Ndio ujue umuhimu wa kusimama kwenye zebra kuruhusu watu wapite. Sijawahi kuendesha gari hata siku moja bila kupisha watu kuvuka kwenye zebra au hata sehemu ambayo haina zebra nikiona watoto au watu wazima/wazee.Leo nimeacha chombo changu sehemu fulani, nikatembea kwa miguu kwa muda mrefu. Kwa kweli nilichokutana nacho njiani kimenifanya nitafakari sana kuhusu usalama wa watembea kwa miguu.
Nilipofika sehemu ya kuvuka barabara, nilihisi wasiwasi mkubwa. Pikipiki zinakuja kwa kasi, magari nayo yanapita kwa kasi, na wakati mwingine unalazimika kuvuka haraka huku ukitazama kulia na kushoto kwa hofu.
Cha kushangaza ni kwamba kwa muda mrefu nimekuwa nikisafiri kwa chombo, hivyo sikuwahi kuzingatia sana changamoto ambazo mtu anayesafiri kwa miguu anakutana nazo kila siku.
🦷Swali langu kwa wanaJF ni hili:🦷
👉 Kwa wale mnaotembea kwa miguu mara kwa mara, ni hatari gani kubwa mnazokutana nazo barabarani?
👉 Kuna maeneo ambayo mnaona ni hatari sana kuvuka?
👉 Tatizo kubwa ni kasi ya magari/pikipiki, kutokuwepo kwa pedestrian crossing, barabara mbovu, au madereva kutowajali watembea kwa miguu?
👉 Na wewe umewahi kukutana na tukio ambalo lilikufanya uogope kuvuka barabara?
Hawa bodaboda huwa wananikera sana. Unapisha watu wavuke yeye anapita mbio! Anafanya dereva kumpisha mtu avuke iwe kuhatarisha maisha ya mvukaji.Afadhali wenye magar wanaweza kukupisha uvuke....shida ipo kwa boda boda hata kwenye zebraaaa inabid kuangalia kushoto na kulia bila hivyo boda anakuzoa, tunateseka sana
Nyinyi watoto wa kishua na mabasi ya njano tangu wadofo hamuwezi kuvuka barabara.Binafsi nimeshindwa… Mara kibao nimeshavushwa na mtu anayegundua kuwa yamenishida.
WaTz ni watu wazuri.
No RR, ni athari za kukulia kijijini unfortunately😂Nyinyi watoto wa kishua na mabasi ya njano tangu wadofo hamuwezi kuvuka barabara.
Nakuelewa posh areas zimetulia kama kijijini 😀😀No RR, athari za kukulia kijijini unfortunately😂
Ila mleta mada una nyota nzuri. Umeleta uzi wa hivi bila kushambuliwa hapa JF?! Hold on....wachangiaji wa kwanza hawajakushambulia, wangekushambulia hao wa kwanza wanaofuata wangeunga tela kama wanavyopiga mwizi bila kujua kaiba nini.Leo nimeacha chombo changu sehemu fulani, nikatembea kwa miguu kwa muda mrefu. Kwa kweli nilichokutana nacho njiani kimenifanya nitafakari sana kuhusu usalama wa watembea kwa miguu
Ndio ujue umuhimu wa kusimama kwenye zebra kuruhusu watu wapite. Sijawahi kuendesha gari hata siku moja bila kupisha watu kuvuka kwenye zebra au hata sehemu ambayo haina zebra nikiona watoto au watu wazima/wazee.
It's sad. Barabara zimekuwa kama uwanja wa vita. And it's getting worse.Mkuu madereva kama nyie mpo wachache sana siku hizi. Juzi tuu hapo Sayansi Kijitonyama, nimeshuhudia mtu yupo katikati gari zinampita huku huku. Mtu mmoja ndo akasimama jamaa akavuka. Asingekuwa na ujanja wa kukaa kwenye chaki, alikuwa anagongwa, ni ile unasubiri taa, chwaa gari zinaondoka upo kati. 😊
Kila mtu ana haraka mjini, kila mtu anawahi. 😊
Wanaomiliki magari hawana shida wenye shida ni madereva wa magari ambao gari siyo zao.yaani hawako tofauti tu na bodabodaAfadhali wenye magar wanaweza kukupisha uvuke....shida ipo kwa boda boda hata kwenye zebraaaa inabid kuangalia kushoto na kulia bila hivyo boda anakuzoa, tunateseka sana
Lazima kuzingatia usalama wa wengine hata kam una haraka ilaMkuu madereva kama nyie mpo wachache sana siku hizi. Juzi tuu hapo Sayansi Kijitonyama, nimeshuhudia mtu yupo katikati gari zinampita huku huku. Mtu mmoja ndo akasimama jamaa akavuka. Asingekuwa na ujanja wa kukaa kwenye chaki, alikuwa anagongwa, ni ile unasubiri taa, chwaa gari zinaondoka upo kati. 😊
Kila mtu ana haraka mjini, kila mtu anawahi. 😊
Zebra sijawahi kuziamini mm nikiwa navuka hahhaa ni mwendo wa ngiri sirembiBodaboda ni tatizo kubwa sana kwa watembea kwa miguu, hawafati sheria kabisa. unavuka umakini umeweka kwenye magari na taa za barabara mara vuuu boda uyooo anapita motooo. Ukizubaa kidogo tu wanakuvunja ugoko.