Leonida Swai, mama aliyekusanya walemavu 38 kwenye ‘guest house’ yake Tandale

Leonida Swai, mama aliyekusanya walemavu 38 kwenye ‘guest house’ yake Tandale

Kila siku wanatoka kuomba mtaani na kumletea mapato jioni.

Malipo yao hupewa tu chakula na malazi. Walemavu hao amewakusanya kutoka mikoa mbali mbali Tanzania.

My take:

Watani zangu wachaga tuangalie njia zetu za utafutaji tusifikirie tu kwenda kuweka heshima Disemba nyumbani.

Chanzo: TBC ardhio 4/1/2021.
Hahahaaaa....... Kwa biashara kama hii lazima disemba akatambike Marangu!
 
Post nyingi za kijinga humu.
Kwanza kisheria hakuna kosa kuwapangisha hapo kuna siasa uchwara
Serikali imefanya nini kuwasaidia walemavu hata huko wanakotoka?
Wapo wengi wanaokaa makanisani na misikitini asubuhi wanaingizwa mitaani waziri nenda na huko kawatandike viboko masheikh, wachungaji na mapadre.
Hakuna mlemavu anaelazimishwa ila ni kwa hiari yao tena wanafurahia kupata ahueni ya maisha.
Huyo mama apongezwe wakati serikali ikitafuta suluhisho ka kudumu kwa walemavu.
Lawama hapa Kwa serikali na Shukrani Kwa mama anaewasaidia walau kupata rizki.
Wajinga endeleeni kukurupuka.
Wewe ni mmoja wa wale wasukuma kile kiti cha mlemavu ... FYI yupo mmoja alihojiwa alisema aliambiwa tu nenda Dar kuna kazi na hawakutaka kumwambia kazi gani
 
Angalieni asiwafanye watu wa Mungu vitega uchumi. Wenye roho nzuri hivyo miaka hii hawapo. Lazima kipo kitu anategemea kupata kwao.
 
Kwa hiyo mlitaka walale bure kwenye hiyo Lodge? Kwanza kawapa offer ya maana sana wako karibu na ofisi zao za kazi halafu wanapata huduma ya maji, umeme, chakula n.k Tena hiyo elfu 10 ni ndogo!!
Sasa mbona haikufanya lodge...inamaana hao walemavu wanalipa kuliko wanaokaoa kwa lodge..

Kulala bure una maana gani wakati hao ndo wanaongiza pesa?
 
Kila siku wanatoka kuomba mtaani na kumletea mapato jioni.

Malipo yao hupewa tu chakula na malazi. Walemavu hao amewakusanya kutoka mikoa mbali mbali Tanzania.

My take:

Watani zangu wachaga tuangalie njia zetu za utafutaji tusifikirie tu kwenda kuweka heshima Disemba nyumbani.

Chanzo: TBC ardhio 4/1/2021.
Huo ni wivu na njaa sasa.
Kama ameweka guest na nyie hamuendi kuvunja amri sasa ataishije
 
Kila siku wanatoka kuomba mtaani na kumletea mapato jioni.

Malipo yao hupewa tu chakula na malazi. Walemavu hao amewakusanya kutoka mikoa mbali mbali Tanzania.

My take:

Watani zangu wachaga tuangalie njia zetu za utafutaji tusifikirie tu kwenda kuweka heshima Disemba nyumbani.

Chanzo: TBC ardhio 4/1/2021.

Leonida Swai kuona fursa😂😂😂😂
 
Kuna kilichosahaulika kwenye tafakuri. Je, ni nini kimepelekea hao walemavu kwa wingi kiasi hicho kukubali kutumika hivyo?
Hivi mlemavu atasema Nini?... Ndugu wa hao walemavu wanawauza

Mtu mlemavu utasema Nini?.... inasikitisha nana
 
"Sisi ni next level, serikali imejaribu kutupoteza imeshindwa. Siku hizi Tunamiliki viwanda pia tunafanya Consultancy kubwa kubwa".
Hongereni..tafuteni Sana Pesa...kwa udi na uvumba...haijalishi inapatikanaje...
 
Nilikuwa msaidiaji mzuri nikiona walemavu wamepangwa juani hasa nikiangalia zile hali zao ila baada ya kujaga kuyagundua haya ndo ikawaga mwisho wangu wa kuwasaidia.

Mana nilichokuwa nakitowa hakiendi kumsaidia niliyemlenga zaidi ya kwenda mtu ambaye ni mzima na asiye na haja ya kusaidiwa.
 
Post nyingi za kijinga humu.
Kwanza kisheria hakuna kosa kuwapangisha hapo kuna siasa uchwara
Serikali imefanya nini kuwasaidia walemavu hata huko wanakotoka?
Wapo wengi wanaokaa makanisani na misikitini asubuhi wanaingizwa mitaani waziri nenda na huko kawatandike viboko masheikh, wachungaji na mapadre.
Hakuna mlemavu anaelazimishwa ila ni kwa hiari yao tena wanafurahia kupata ahueni ya maisha.
Huyo mama apongezwe wakati serikali ikitafuta suluhisho ka kudumu kwa walemavu.
Lawama hapa Kwa serikali na Shukrani Kwa mama anaewasaidia walau kupata rizki.
Wajinga endeleeni kukurupuka.
Ndungu mchaga...naona unamtetea mchaga mwenzako...
.Kumbuka Dunia ya leo ulemavu waweza mpata yoyote..Kuna kisukari Watu wanakatwa miguu....

Kuna ajali... Unapenda Ndugu Zako wakuuze ...wakuanike juani pale mnazi mmoja asubuhi Hadi jioni...ukiomba Mia Mia...

Tunajua mnapenda pesa...lakini TUWE NA UTU....
 
Halafu nasikia mbinu wanazotumia kuwaleta huku mjini ni kwenda kuwadanganya wazazi wao huko vijijini kwamba wanawachukua kwa lengo la kuja kuwapeleka kwenye matibabu na vile wazazi hali zao ni duni basi huwa hawana jinsi zaidi ya kutowa watoto wao.

#Mbayasanahii.
 
Nilikuwa msaidiaji mzuri nikiona walemavu wamepangwa juani hasa nikiangalia zile hali zao ila baada ya kujaga kuyagundua haya ndo ikawaga mwisho wangu wa kuwasaidia.

Mana nilichokuwa nakitowa hakiendi kumsaidia niliyemlenga zaidi ya kwenda mtu ambaye ni mzima na asiye na haja ya kusaidiwa.
Ulipata ujira wako mbele ya mola wako.
 
Aisee...sinto sahau siku moja natoka hospital general ..nikakutana na omba omba...mtu mzima hivi...

Akaniambia Dada naomba miambili Nile ukoko...Nina njaa..

Nlikua na elfu mbili tu ambayo Ni yangu.. nyingine nlikua nimagizwa matunda.

Daah nikamuona huruma..nikamwambia ngoja nitafute chenji..nikapata chenjii..nikamrudia alipokua amekaa..

Nlimkuta anahesabu hela kibao..buku buku..jelo, miambili ..yaani hela alizonazo Mimi Sina..

Aisee nilisikitika Sana...NIKASEMA dooh
Kweli.
 
Back
Top Bottom