Washtue majaji, ni kosa shahidi kudanganya akiwa chini ya kiapo. Ama sivyo acha ujuaji.Mpaka hapa Heche ni muongo
Lipi?Heche ana tatizo leo ndio nimeamini rasmi, naamini Lissu nae amesikia na kujionea mwenyewe.
Kwa sababu ya UCHAGUZI.Katuga acha utoto pumbavu zako mbona serikali yako unayoitetea haikuwakamata wauaji wakati kosa la MAUAJI ni jinai 100% na wakili wake ni muuaji Katuga.WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 15.
Nassoro Katuga: Nilikusikia kwamba ulitiwa hatiani ukalipishwa milioni 40.
Heche: Ni sahihi.
Nassoro Katuga: Ni kweli kwamba hizo pesa mlichangisha watu?
Heche: Mimi nilikuwa gerezani.
Nassoro Katuga: Kwani wewe ulitoa pesa zako?
Heche: Kililipa chama.
Nassoro Katuga: Ikitokea mtu akasema ni wananchi ndiyo walichangia na siyo chama, atakuwa mwongo?
Heche: Nitashukuru.
Nassoro Katuga: Nilisikia ukisema ulifungwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Heche: Ni sahihi.
Nassoro Katuga: Kwani kwa uelewa wako hakuna Mahakama inaitwa Kisutu?
Heche: (Anacheka.)
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ni wewe ulieleza Bhoke aliuawa na baadaye wahusika wakaachiaa na kesi ikaisha hivyo hivyo.
Heche: Sahihi.
Nassoro Katuga: Ulifafanua hiyo “hivyo hivyo”?
Heche: Hapana.
Nassoro Katuga: Unajua rate ya mauaji ya Tarime ipo juu?
Heche: Sijui.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ni wewe uliyeeleza Bwana Alphonce Mawazo aliuawa?
Heche: Ni kweli.
Nassoro Katuga: Eleza Mahakama kama ulisema ni sababu ya uchaguzi.
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa kama unamjua muuaji.
Heche: Simjui.
Nassoro Katuga: Ulieleza hiyo sababu ya huyo muuaji kumuua Mawazo?
Heche: Ni kwa sababu ya uchaguzi.
Nassoro Katuga: Kama ulikuwa humjui muuaji, ulijuaje ni sababu ya uchaguzi?
Heche: Ni kwa sababu ni wakati wa uchaguzi.
Nassoro Katuga: Mtu mwenye wivu wa kimapenzi unazuia mtu kumuua Mawazo?
Heche: Sheria inazuia.
Nassoro Katuga: Unapata wapi sababu ya kueleza Mahakama hii kwamba Mawazo ameuawa kwa sababu za uchaguzi?
Heche: Tulijadili katika Kamati Kuu.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Hawa ni watu ambao wana ajenda zao dhidi ya Heche, Walikuwa wanasubiri hii session kwa hamu wapitishe ajenda zao.Kuna kitu hakiko sawa hasa kwemye mtazamo wetu juu ya viongozi wa upinzani.
Yes, ni kweli sio wote ni waaminifu, na kweli wengine wanatumika na dola, lakini haimaanishi ukiwa mpinzani, usifanye biashara au usiwe na deals na watu tofauti tofauti. Cha muhimu, je hizo deals ni CLEAN?.
Heche amekuwa diwani na mbunge kwa miaka mingi, hivi kwa level yake Milioni 20 kweli ni hela ya kuanza kuishangaa?
Upinzani sio umasikini.
Majungu tu yamewatawala.Hata zile komedi za tone tone,wakatoliki feki,chadema feki mwasisi wake ni Katuga akishirikiana na Mbowe.Hawa ni watu ambao wana ajenda zao dhidi ya Heche, Walikuwa wanasubiri hii session kwa hamu wapitishe ajenda zao.
Katuga tuletee ushahidi nani alikuwa anaua watu Kibiti.WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 16.
Nassoro Katuga: Sababu za muuaji kumuua Mawazo umezitoa wapi?
Heche: Nimesikia katika vyombo vya habari. Nilikuwa Bungeni na tukajadiliana katika Kamati Kuu ya CHADEMA, na mimi nilikuwapo.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa, sasa ni ushahidi uliowasilisha hapa ni kutoka kwa viongozi wa Geita?
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Na hujawataja hapa Mahakamani waliokwambia hiyo taarifa?
Heche: Sijawataja Sikuambiwa nitaje.
Nassoro Katuga: Unafahamu kwamba Kibiti kuna watu walikuwa wanauawa?
Heche: Nafahamu.
Nassoro Katuga: Na waliokuwa wanauawa huko Kibiti walikuwa viongozi wa CCM na viongozi wa vijiji?
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Je, mtu yeyote atakuwa sahihi akisema hao watu wa CCM walikuwa wanauawa kwa sababu za uchaguzi?
Heche: Anaweza kuwa sahihi akisema hivyo.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, Shahidi ananikumbusha ni saa 7.
Kwa ridhaa ya Mahakama hii, naomba tupate ile health break.
Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, naomba tuhairishe kwa lisaa limoja.
Lissu: Why saa 1?
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, unasema?
Lissu: Waheshimiwa Majaji, ni utamaduni tuna-break kwa saa 1 na nusu.
Na ni kwa sababu mimi napata nusu saa ya kuongea na mashahidi kwa sababu natokea gerezani.
Kwa hiyo ni saa 1 na nusu, kama ambavyo imekuwa.
Jaji Ndunguru: Tutaenda mapumziko ya saa moja na nusu.
Saa 8 na nusu shauri litaendelea.
MAJAJI WANATOKA.
TUKUTANE SAA 8:30 MCHANA
WEKA EMOJI KAMA TUPO SAMBAMBA.
Katuga alimshindwa Lissu mwanzo hadi mwisho vilevile Mnyika wengine wote kawaweza ngoja tuone ataishia wapi na Wegesa
Sijui wew ni wakike au kiume ila kama ni wa kike Mungu akusamehe ila kama ni mwanaume jiandae kuna msiba mkubwa upo juu yako......Allah hajawahi niangusha na maono yangu....
Asante ManyanzaWAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 16.
Nassoro Katuga: Sababu za muuaji kumuua Mawazo umezitoa wapi?
Heche: Nimesikia katika vyombo vya habari. Nilikuwa Bungeni na tukajadiliana katika Kamati Kuu ya CHADEMA, na mimi nilikuwapo.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa, sasa ni ushahidi uliowasilisha hapa ni kutoka kwa viongozi wa Geita?
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Na hujawataja hapa Mahakamani waliokwambia hiyo taarifa?
Heche: Sijawataja Sikuambiwa nitaje.
Nassoro Katuga: Unafahamu kwamba Kibiti kuna watu walikuwa wanauawa?
Heche: Nafahamu.
Nassoro Katuga: Na waliokuwa wanauawa huko Kibiti walikuwa viongozi wa CCM na viongozi wa vijiji?
Heche: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Je, mtu yeyote atakuwa sahihi akisema hao watu wa CCM walikuwa wanauawa kwa sababu za uchaguzi?
Heche: Anaweza kuwa sahihi akisema hivyo.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, Shahidi ananikumbusha ni saa 7.
Kwa ridhaa ya Mahakama hii, naomba tupate ile health break.
Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, naomba tuhairishe kwa lisaa limoja.
Lissu: Why saa 1?
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, unasema?
Lissu: Waheshimiwa Majaji, ni utamaduni tuna-break kwa saa 1 na nusu.
Na ni kwa sababu mimi napata nusu saa ya kuongea na mashahidi kwa sababu natokea gerezani.
Kwa hiyo ni saa 1 na nusu, kama ambavyo imekuwa.
Jaji Ndunguru: Tutaenda mapumziko ya saa moja na nusu.
Saa 8 na nusu shauri litaendelea.
MAJAJI WANATOKA.
TUKUTANE SAA 8:30 MCHANA
WEKA EMOJI KAMA TUPO SAMBAMBA.
Sijui wew ni wakike au kiume ila kama ni wa kike Mungu akusamehe ila kama ni mwanaume jiandae kuna msiba mkubwa upo juu yako......Allah hajawahi niangusha na maono yangu....
Mko kwenye ushabiki, wenzenu wanafanya kweli!huo ujinga wenu umeshindwa kuthibitisha uhaini mnarukaruka tinawataka wale wanaojiita makamanda siku hiyo ndio watamjua lissu ni nani.
Kutoka kesi ya msingi mtu anauliza maisha binafsiWAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 6.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, nina maswali machache. Naomba kuendelea kwa kadiri atakavyokuwa anajibu, Waheshimiwa Majaji.
Nassoro Katuga: Bwana Heche, kama nimekusikia una miaka 45?
Heche: Ni sahihi.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo nikikuita Bwana Mdogo usijisikie vibaya, kwa sababu nina miaka 52.
Nassoro Katuga: Unajua au hujui kwamba tunataka ushahidi wako uonekane wa uongo?
Heche: Hata kama ni kweli.
Nassoro Katuga: Ni kweli kwamba baba yako anaitwa Suguta?
Heche: Ni kweli.
Nassoro Katuga: Shahidi, una elimu gani?
Heche: Elimu ya Chuo Kikuu.
Nassoro Katuga: Umesomea nini?
Heche: Bachelor of Arts with Education.
Nassoro Katuga: Ulienda chuo direct?
Heche: Nilitoka Form Six nikaenda kusoma Chuo cha Ualimu.
Nassoro Katuga: Huko Chuo cha Ualimu ulisomea nini?
Heche: Diploma ya Ualimu.
Nassoro Katuga: Ni kweli kwamba Form One hadi Form Six ulikuwa unaitwa Charles Wegesa Heche?
Heche: Ni kweli.
Nassoro Katuga: Ni kweli kwamba Form Four ulipata Division Four ya 27?
Heche: Si kweli. Nilipata Division One.
Heche: Huwezi kupata Division Four ukachaguliwa Musoma Alliance.
Nassoro Katuga: Katika familia yenu nani anaitwa David Suguta Heche?
Heche: Ni mdogo wangu.
Nassoro Katuga: Kuna David Suguta wangapi?
Heche: Wapo watatu, na baba yangu alikuwa na wake 8.
Nassoro Katuga: Nani alienda kutibiwa nje ya nchi?
Heche: David Suguta Heche.
Nassoro Katuga: Alienda kutibiwa na nani?
Heche: Tulimchangia.
Nassoro Katuga: Alienda kutibiwa na nani?
Heche: Unataka nikutajie? Hata mimi nilichanga.
Nassoro Katuga: Umeiambia Mahakama una chanzo gani cha kukuingizia mapato kama mshahara au posho?
Heche: Sikuiambia.
Nassoro Katuga: Kwa cheo chako cha Makamu Mwenyekiti, unalipwa posho au mshahara?
Heche: Silipwi chochote.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ni kweli au si kweli una malori ya ku-operate nchini Kenya?
Heche: Si kweli. (Ha ha ha... mimi ni mkulima wa parachichi.)
Nassoro Katuga: Kwa kuwa hulipwi katika Chama, waambie Waheshimiwa Majaji kuwa una magari 4 ya bei mbaya.
Heche: Hapana. Sina magari mawili, na sijui “bei mbaya” ni ipi.
Nassoro Katuga: Unajua kwamba taarifa za umiliki wa magari zinahifadhiwa TRA?
Heche: Najua.
Nassoro Katuga: Kwa ridhaa ya Mahakama, naomba nikuonyeshe nyaraka hizi.
Heche: Sawa.
Nassoro Katuga: Hizo ni nini?
Heche: Kadi za magari.
Nassoro Katuga: Zipo ngapi?
Heche: Zipo 5, lakini kuna mashine pia kama tractors.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji zinaonyesha umiliki wa kitu gani?
Heche: Hii moja ni tractor, Mitsubishi Canter ya kwangu, Toyota Crown, Hilux Double Cabin na Prado ninayotumia kila siku.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, Mitsubishi ni gari au si gari?
Heche: Ni gari.
Nassoro Katuga: Crown ni gari au si gari?
Heche: Ni gari.
Nassoro Katuga: Prado ni gari au si gari?
Heche: Ni gari.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji ulisema una gari ngapi?
Heche: Niliwaambia gari 2.
MASUALA YA FEDHA NA “TONETONE”
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, hivi utaratibu wa CHADEMA, zile “tonetone”, au kiongozi anapopata mchango kutoka kwa marafiki, anafanya nini?
Heche: Tonetone imeanza juzi.
Nassoro Katuga: Makamu Mwenyekiti anapopata, ukipokea mchango kwa ajili ya Chama, huwa unafanya nini?
Heche: Masuala ya fedha yapo kwa Katibu Mkuu.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo wewe huwezi kupokea fedha?
Heche: Siwezi.
Nassoro Katuga: Zile pesa ulizopokea kwa Nilesh ulipeleka wapi?
Heche: Unaleta majungu ya mtaani hapa?
Nassoro Katuga: Wewe jibu swali, Shahidi.
Heche: Huyo mtu simjui.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Kesi inazalisha mambo kibao nje ya uhaini. Na mambo hayo ndo wanayoyataka CCM kuliko ht hilo la uhaini kama hamjuiSawa.... Huoni hii kesi ni kama kata funua..
Yaani kesi ni Uhaini lakini kinachoendelea ni Tone tone...
Mimi ni mkulima...
Aliyeuwawa mwaka flani ulikuwepo ?
Hapa tusubiri.. Heche iyambie Mahakama una nyumba ngapi ?
Kesi itaendelea... Tuambie vikao vya CHADEMA vina wajumbe wangapi ..
Haya tusubiriAjitoe kisa nini mkuu huyo katuga mbona maswali yake ya kawaida sana