Leo nimegundua kitu kimoja, kuvuka barabara si kitu kidogo!

H r n

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2019
Posts
1,100
Reaction score
2,079
Leo nimeacha chombo changu sehemu fulani, nikatembea kwa miguu kwa muda mrefu. Kwa kweli nilichokutana nacho njiani kimenifanya nitafakari sana kuhusu usalama wa watembea kwa miguu.

Nilipofika sehemu ya kuvuka barabara, nilihisi wasiwasi mkubwa. Pikipiki zinakuja kwa kasi, magari nayo yanapita kwa kasi, na wakati mwingine unalazimika kuvuka haraka huku ukitazama kulia na kushoto kwa hofu.

Cha kushangaza ni kwamba kwa muda mrefu nimekuwa nikisafiri kwa chombo, hivyo sikuwahi kuzingatia sana changamoto ambazo mtu anayesafiri kwa miguu anakutana nazo kila siku.

🦷Swali langu kwa wanaJF ni hili:🦷
👉 Kwa wale mnaotembea kwa miguu mara kwa mara, ni hatari gani kubwa mnazokutana nazo barabarani?
👉 Kuna maeneo ambayo mnaona ni hatari sana kuvuka?
👉 Tatizo kubwa ni kasi ya magari/pikipiki, kutokuwepo kwa pedestrian crossing, barabara mbovu, au madereva kutowajali watembea kwa miguu?
👉 Na wewe umewahi kukutana na tukio ambalo lilikufanya uogope kuvuka barabara?
 
Ndio ujue umuhimu wa kusimama kwenye zebra kuruhusu watu wapite. Sijawahi kuendesha gari hata siku moja bila kupisha watu kuvuka kwenye zebra au hata sehemu ambayo haina zebra nikiona watoto au watu wazima/wazee.
 
Afadhali wenye magar wanaweza kukupisha uvuke....shida ipo kwa boda boda hata kwenye zebraaaa inabid kuangalia kushoto na kulia bila hivyo boda anakuzoa, tunateseka sana
Hawa bodaboda huwa wananikera sana. Unapisha watu wavuke yeye anapita mbio! Anafanya dereva kumpisha mtu avuke iwe kuhatarisha maisha ya mvukaji.
 
Leo nimeacha chombo changu sehemu fulani, nikatembea kwa miguu kwa muda mrefu. Kwa kweli nilichokutana nacho njiani kimenifanya nitafakari sana kuhusu usalama wa watembea kwa miguu
Ila mleta mada una nyota nzuri. Umeleta uzi wa hivi bila kushambuliwa hapa JF?! Hold on....wachangiaji wa kwanza hawajakushambulia, wangekushambulia hao wa kwanza wanaofuata wangeunga tela kama wanavyopiga mwizi bila kujua kaiba nini.
 
Ndio ujue umuhimu wa kusimama kwenye zebra kuruhusu watu wapite. Sijawahi kuendesha gari hata siku moja bila kupisha watu kuvuka kwenye zebra au hata sehemu ambayo haina zebra nikiona watoto au watu wazima/wazee.

Mkuu madereva kama nyie mpo wachache sana siku hizi. Juzi tuu hapo Sayansi Kijitonyama, nimeshuhudia mtu yupo katikati gari zinampita huku huku. Mtu mmoja ndo akasimama jamaa akavuka. Asingekuwa na ujanja wa kukaa kwenye chaki, alikuwa anagongwa, ni ile unasubiri taa, chwaa gari zinaondoka upo kati. 😊
Kila mtu ana haraka mjini, kila mtu anawahi. 😊
 
It's sad. Barabara zimekuwa kama uwanja wa vita. And it's getting worse.
 
Siku moja nilikuwa tegeta njia inayoelekea sokoni nyuki sasa pale ikiwa unatokea mwenge ndio barabara mbili zinaishia kwa hiyo kuna kama tuta fulani hivi lipo la kutenganisha barabara kutoka njia mbili kwenda njia moja kwangu mimi nikaona ndio sehemu salama kuvuka sababu ni rahisi kuvuka upande mmoja na kuyaona magari kiurahisi kisha ukahamia upande mwingine uwezi amini halafu ilikuwa muda ya saa tatu usiku nikiwa nishavuka upande mmoja naelekea upande wa pili nikawa juu ya lile tuta ili nivuke upande wa pili Mmmm!! Acha tu sijui yule dereva alilewa au vipi na sijui hakujua kuwa pale njia inabadilika toka njia mbili kwenda moja ghafla akaliparamia lile tuta nashukuru nilisalimika ila sitosahau Ila kuvuka barabara hasa kwa dar ni hatari
 
Afadhali wenye magar wanaweza kukupisha uvuke....shida ipo kwa boda boda hata kwenye zebraaaa inabid kuangalia kushoto na kulia bila hivyo boda anakuzoa, tunateseka sana
Wanaomiliki magari hawana shida wenye shida ni madereva wa magari ambao gari siyo zao.yaani hawako tofauti tu na bodaboda
 
Bodaboda ni tatizo kubwa sana kwa watembea kwa miguu, hawafati sheria kabisa. unavuka umakini umeweka kwenye magari na taa za barabara mara vuuu boda uyooo anapita motooo. Ukizubaa kidogo tu wanakuvunja ugoko.
 
Mkuu madereva kama nyie mpo wachache sana siku hizi. Juzi tuu hapo Sayansi Kijitonyama, nimeshuhudia mtu yupo katikati gari zinampita huku huku. Mtu mmoja ndo akasimama jamaa akavuka. Asingekuwa na ujanja wa kukaa kwenye chaki, alikuwa anagongwa, ni ile unasubiri taa, chwaa gari zinaondoka upo kati. 😊
Kila mtu ana haraka mjini, kila mtu anawahi. 😊
Lazima kuzingatia usalama wa wengine hata kam una haraka ila
 
Back
Top Bottom