Leo naomba niongee na wewe brother unaetaka kuoa. Ongea na wakubwa

Leo naomba niongee na wewe brother unaetaka kuoa. Ongea na wakubwa

Kwanza naomba kwa nitakae mchukiza kwa hiki ninachoenda kukiandika hapa tusameheane ila nitasema ukweli na ukweli tupu sitosema uongo.

Niende moja kwa moja, kwanza brother huyo binti au mwanamke kabla hujamuoa hakikisha unamjua vizuri nje ndani.

Sio unamjua juu juu tu kisha unapapatika kutaka kumuoa chukua muda kumjua vizuri. Usikurupuke milio ya waliokurupuka sasa hivi wanasaga meno kwa sababu walikurupuka.

Mbili ni kwamba kabla hujamuoa huyo binti au mwanamke onana na wakubwa upande wa kiume yaani wanaume wanaomuona na wanaoishi na huyo binti au mwanamke ili wakupe ABC zake mapema.

Unanielewa ninapokwambia onana na wakubwa na uongee nao namaanisha nini?

Huyo binti au mwanamke lazima atakua na watu upande wa kiume anaoishi nao anapoishi sio lazima awe kaka yake au mjomba wake au ndugu yake yoyote wa kiume anaweza akawa jamaa tu hapo mtaa wa pili nyumba jirani ila anamjua vizuri tu huyo mwanamke au huyo binti na wewe haumjui hivyo km jinsi yeye anavyomjua.

Ukionana nae atakupa ABC zake zote. Ishanitokea nikapewa ABC za binti kuanzia siku hio nikawa makini sana ninapoleta suala la mahusiano kwenye meza yangu ya majadiliano binafsi. Niamue nini na nini nisiamue au nijilipue nitajua mbele ya safari?

Usioe huyo binti km hujaongea na upande wa kiume wanaomjua huyo binti vizuri ili wakupe ABC zote mapema na wewe utaamua jinsi ya kupambana nazo. Sio lazima awe kaka, mjomba au Baba yake.

Imetokea kuna bwana kaoa muda kidogo, sasa imepita miaka km mitatu hivi ila ndani ya miaka miwili bwana yule alianza kutoa milio ndani ya nyumba mwanamke ndio kageuka kubwa la maadui nyumbani hapakariki tena nyumba anaiona chungu mbichi. Baba wa mtoto wa kike ndio anafikishiwa malalamiko kuhusu binti yake na hua anaenda mara kwa mara kwenda kusuruhisha ugomvi wa binti yake na jamaa.

Alichokosea jamaa pale mwanzoni kabisa kabla ya kuoa hakuonana na wakubwa wakampa ABC za mwanamke huyu yupo hivi na hivi na hivi kwa hio utajua mwenyewe unaishi nae vipi ila sisi wakubwa zake tunaomjua ndio tunakwambia hivyo kwa hio shauri ni lako utaamua unaoa au unaghairisha kuoa.

Mwisho, neno langu hili hapa sio sheria kwa hio utaamua wewe unafuata au haufuati, huo ni uamuzi wa kwako ila nimekwambia mapema kabisa hata hiki kidogo wasichokwambia hao wanaokuficha.

Ongea na wakubwa zungumza na wakubwa kabla jumba bovu halijakuangukia.

Nimemaliza
Ushauri mzuri sana. Wengi wanaangalia ukubwa wa matakwo na uzuri wa nje. Ni afadhali usioe kabisa kuliko kuaoa mwanamke kilaza. Utapata taabu sana kijana.
 
Hii statement sio ya kweli. Mtaani tunaona nice guys ndio wanateswa zaidi na mapenzi.

Kikawaida niceguys ndio wanaopelekeshwa na kitu kidogo kiitwacho mapenzi

Kitu ambacho unaweza kuamua kumuacha mtu ukaendelea na maisha yako bila kuathirika.
Kama ni kutafuta mwanamke mwingine wamejaa huko mabarabarani, makanisani, masokoni, mitandaoni.
Sasa kipi kinafanya watu waumizww na mapenzi?

Niceguys kwao mapenzi ni hisia.
Alphamale kwao Mapenzi ya uamuzi tuu.

Wanaweza kuamua kuchagua kupenda na hapo hapo wakaamua kufukuza mtu asiyefit matakwa yake
 
watu hubadilika, hayanaga muongozo
Sio kweli ila wakubwa hawawezi kukuambia uongo hata km utasema watu wanabadirika na yes ni kweli watu hubadirika ila wakubwa watakwambia hayo ni wewe kuamua kwamba watu hubadirika

Ngoja nikwambie, kuna huyu binti tulitokea kua pamoja kwa kipindi kirefu kiasi cha kuaminiana ile sana akaanza kuniconnect na ndugu zake especially wa kiume mara kadhaa aakisema huyu ni kaka yangu

Sasa kuna kipindi alinitafuta kaka yake akitaka niongee nae kuhusu sister yake mimi sina hili wala sina lile, basi siku hio kapiga simu mimi nikajua labda ni binti ndio alienitafuta baada ya kuona missed call nikaenda hewani basi tukaongea vizuri na kijana anaitwa ISAYA ambae ni brother wa huyo binti safi

Sasa kijana akaanza kuona mimi mboni ni mtu mmoja mstaarabu sana na siendani kabisa na yule binti ikabidi lasivyo kitachonikuta ni shauri langu akaona ngoja aanze kunipa ABC zake ndio nikajijua kua mimi yule binti simjui hivyo yaan nikajiona mimi ni mweupe kabisa jinsi anavyoniambia yupo sivyo alivyo ni mtu mwingine kabisa

Copy that?
 
Kikawaida niceguys ndio wanaopelekeshwa na kitu kidogo kiitwacho mapenzi

Kitu ambacho unaweza kuamua kumuacha mtu ukaendelea na maisha yako bila kuathirika.
Kama ni kutafuta mwanamke mwingine wamejaa huko mabarabarani, makanisani, masokoni, mitandaoni.
Sasa kipi kinafanya watu waumizww na mapenzi?

Niceguys kwao mapenzi ni hisia.
Alphamale kwao Mapenzi ya uamuzi tuu.

Wanaweza kuamua kuchagua kupenda na hapo hapo wakaamua kufukuza mtu asiyefit matakwa yake
Kwenye mapenzi usitangulize hisia mbele ukaziacha akili nyuma,utateseka sana,
Akili ndio inatakiwa itangulie mbele.
 
Kwenye mapenzi usitangulize hisia mbele ukaziacha akili nyuma,utateseka sana,
Akili ndio inatakiwa itangulie mbele.

Sahihi Kabisa.

Kwa Dunia ya sasa. Dunia ambayo watu wanaoana bila miiko ni majinga tuu ndio huyachukulia mapenzi kama jambo la hisia na lazima.

Mapenzi bila mipaka.
Mapenzi bila Ukabila
Mapenzi bila udini
Mapenzi bila hadhi
Ulisikia wapi? Lazima watu wapasuane
 
Back
Top Bottom