TANZIA Leopold Kweyamba Lwajabe amekutwa amefariki Mkuranga baada ya kupotea wiki iliyopita

TANZIA Leopold Kweyamba Lwajabe amekutwa amefariki Mkuranga baada ya kupotea wiki iliyopita

Dar es Salaam. Mkurugenzi msaidizi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe amekutwa amekufa wilayani Mkuranga.
Taarifa za zilizotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja zimesema wamejiridhisha kuhusu kifo hicho, muda mfupi wakijiandaa kutoa taarifa ya kumtafuta.
“Alitoweka wakati fulani wiki iliyopita lakini akaonekana. Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake kutoka kazini. Alipoonekana alitakiwa kwenda kutoa maelezo polisi lakini kabla hajafanya hivyo, akapotea tena. Leo ilikuwa tutoe taarifa kwa vyombo vya habari kumtafuta,” amesema Mwaipaja.
Mkwaipaja amesema walisitisha kutoa taarifa hiyo baada ya kupokea fununu za mwili wake kuonekana huko Mkuranga hivyo wakatuma watu kwenda kujiridhisha na kukuta ni kweli. Kifo hicho kimethibitishwa leo, Julai 29.

R.I.P Eng LL.
Isman, Kilos, Mufind, Songe, Ihemb, Mbing nk na TZ nzima tutakukumbuka.
 
Wakuu, Habari zilitufikia hivi punde ni kwamba aliyekua mkuu wa Kitengo cha EU, Wizara ya Fedha Leopard Lwajabe Amekutwa Amefariki huko Mkuranga.

Lwajabe alitekwa na watu wasiojulikana Akiwa ofisini kwake baada ya kupigiwa simu Stoke nje ya Ofisi, Walimshikilia kwa siku 3 kisha kumutelekeza Nyumbani kwake Kinyerezi,Tabata. Baada ya ndugu na majirani kumuhoji alidai alichanganyikiwa tu.

Juzi alhamisi wiki iliyopita alitekwa tena na baada ya ndugu kutoa taarifa Polisi walisema wasubiri baada ya SAA 72, Leo hii Asubuhi mwili wake Amekutwa akining'inia huko Mkuranga.

Taarifa zaidi zinakuja
We are in the middle of the most shameless regime in Africa.
It will take the spilling of blood to do away with this blood thirst regime.
 
H
Awamu hii kama una mishe zako zinazokuingizia kipato ni vyema ukatulia, Mambo ya kujiingiza katika siasa mwisho wake ndio kama huu...

Kama huwezi kuisifia ni vyema ukaacha kujihusisha na siasa...

Apumzike kwa amani.
Hakuwa maana siasa kabisa.
 
Mara mkuranga umekutwa mwili, mara alirudishwa kwa kinyerezi akadai alichanganyikiwa! so which is which? au umechanganyikiwa wewe mleta habari? Ukiwa mwongo usiwe msahaulifu
Mara ya kwanza alirudishwa,ya pili kauliwa mkuranga.
 
Mkuu una uhakika gani watawala ndiyo wahusika,afu Tanzania siyo shithole.

Tanzania is a prison this time around!

Kama wewe huoni tatizo heri yako ndugu yangu!

Kama kuna utawala tumeuweka madarakani utulinde na kusimamia kila kitu,then mambo mabaya yanatokea consistently ndani ya nchi,then ni state sponsored,aidha directly which is true au by their sheer neglect kutimiza mandate tuliyowapa!

Tanzania at the moment declared under totalitarian dictatorship,hii huwezi kubisha!

Sometimes uwe honest!
 
Mwili umepatikana tangia Jumamosi asubuhi
pole mno kwa wafiwa,BUT mtu ameripotiwa kupotea na jeshi la polisi linawajibu wanandugu wasubiri kwanza 72hrs ndio msako uanze,tukiambiwa tunaishi in a pithole country tunalalamika mno,common police mtu akipotea msako unaanza straight sio kusubiri,huyu atakuwa ni another Akwilina,tutamsahau punde ,maana sisi ni mahodari wa kulalama mitandaoni.
.
 
Hakuna aliye salama, halafu hii kasumba ya watu kutekwa wakirudi hawataki jamii ijue kilichoendelea ndo mbaya maana watekaji wanaendelea kuwa salama bila kujulikana! Huyu karudishwa kakataa kuwataja matokeo wamemuibukia tena na kumuua, hakuna wa kutusemea maana hata rais mwenyewe hajawahi kuguswa n utekaji, utasikia hata vyombo vya dola vikisema huyu kajiteka na baadae kajiua, huu ni ushetani tuukemee
 
Habari mbaya sana hizi..kutokea katika zama hizi..
Hivi tunaelekea wapi kama taifa...?
Hivi hawa wanaodhani kuwa wamesimama leo; wanadhani kuwa watasimama milele..??
Anyway; mimi sitajifanya jiwe...
Itafikia mahali watanzania wengi hawataogopa kifo kama mimi..
Tutawasubiri; waje watuue wote!
 
Back
Top Bottom