Leonida Swai, mama aliyekusanya walemavu 38 kwenye ‘guest house’ yake Tandale

Leonida Swai, mama aliyekusanya walemavu 38 kwenye ‘guest house’ yake Tandale

Kila siku wanatoka kuomba mtaani na kumletea mapato jioni.

Malipo yao hupewa tu chakula na malazi. Walemavu hao amewakusanya kutoka mikoa mbali mbali Tanzania..
Nilisikia mkuu wa wiraya kinondoni akimpa masaa 24 akaripoti kwake sasa sijui alishatekeleza hilo agizo?
 
Aisee...sinto sahau siku moja natoka hospital general ..nikakutana na omba omba...mtu mzima hivi...

Akaniambia Dada naomba miambili Nile ukoko...Nina njaa..

Nlikua na elfu mbili tu ambayo Ni yangu.. nyingine nlikua nimagizwa matunda.

Daah nikamuona huruma..nikamwambia ngoja nitafute chenji..nikapata chenjii..nikamrudia alipokua amekaa..

Nlimkuta anahesabu hela kibao..buku buku..jelo, miambili ..yaani hela alizonazo Mimi Sina..

Aisee nilisikitika Sana...NIKASEMA dooh
Kweli.
Kwahiyo ulimpatia au ukaahirisha?
 
Itakuwa majungu ya wenye Majumba ya kupangisha...kafanya discount ya kodi ya pango,ili walemavu nao wajimudu..amezushiwa ..Wabongo Bwana.
Utakuwa hujaiona hii habari na wale vilema walivyokuwa wakihojiwa.
 
Huyu maza kaona wabongo wakarimu wakiombwa wanatoa akaamua abuni mradi
 
Yupo na jamaa pale maeneo ya DIT
Yule jamaa ni mzima kabisa anamigue yote but huwa anajikunja anaweka madawa madawa kwenye mikono kama mgonkwa anaanza kuomba hela
Ikifika usiku kabisa giza giza anaanza kutumbee vizuri tu

Siku niliyokutana naye nilishangaa sana aseh kumbe jamaa huwa mzima kabisa.
 
Walemavu 30
Kila moja 10000 kwa siku .
= 300000/=
Tena siku ya jumapili wanatagi makanisa kuna madon wazungu na wahindi kama St joseph pale maeneo ya posta kutoa elfu kumi ni virahisi sana
Watu wanatajirika faster faster sana bongo


300000x7( siku saba kwa wiki))= 2100000
Kwa wiki wanapata=2,100,000 hiyo cash.
Vitu haramu vyote vinalipa sana

Je.mtu kama anaomba anaomba 100 itakueaje kwa wiki sasa hapo?
 
Post nyingi za kijinga humu.
Kwanza kisheria hakuna kosa kuwapangisha hapo kuna siasa uchwara
Serikali imefanya nini kuwasaidia walemavu hata huko wanakotoka?
Wapo wengi wanaokaa makanisani na misikitini asubuhi wanaingizwa mitaani waziri nenda na huko kawatandike viboko masheikh, wachungaji na mapadre.
Hakuna mlemavu anaelazimishwa ila ni kwa hiari yao tena wanafurahia kupata ahueni ya maisha.
Huyo mama apongezwe wakati serikali ikitafuta suluhisho ka kudumu kwa walemavu.
Lawama hapa Kwa serikali na Shukrani Kwa mama anaewasaidia walau kupata rizki.
Wajinga endeleeni kukurupuka.
wewe kwa mwandiko huu huna sheria yoyote unayoijua zaidi ya sheria za vijiweni.
 
Huyu mama mchaga nimemuelewa sana kwa huo mfumo wake wa win-win situation sio kama haya maccm yanayosubiri kupata ajira kwa kuteaka na kuiba kura
 
Ukizubaa tunakukamata tunaenda kukufuga Tandale
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]....Fanyeni TU mabaya ya kila Aina ....Kama Ni PESA mtazipata Sana

Mtatanua Sana..mtaendesha Magari mazuri Sana..mtamwaga makreti ya bia.

Na mtatoa Sadaka lukuki kanisani...Nia ikiwa Ni kujionesha TU kwa watu..
Na mkienda December mnasujudiwa...

Hayo maisha ndio mloyachagua....
 
Huyu mama mchaga nimemuelewa sana kwa huo mfumo wake wa win-win situation sio kama haya maccm yanayosubiri kupata ajira kwa kuteaka na kuiba kura
kwani huko vijijini walipowatoa walikuwa hawali chakula na kulala. Huwez ukawa na akili timamu ukaita hii ni win win situation.
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]....Fanyeni TU mabaya ya kila Aina ....Kama Ni PESA mtazipata Sana

Mtatanua Sana..mtaendesha Magari mazuri Sana..mtamwaga makreti ya bia.

Na mtatoa Sadaka lukuki kanisani...Nia ikiwa Ni kujionesha TU kwa watu..
Na mkienda December mnasujudiwa...

Hayo maisha ndio mloyachagua....
Huyo mama ni tabia yake tu mbovu ila hawezi kureflect tabia za kabila zima. Tabia ya mtu hutokana na makuzi na vinasaba alivyorith kwa wazazi wake.
 
Nimeshangaa sana Na kubaki mdomo wazi;
1. Watanzania tunaroho za kikatili hadi tunafikia kuwatumikisha walemavu?!!

2. Serikali ZA mitaa, wilaya, mkoa Na hata mbunge wa eneo husika walikuwa wapi hadi biashara hii haramu ikaota mizizi na kustawi?!!!!

Tafadhali ndugu zangu viongozi na wananchi wapenda amani tusifumbie macho uovu wa aina hii na mwingine.
Naomba hao walio husika wachukuliwe hatua kali ZA kisheria ili iwe funzo Kwa wengine
 
Kakojoe ulale we liccm
hapa uchama umetokea wapi? Tumia akili tu ya kawaida ndugu yako ambaye huko kwenu mlikua mkimuhudumia vizuri, ghafla anatokea mtu akampatie matibabu sehemu fulani au hisani tu yoyote. Mwisho wa siku unakuta anafanyiwa vitendo vya namna hii ungejisikiaje?

Muda mwingine tujifunze kuvaa uhusika wa watu wengine kabla ya kutoa maoni yetu. Hao walemavu wenyewe wanakili mpaka wanalia kwa ukatili waliokuwa wakifanyiwa kutumikishwa Kama ombaomba.
 
Kama mtu mzima anaweza kuwatumikisha binaadamu wenzake bila huruma tena walemavu wa viungo...,,,huyo mtu anaweza kutenda dhambi yoyote bila uoga wala kujali. Wanaweza kujihusisha Na jambo lolote lile ilimradi wapate fedha!!! Hawa watu ni hatari sana ktk jamii
 
Hii biashara inafanyika karibu sehemu kubwa sana bara Asia hasa India. Mara nyingi wanacheza na Trafiki waongoza magari wanaharibu mfumo wa taa za barabarani. Ni biashara inayolipa sana. Kila mwenye uwezo wa kufanyakazi afanye.
 
Back
Top Bottom