Asante kwa kupaza sauti, lakini kosa la sauti hii ni kuutuhumu au kuituhumu serikali Moja kwa moja. Hamuoni kwamba inawezekana maadui wa utawala wa mama Samia pia wanaweza kufanya hivyo ili kuuchafua utawala wa mama kwa kuwa watanzania wengi wameanza kupata matumaini?
Kwa nini hamkuwatuhuhumu wasiojulikana moja kwa moja? Hivi hatujui kwamba kipindi hiki mama ana wakati mgumu sana wa kututoa huko tulikotoka?
Nchi imetoka kufiwa na Rais hivi karibuni, mama ametwaa utawala hivi karibuni baada ya kufiwa, hata nusu mwaka hajamaliza tunaanza kumtwisha mituhuma kibao, hivi lengo letu ni nini watanzania?
Mnachosha mpaka akili. Kila mtu anajifanya anajua, ebu mwacheni mama atutengenezee nchi bwanaaa aha!