Leo ni leo asemaye kesho muongo. Polepole kuongea na Watanzania saa mbili kamili usiku! Usikose!

Records matter!,mkuu,huwezi kujiibukia tu huko utokako,unaropoka ropoka tu,kwa upumbavu tukakuamini KIJINGA,tunaangalia rekodi zako,je zipoje? je huyu mtu ni safi kweli, ngoja tuone faili zake,ndivyo dunia ilivyo!
Sawa umeangalia record zake ni mchafu kwahiyo mtafanya nini? Mtaanza kumhukumu kwa record zake chafu? Huo muda mnaupata wapi wa kutaka kujiridhisha na mambo yaliyopita yasiweza kurekebishika kwasababu muda umepita tayari? Kama tuko serious tukubaliane hakuna aliemsafi atakae kuja kutusafishia nchi yetu ila ni dhamira ya pamoja sote tuache tofauti zetu tuijenge Tanzania bora kwa wote kuanzia sasa! Kama unaona ni muhimu kunga'ng'ania yaliyopita mpaka uridhike na roho yako ,utapoteza fursa muhimu ya kuibadili Tanzania wakati huu ambao ni golden chance in lifetime!
 
Mimi nilikuwa sijuhi kama JPM alipewa ujumbe kuwa wanajiandaa kumuua, Mimi sikuwa nikifahamu kuwa simu ilipigwa kutoka juu Rostam Aziz akapewa mgodi wote wa makaa ya Mawe.....
 
Hakuna kinachopita mkuu,hata leo hii ndani ya CCM,Wanaofanya upumbavu wataulipia tu,ipo siku yaja!,CHAMA CHETU KITAJIVUA GAMBA PHASES II.
 
Hakuna kinachopita mkuu,hata leo hii ndani ya CCM,Wanaofanya upumbavu wataulipia tu,ipo siku yaja!,CHAMA CHETU KITAJIVUA GAMBA PHASES II.
Haya wewe na wenzako endeleeni kujivua hayo magamba! Kina POLEPOLE washafikiria vinginevyo! Kila mtu ashike linalompendeza,nikutakie kutwa njema huku nikisubiri tukio la POLEPOLE hapo baadae.
 
Polepole=dead body
 
Kwa mtazamo wangu, Polepole anapoteza muda. Anachokifanya sasa kilipaswa kufanyika tangu mwaka 2000 au angalau 2005. Kwa sasa, hao anaowaita wahuni ndio walioko madarakani, na muda umeshapita.

Kuhusu Magufuli, ukweli ni kwamba alitokana na migongano na usaliti baina ya hao hao wahuni. Tayari wameshajifunza kosa walilolifanya na hawatarudia tena.

Kilicho kibaya zaidi, Polepole anapigania maslahi ya CCM lakini kwa namna fulani anaonyesha chuki ya waziwazi kwa Mama Samia – jambo ambalo linamharibia yeye mwenyewe. Anaposema CCM ifuate utaratibu na katiba iliyojiwekea, ukweli ni kwamba hata viongozi wastaafu kama Jakaya na wengine wa zamani wakimsikia watamcheka. CCM haina utaratibu huo – anayekuwepo madarakani ndiye mwenye uamuzi wa mwisho; ndiye katiba na taratibu zenyewe.

Tukumbuke, Polepole mwenyewe alikuwa sehemu ya uharibifu wa uchaguzi wa 2020 ambapo wagombea wa upinzani walikandamizwa kwa visingizio visivyo na msingi. Sasa leo aje kusema Magufuli alipata kura nyingi kwa heshima kubwa – si kweli. Ukweli ni kwamba CCM ilitumia mbinu za nguvu na yeye alikuwa sehemu ya huo mfumo.

Kwa sasa kinachomtokea ni kwamba Polepole bado hajaamini kuwa Magufuli hayupo na hatarudi tena. Inaonekana kama amepata mshtuko au hata sonona, pengine kwa sababu aliahidiwa mambo makubwa ambayo hayajatimizwa.

Badala ya kueneza taharuki zisizo na msingi, afuate taratibu za chama chake huko ndani. Sisi wananchi wengi hatuna muda na lawama zake dhidi ya CCM au mwenyekiti wake. Watanzania tayari tumeshakubaliana na hali tuliyonayo – liwalo na liwe.

Kwa ufupi, Polepole anapoteza muda wake bure.
 
Mbona kama mna hofu fulani hivi tulieni dawa iwaingie fresh.
 
Haya wewe na wenzako endeleeni kujivua hayo magamba! Kina POLEPOLE washafikiria vinginevyo! Kila mtu ashike linalompendeza,nikutakie kutwa njema huku nikisubiri tukio la POLEPOLE hapo baadae.
Guitarist polepole and its tirelessly effortless unknown and ignored speeches!
 
Kilicho kibaya zaidi, Polepole anapigania maslahi ya CCM lakini kwa namna fulani anaonyesha chuki ya waziwazi kwa Mama Samia – rudia kusema hapo, ila pia Polepole ameishajibu hili la chuki kwa Rais akiweka pia mifano thabidi ya kuwa yupo na Rais....
Subiri Leo ndio utajua kuwa na Samia naye ni Mhuni pro max!
 
Kuwa macho sana , ukionekana unaungana/unasupport na HP watakuwa na negative impression on you and you will be in trouble. Take care!
Mkuu Retired ,usemayo ni kweli kabisa,mtu ukiwa mkweli toka ndani ya nafsi yako,kama alivyo Comred Polepole,utaonekana an enemy of the people!,hiki anachokipigia kelele Polepole,mimi nilimtangulia kukizungumzia kwa kumwandikia Dada barua Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa they didnt take it well!,lakini sisi wa jicho la tatu,kuna vitu tunaviona,wengine hawavioni,hivyo tunasaidia kuviepusha,ndiko kumsaidia kwenyewe!mada kama hii Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe? ni msaada mkubwa kwake!
P
 
A Day To Remember
 
Unafanya 'Sarcasm' tu Ili mitandao ifungwe tusisikie vitimbi vya Ccm.
 
Chama tawala kilipaswa kuona hili na kukemea kwani ndicho chenye RAIS!
Tatizo ni nani anayeweza kumkoromea au kumkemea Rais au vyombo vya Dola ndani ya ccm?????

Kumbuka kuwa siku hizi kuna Policcm, Takukuccm, TISSCCM. Yaani kila mahala ni CCM wenyewe. Wahalifu wanalindana wenyewe maana kila mmoja ni mhalifu. Nani anayeweza kunyanyua mdomo wake, hajipendi au hataki ugali????

Usione Polepole kaamua kuacha madaraka na kuanza kupambana nao akiwa mafichoni. Ukiwa ndani huwezi, unless ujitoe ufahamu. La sivyo utaliwa kichwa asubuhi kweupe.

Rais na serikali yake nani anaweza kusema ili hali Rais ndo mwenyekiti wa chama. Vikao vyote vya maamuzi yeye ndo mwenyekiti.

Usione akina Gwajima wamesubiri muda wa bunge uko ukingoni kuiisha ndo wakaanza kukoloma. Walifanya hivyo kwa sababu hawana cha kupoteza baada ya bunge kuvunjwa, maana walijua kuchaguliwa tena ubunge haiwezekani.

Lakini funga kazi ya yote haya ni ubinafsi na unafiki wa kupindukia. UJINGA umetamalaki. Taifa limejaa watu wenye umasikini wa kifikra. Ndiyo maana wamebuni mbinu mpya ya kuishi nayo ni Uchawa na Ukunguni japo waendelee kula mabaki.

Matokeo yake taifa linaongozwa na watu wenye ufinyu wa akili na wasio na vision. Vichwa vyao vimebeba tui la nazi.
 
Awe serious narratives za uongozi sio Muhimu tena. Atoboe jipu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…