Leo naomba niongee na wewe brother unaetaka kuoa. Ongea na wakubwa

Leo naomba niongee na wewe brother unaetaka kuoa. Ongea na wakubwa

Kikawaida niceguys ndio wanaopelekeshwa na kitu kidogo kiitwacho mapenzi

Kitu ambacho unaweza kuamua kumuacha mtu ukaendelea na maisha yako bila kuathirika.
Kama ni kutafuta mwanamke mwingine wamejaa huko mabarabarani, makanisani, masokoni, mitandaoni.
Sasa kipi kinafanya watu waumizww na mapenzi?

Niceguys kwao mapenzi ni hisia.
Alphamale kwao Mapenzi ya uamuzi tuu.

Wanaweza kuamua kuchagua kupenda na hapo hapo wakaamua kufukuza mtu asiyefit matakwa yake
Hapa umeusema ukweli mkuu ndio maana nikasema ongea na wakubwa kabla hujaingia mto ulijaa Mamba utaliwa na Mamba ongea na wakubwa wakwambie km huo mto unaotaka kuuvuka ni salama au la badirisha njia mbele kuna daraja la juu nenda kavuke kule hapo kuna Mamba, ushanielewa sio kanisani sio bar sio barabarani sio wapi ongea na wakubwa wakupe ABC kabla haujavuka
 
Yeah watu hubadilika kulingana na mazingira na watu wanaoishi nao. Unaweza kutoa mfano
ndio mifano ni mingi, lakini nitatoa endapo mleta mada atasema hao upande wa kiume wa majirani,tunawauliza kitu gani kuhusu binti? Je tunawauliza kuhusu tabia,uchapakazi au ?
 
Kwanza naomba kwa nitakae mchukiza kwa hiki ninachoenda kukiandika hapa tusameheane ila nitasema ukweli na ukweli tupu sitosema uongo.

Niende moja kwa moja, kwanza brother huyo binti au mwanamke kabla hujamuoa hakikisha unamjua vizuri nje ndani.

Sio unamjua juu juu tu kisha unapapatika kutaka kumuoa chukua muda kumjua vizuri. Usikurupuke milio ya waliokurupuka sasa hivi wanasaga meno kwa sababu walikurupuka.

Mbili ni kwamba kabla hujamuoa huyo binti au mwanamke onana na wakubwa upande wa kiume yaani wanaume wanaomuona na wanaoishi na huyo binti au mwanamke ili wakupe ABC zake mapema.

Unanielewa ninapokwambia onana na wakubwa na uongee nao namaanisha nini?

Huyo binti au mwanamke lazima atakua na watu upande wa kiume anaoishi nao anapoishi sio lazima awe kaka yake au mjomba wake au ndugu yake yoyote wa kiume anaweza akawa jamaa tu hapo mtaa wa pili nyumba jirani ila anamjua vizuri tu huyo mwanamke au huyo binti na wewe haumjui hivyo km jinsi yeye anavyomjua.

Ukionana nae atakupa ABC zake zote. Ishanitokea nikapewa ABC za binti kuanzia siku hio nikawa makini sana ninapoleta suala la mahusiano kwenye meza yangu ya majadiliano binafsi. Niamue nini na nini nisiamue au nijilipue nitajua mbele ya safari?

Usioe huyo binti km hujaongea na upande wa kiume wanaomjua huyo binti vizuri ili wakupe ABC zote mapema na wewe utaamua jinsi ya kupambana nazo. Sio lazima awe kaka, mjomba au Baba yake.

Imetokea kuna bwana kaoa muda kidogo, sasa imepita miaka km mitatu hivi ila ndani ya miaka miwili bwana yule alianza kutoa milio ndani ya nyumba mwanamke ndio kageuka kubwa la maadui nyumbani hapakariki tena nyumba anaiona chungu mbichi. Baba wa mtoto wa kike ndio anafikishiwa malalamiko kuhusu binti yake na hua anaenda mara kwa mara kwenda kusuruhisha ugomvi wa binti yake na jamaa.

Alichokosea jamaa pale mwanzoni kabisa kabla ya kuoa hakuonana na wakubwa wakampa ABC za mwanamke huyu yupo hivi na hivi na hivi kwa hio utajua mwenyewe unaishi nae vipi ila sisi wakubwa zake tunaomjua ndio tunakwambia hivyo kwa hio shauri ni lako utaamua unaoa au unaghairisha kuoa.

Mwisho, neno langu hili hapa sio sheria kwa hio utaamua wewe unafuata au haufuati, huo ni uamuzi wa kwako ila nimekwambia mapema kabisa hata hiki kidogo wasichokwambia hao wanaokuficha.

Ongea na wakubwa zungumza na wakubwa kabla jumba bovu halijakuangukia.

Nimemaliza
Uzi bila picha ni batili kabisa,tena uzi bila kisa cha kweli chako binafsi ama kusimuliwa ni batili zaidi.
Kingine punguza ushauri mambo ya kuchunguzana peleka kwenye kitchen party!
We kina Elon musk wanakuwa ma tilioenea uko bize na ushauri wa mapenzi na ushauri wenyewe hauna kichwa wala miguu
Don't take it personal!
SHUBAMIT!
 
Hyo ilikua Zamani kwa sasa hvi movement zimekua nyingi ni ngumu kua na taarifa za watu in full.

Haiwezekani Binti alitoka Same akiwa bikra wa miaka 16/17 akaja UDSM kusomea Degree ya ualimu, anamaliza anaenda kufanya kazi mwanza, Halafu wewe utuambie tufatr taarifa zake SAME kwa boda boda huoni hizo taarifa ni outdated?

Bitches utawajua tu, Na kila mtu anae oa hua anajua kabisa hapa pangu pakavu, ila sasa moyo ni nn bhana unakwambia ukimuweka ndani utammudu.
 
ndio mifano ni mingi, lakini nitatoa endapo mleta mada atasema hao upande wa kiume wa majirani,tunawauliza kitu gani kuhusu binti? Je tunawauliza kuhusu tabia,uchapakazi au ?
Vyote ongea nao watakwambia tu sisi binadamu tuna kawaida moja utanyiwa hata chakula ila hakuna mtu atakunyima maneno utapewa unayoyataka kuyasikia na usiyoyataka kuyasikia yote kwa ujumla wewe si unataka kuoa au? Haya pokea hivi ule wimbo wa wanaimba -huyo ni chaguo lako unauelewa maana yake unamaanisha nini? Umechagua mwenyewe pamoja na mabalaa yake utaishi nae hivyo hivyo sio baadae unaanza kutoa milio na tulikwisha kwambia kabla
 
Usiamini sana watu maana hubadilika kwa nyakati.
Hii ipo wazi ila hilo ni wewe kuamua utachagua kipi unafuata na kipi haufuati ila ulikwishaambiwa kabla kwamba hio njia unayoenda ina miiba ya kutosha na wewe upo pekupeku pita njia ile kule haina miba wewe ukakomaa na njia yenye miba mbele miiba imeanza kukuchoma miguuni unaanza kupiga mikelele sasa kelele za nini bro si ulisema njia zenye miiba hua zinabadirika huko mbele kiko wapi?
 
Hyo ilikua Zamani kwa sasa hvi movement zimekua nyingi ni ngumu kua na taarifa za watu in full.

Haiwezekani Binti alitoka Same akiwa bikra wa miaka 16/17 akaja UDSM kusomea Degree ya ualimu, anamaliza anaenda kufanya kazi mwanza, Halafu wewe utuambie tufatr taarifa zake SAME kwa boda boda huoni hizo taarifa ni outdated?

Bitches utawajua tu, Na kila mtu anae oa hua anajua kabisa hapa pangu pakavu, ila sasa moyo ni nn bhana unakwambia ukimuweka ndani utammudu.
Suala linarudi palepale najua kwenu kuna chumba chenye taa na pia kuna chumba chenye giza, akija mgeni akakwambia anataka kujua kuhusu tofauti ya chumba chenye taa na chumba chenye giza ni ipi najua lazima utakua na ABC za chumba chenye taa na chumba chenye giza hiki ndicho ninachomaanisha mimi km hujanielewa niambie nirudie kukuelekeza nipo tayari kufanya hivyo hata mara 100 usiponielewa nipo tayari kukuelekeza mpaka unielewe
 
Hii ipo wazi ila hilo ni wewe kuamua utachagua kipi unafuata na kipi haufuati ila ulikwishaambiwa kabla kwamba hio njia unayoenda ina miiba ya kutosha na wewe upo pekupeku pita njia ile kule haina miba wewe ukakomaa na njia yenye miba mbele miiba imeanza kukuchoma miguuni unaanza kupiga mikelele sasa kelele za nini bro si ulisema njia zenye miiba hua zinabadirika huko mbele kiko wapi?
Kuna jambo hulielewi,inawezekana ni kwasababu ya umri ulionao au lack of experience kuhusu haya mambo,

Mwanamke unaweza kuishi nae kwa miaka hata 10 ila akaja kukubadilikia,haya mambo hayana dhamana hata siku moja,

Mfano mzuri angalia kwa aliyekua mke wa Bill Gate,ipo mifano mingi sana.
 
ndio mifano ni mingi, lakini nitatoa endapo mleta mada atasema hao upande wa kiume wa majirani,tunawauliza kitu gani kuhusu binti? Je tunawauliza kuhusu tabia,uchapakazi au ?
Nafikiri atauliza history yake(Binti) kwenye mapenzi na ngono. Jinsi anavyo ishi na watu. Maadili yake. etc.
 
Back
Top Bottom