Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
RIPHuyu mzee ndio kawakomboa vijana wengi Waweze kujiajiri kupiita bodaboda na kuajiri kuliko Marais wote hakika huyu angeongezewa Miaka ya kuongoza kuliko kutuletea bwana yule.
Mzee katimiza 70's hv haiwezekani akagonbea tena 2025?
Uzi umekwisha.View attachment 2774547
"Kifo ni mipango ya Mungu tuombeane mema" Philip Mpango
[emoji1]Nasikia kwenye yale masuala ya kimasihara, mzee katembeza sana rungu kwa hawa wakinamaza na wakina dada Shobodundo na viherehere
+1 kwake
Hongera sana mzee!! Mungu akuongezee miaka mingine kama hiyo!Mhe. Kikwete amewaleta kwenye uwanja wa siasa vijana na wazee wengi wanaongara leo.
Lakini wasipokumbishwa kumtakia happybithday huyu father may be wanaweza kupotezea.
Sisi jukumu letu nikuwakumbusha kuandika hata KINAFIKI kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kwamba mzee kazaliwa. Naona wanasiasa wengi wamepotezea kuzaliwa kwa huyu dingi .
Happybithday Baba Riz
Huyu aliuza gas yetu kwa wazungu sina hamu yeye.Mhe. Kikwete amewaleta kwenye uwanja wa siasa vijana na wazee wengi wanaongara leo.
Lakini wasipokumbishwa kumtakia happybithday huyu father may be wanaweza kupotezea.
Sisi jukumu letu nikuwakumbusha kuandika hata KINAFIKI kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kwamba mzee kazaliwa. Naona wanasiasa wengi wamepotezea kuzaliwa kwa huyu dingi .
Happybithday Baba Riz
Siyo Putin kafoji vyeti? Kama Yule kiongozi wa YUVISISIEMU😂😂Kumbe anamzidi umri Putin!
Ungeandika hili bango ukabandike pale chalinze njia panda ya msoga ingependeza zaidi.Ndugu zangu Watanzania,
Leo Tarehe 7 October Ndio siku aliyozaliwa Jabali na Nguli wa siasa Za ndani na nje ya Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete.Ni mwamba kweli kweli wa siasa,Ni fundi wa siasa aliyekulia katika siasa na anayezijuwa siasa. Ni mwanamikakati mzuri sana na mwenye mipango ya ushindi na ushawishi katika siasa. Ni mwenye historia ya kuvutia kisiasa inayotufundisha vijana subiri na uvumilivu katika safari yoyote ile kisiasa. Ni kiongozi wa mfano Barani Afrika Na Dunia nzima kwa ujumla.
Ni waziri wa mambo ya nje aliyehuduma kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa sana kwa Taifa letu,Ni wakati wake ambapo vijana wengi sana walipenda na kujiingiza katika siasa,ni wakati wake ambapo demokrasia ilichanua katia Taifa letu,Ni wakati wake ambapo Taifa letu lilipokea viongozi wote wakubwa katika ulimwengu huu,na kwa wakati fulani tumewahi kupokea kwa wakati mmoja Rais aliyepo madarakani na aliyestaafu kutoka Taifa la Marekani, ni wakati wake Elimu ya chuo kikuu vijana wengi sana waliipata bila kikwazo,ni wakati wake ajira watu walikuwa wanachagua waende private au serikalini,ni wakati wake ambapo miundombinu ya barabara ilijengwa kila kona ya Taifa letu na ni wakati wake mtu akipangiwa ajira kijijini haendi kwa kuwa private alikuwa na uhakika wa kupata ajira.
Ni wakati wake shule za kata zilijengwa sana na kutoa nafasi kwa wanafunzi wengi sana kupata na kutimiza ndoto ya kupata Elimu ya sekondari,ni wakati wake huduma za afya zilisogezwa karibu ya watanzania,Ni wakati wake Biashara zilishamiri sana nchini,ni wakati wake vijana wengi sana walipata nafasi ya kuaminiwa kushika nafasi kubwa serikalini na hata katika mashirika ya umma na Taasisi mbalimbali,Ni wakati wake na kwa ushawishi wake Tulishuhudia mh Dr Asha Rose migiro akiwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa chini ya Ban kin moon aliyekuwa Rafiki yake na mh Kikwete.
Ni kupitia yeye viongozi mbalimbali aliwakuza ambao mpaka leo wapo serikalini na wanaendelea kulitumikia Taifa letu katika nyadhifa mbalimbali. Alikuwa fundi wa kuibua vipaji vya vijana ,hakuwa na hiyana katika kuwapatia nafasi vijana. Leo viongozi wengi ni kazi ya mikono yake na macho yake ya kuwaona na kuwapatia nafasi ya uongozi.
Ni Dr Jakaya Mrisho Kikwete aliyenishawishi kuipenda siasa na chama cha Mapinduzi mwaka 2005 mkoani Rukwa katika mji mdogo wa Laela wilaya ya sumbawanga vijijini alipokuja katika kampeni za kuomba kura za urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Kwa hakika Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia Maisha Marefu yenye heri na baraka tele kwake.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
Teh tehAkumbuke tu kutubu dhambi za wizi na nyinginezo.
Tunakumbushana tu kisela.
Dogo, hakuna kiongozi makini duniani nyakati hizi kama Putin. Hawezi kuwa na kashfa za kipumbavu kama hizo.Siyo Putin kafoji vyeti? Kama Yule kiongozi wa YUVISISIEMU😂😂