Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
afrodenzi, ni kweli unachosema kwasababu tumejitolea sana katika muungano.Malalamiko hayataisha hata kama Muungano utavunjika..
we are like "Big Brother" to them (Zanzibar) kwa hiyo hata huo muungano
ukivunjika bado watakuja na malalamiko mengine mfano tumewanyonya ,
umaskini uliopo Zanzibar ni ajili ya Bara.
"Tuwalipe" .... Swali Je hata huu Muungano ukivunjika , wataacha ku lalamika???
nionavyo binafsi La.
Wamedai bendera, wimbo wa taifa, vyombo vyao kama BPZ, ZRA, taasisi zao na hata kubadili katiba peke yao.
Wametupiga marufuku mambo mengi ingawa wao ni wanufaika. Hakuna wanachodai na hawajapewa lakini bado wanalalamika.
Malalamiko yao ni kama kuwa na IGP, waziri wa mambo ya nje, kiti EAC,UN n.k
Tutakapo waacha wawe wenyewe watakuwa katika nafasi nzuri sana ya kuelewa muungano ulikuwa na maana gani.
Watakuwa katika nafasi ya kulinganisha kati ya sasa na zamani
Ikifika hapo watapatwa na aibu ya kusota vidole maana hawatakuwa na la kusema
Lakini la muhimu zaidi tutapata nafasi ya kushughulikia matatizo yetu wenyewe.
Tunayo mengi na muda wa kubembeleza mtoto mgongoni hatuna.
Kwanini tusifikirie matatizo ya watu milioni 40, tubaki tunacheza mdumange na watu laki tisa na nusu
Hatari ya kuendelea kuwa nao ni pamoja na wao kusambaza mbegu za ubaguzi. Watu wanaojiona ni bora kuliko wanadamu wengine ni hatari sana. Watakapomaliza kuwafurumisha Watanganyika wataendelea kuvuka mipaka ili kusambaza sumu.
Tunajua wanapenda kuishi katika makundi kama kule makorora, msasani, Ilala n.k. Ipo siku watawafukuza wakazi a makorora kwasababu tu hawana imani yao. Ipo siku wataomba Morogoro iwe sehemu za Zbar kwasababu tu kila wanachoomba wanapewa.
Ipo siku tutasikia UAMSHO Tanzania bara ikiwataka machogo na wakristo wahame pwani kwani ni sehemu ya sultan, wao wanaamini huwezi kuwa mchaga mwislam na hata ukiwa basi utakuwa na uwalakini kwasababu siyo Mzanzibar ambaye ni bora.
Na mwisho tujiulize hivi sisi tunapata nini kutoka Zbar? Tutaendelea kulipa mishahara, umeme, ulinzi, wastaafu, gharama za elimu n.k kwa ujira wa matusi,ubaguzi, kashfa hadi lini?
LET ZBAR GO