika kampeni za kuomba kura za urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Kwa hakika Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia Maisha Marefu yenye heri na baraka tele kwake.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.