Uchaguzi 2020 Leo nimeamini Mbowe mzalendo, Wahariri TBC wachukuliwe hatua kutangaza kinyume na sheria za utangazaji

Mwaka wa ishirini mkisema hivyo.huijui hii moshi wewe.MOSHI NI CHUO CHA SIASA.KAMUULIZE DAVIS MOSHA UCHAGUZI ULIOPITA ALITUMIA ZAIDI YA BILLION 5 .Moshi ni chuo cha siasa mkuu.
Acha uongo, bil 5 unaijua au unaisikia
 
Naangalia TBC hapa na naona wametoa kipande cha Mbowe kuwapa dakika kumi na tano kuondoka lakini ikafuatiwa na TAMKO la TBC ambalo pamoja na maelezo yote wameeleza pia kuwa wao ni chombo cha umma.

Kwa miaka mitano TBC hawajwahi kuripoti kitu positive cha upinzani na naamini tukio la leo limewakamata "pants down".

Ni jukumu la TBC aidha kujisahihisha na kuwa kweli chombo cha umma au kuendelea kutumikia upande mmoja.Pia kuna kanuni za uchaguzi na sheria mbalimbali na ikiwa mtu atatukana au kueleza yasiyostahili sheria itachukua upande wake.

Ngoja tuone ya Dodoma kuwa patakuwa na editing na masimulizi kama ya kusimulia mchezaji wakati mechi inaendelea?

Tunatembea katika kamba nyembamba sana katika siku chache hizi.Busara,Busara na hekima vitumike.
 
Imewauma sana?
 
Mbowe mtoto wa mjini, alijua Live ya TBC itaweka record mbaya kwa wanayokusudia kuongea. Anatangaza ati amesikia TBC wamezima matangazo ili wananchi wasisikie hotuba zao, hali sisi tunamsikia akisema hayo na kuwafukuza kupitia hiyo hiyo TBC, Tbc maripota wanaondoka hali wakizomewa tunaona live. Sasa jiulize TBC aliyoambiwa imezimwa ni ipi?
 
Mkuu umeandika huku umekalia ukuni kitu kigumu chenye ncha butu laini
 
Anzia hapa
Kweli Kuna Upinzani!!
Na Haya nimalipo ya Wasaliti shenzi kabisaView attachment 1550997
Kumbukumbu kidogo,2015 nchi imeingia katika kampeni vyama vikiwa vimepata almost fursa sawa kujitangaza nchi nzima.2020 tunaingia katika kampeni chama kimoja kikiwa kimepata fursa miaka mitano wakati vyama vingine vikiwa kifungoni.Pia pitia sheria ngapi mpya zimeanzishwa katika kupunguza uhuru wa maoni.

Naamini siku zinavyokwenda na uoga unavyoanza kuwaondoka watu inawezekana usiamini utakachokiona.Muda ni mwalimu mzuri!
 
mimi naona Muheshimiwa MBOWE alidanganywa Kabla ya kumkaribisha mgombea Uraisi kuwa TBC haipo hewani; naye akawafukuza waondoke ndani ya dkk15; sisi tulikuwa tuna angalia live kwenye ukumbi wetu wa kuangalilia mpira;

ghafla TBC wakaomba msamaha kuwa wameambiwa waondoke. Ukweli hatukupata fursa ya kuona kilichoendelea. Tuache unafiki; wanachadema wengi wamekosa uhondo wa kumsikiliza mgombea Uraisi wao.
 
TBCccm ni kitengo kingine cha maccm kueneza ujinga Nchini. Ni wahuni tu hao.

Naangalia TBC hapa na naona wametoa kipande cha Mbowe kuwapa dakika kumi na tano kuondoka lakini ikafuatiwa na TAMKO la TBC ambalo pamoja na maelezo yote wameeleza pia kuwa wao ni chombo cha umma...
 
Naangalia TBC hapa na naona wametoa kipande cha Mbowe kuwapa dakika kumi na tano kuondoka lakini ikafuatiwa na TAMKO la TBC ambalo pamoja na maelezo yote wameeleza pia kuwa wao ni chombo cha umma...
Kesho Dodoma tv zote zitakuwa live kuanzia TV mpaka YouTube. Azam TV mpaka Millard ayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…