Leo naomba niongee na wewe brother unaetaka kuoa. Ongea na wakubwa

Leo naomba niongee na wewe brother unaetaka kuoa. Ongea na wakubwa

AXIOM APEX VERBOSE

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
13,769
Reaction score
23,676
Kwanza naomba kwa nitakae mchukiza kwa hiki ninachoenda kukiandika hapa tusameheane ila nitasema ukweli na ukweli tupu sitosema uongo.

Niende moja kwa moja, kwanza brother huyo binti au mwanamke kabla hujamuoa hakikisha unamjua vizuri nje ndani.

Sio unamjua juu juu tu kisha unapapatika kutaka kumuoa chukua muda kumjua vizuri. Usikurupuke milio ya waliokurupuka sasa hivi wanasaga meno kwa sababu walikurupuka.

Mbili ni kwamba kabla hujamuoa huyo binti au mwanamke onana na wakubwa upande wa kiume yaani wanaume wanaomuona na wanaoishi na huyo binti au mwanamke ili wakupe ABC zake mapema.

Unanielewa ninapokwambia onana na wakubwa na uongee nao namaanisha nini?

Huyo binti au mwanamke lazima atakua na watu upande wa kiume anaoishi nao anapoishi sio lazima awe kaka yake au mjomba wake au ndugu yake yoyote wa kiume anaweza akawa jamaa tu hapo mtaa wa pili nyumba jirani ila anamjua vizuri tu huyo mwanamke au huyo binti na wewe haumjui hivyo km jinsi yeye anavyomjua.

Ukionana nae atakupa ABC zake zote. Ishanitokea nikapewa ABC za binti kuanzia siku hio nikawa makini sana ninapoleta suala la mahusiano kwenye meza yangu ya majadiliano binafsi. Niamue nini na nini nisiamue au nijilipue nitajua mbele ya safari?

Usioe huyo binti km hujaongea na upande wa kiume wanaomjua huyo binti vizuri ili wakupe ABC zote mapema na wewe utaamua jinsi ya kupambana nazo. Sio lazima awe kaka, mjomba au Baba yake.

Imetokea kuna bwana kaoa muda kidogo, sasa imepita miaka km mitatu hivi ila ndani ya miaka miwili bwana yule alianza kutoa milio ndani ya nyumba mwanamke ndio kageuka kubwa la maadui nyumbani hapakariki tena nyumba anaiona chungu mbichi. Baba wa mtoto wa kike ndio anafikishiwa malalamiko kuhusu binti yake na hua anaenda mara kwa mara kwenda kusuruhisha ugomvi wa binti yake na jamaa.

Alichokosea jamaa pale mwanzoni kabisa kabla ya kuoa hakuonana na wakubwa wakampa ABC za mwanamke huyu yupo hivi na hivi na hivi kwa hio utajua mwenyewe unaishi nae vipi ila sisi wakubwa zake tunaomjua ndio tunakwambia hivyo kwa hio shauri ni lako utaamua unaoa au unaghairisha kuoa.

Mwisho, neno langu hili hapa sio sheria kwa hio utaamua wewe unafuata au haufuati, huo ni uamuzi wa kwako ila nimekwambia mapema kabisa hata hiki kidogo wasichokwambia hao wanaokuficha.

Ongea na wakubwa zungumza na wakubwa kabla jumba bovu halijakuangukia.

Nimemaliza
 
mmmh 😀😀😀watu hawahawa ambao wanawachukia watu bila sababu wooi
Sio wote ila wapo ambao watakwambia ukweli sio chuki ila ukweli utaamua wewe uchukue kipi uache kipi hii ni kwa upande wa wanaume wanawake hii sidhani km itawahusu sana ila nimeandika kwa ajili ya wanaume sababu nimeona jamaa anapata tabu sasa hivi ambayo angeiepuka miaka mitatu nyuma huko ila leo anatamani muda urudi nyuma na ndio kashaingia kwenye mfumo tayari
 
Sio wote ila wapo ambao watakwambia ukweli sio chuki ila ukweli utaamua wewe uchukue kipi uache kipi hii ni kwa upande wa wanaume wanawake hii sidhani km itawahusu sana ila nimeandika kwa ajili ya wanaume sababu nimeona jamaa anapata tabu sasa hivi ambayo angeiepuka miaka mitatu nyuma huko ila leo anatamani muda urudi nyuma na ndio kashaingia kwenye mfumo tayari
Huyo jamaa anakumbana na changamoto zipi
 
Ukitaka kuishi vizuri na binadamu yyte kuwa na nguvu kumzidi. Kula vizuri utune kisha mazoezi (hasa kung Fu au boxing).

Mambo ya kutaka watu/wake wawe watakatifu achana nayo.Binadamu si mkamilifu ila akiona nguvu iliyopo ataku heshimu.

Hiyo point Yako kufanya research siipingi ni mkakati mzuri.
 
Back
Top Bottom