Mulamula, nafasi imezidi uwezo wa akili yake.huyu mama mulamula nikimtazama simuelewi naona kajaa stress na anamponza shogaake 😎
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mulamula, nafasi imezidi uwezo wa akili yake.huyu mama mulamula nikimtazama simuelewi naona kajaa stress na anamponza shogaake 😎
Kuna kitu kimoja ambacho nakichukia kupita kiasi katika maisha yangu ya U-Tanzania. Hiki ni kauli za Polisi au wanasiasa pale ambapo wanajaribu kuficha au kupotosha ukweli ambao ukiwekwa wazi wananchi wataona wanavyokiuka haki za msingi za Watanzania, wanavyokandamiza demokrasia au hata wanavyofanya uhalifu kama wanasiasa au polisi.
Nadhani mmesikia kauli za polisi za "waliuwawa katika mapambano makali ya silaha na polisi na hakuna askari aliyejeruhiwa", "aliuwawa na kitu cha ncha kali tunafanya uchunguzi", "alikufa kwa kujaribu kuruka toka kwenye gari akiwa na pingu" nk.
Na pia kauli za wanasiasa kama "kama hutaki tozo nenda Burundi"; "kama huna nauli piga mbizi"nk.
Sasa leo nimekutana na kauli ya Waziri wa Mambo ya Nchi za nje, Liberata Malamula, akijaribu kueleza kwa nini mkutano kati ya Raisi Samia na wapinzani haukutokea. Anasema "Raisi Samia alipanga kukutana na wapinzani lakini ratiba zikaingiliana". Hivi huu mkutano ulikuwa ufanyike kwa muda gani, miezi sita mfululizo?
Ni wazi kwamba hawa watu wanapotoa hizi kauli wanaona sisi Watanzania ni wajinga, hatuna akili na tanakubali lolote tutakalowaambiwa.
Kwa kiingereza huwa ni ni falsafa ya "insulting Tanzanians' intelligence"
Napenda kwa mara nyingine niwaambie Polisi na Wanasiasa jambo moja, kwamba mtitutukane Watanzania, msidhani kwamba hatuna aiki, na msione upole wetu na utunzaji wetu wa hali ya amani nchini kuwa ni watu ambao tupotupo tu kama mazezeta. Uvumilivu wa kutukanwa una mipaka yake, na mnatutukana sana kwa hizi kauli zenu.
Hizi ni kauli zinafanya niwachukie wanasiasa na polisi kwa kiwango cha juu kabisa, kwa kuwa ni kauli ambazo naziona kama matusi kwa Watanzania. Ninavyozitafsiri mimi ni kwamba mnatoa kauli kama hizo eidha kwa kuwa nyie hamna uwezo wa kufikiri, au kwa kuwa mnadhani sisi Watanzania hatuna uwezo wa kufikiri. Jitafakarini sana. Tanzania ya 2021 sio Tanganyika ya 1961. We are not naive - you are disgustingly naive.
Heshima haiombwi wala kulazimishwa bali inatengenezwa na matendo yako.Uwe na heshima kwa Mheshimiwa Rais wetu. Ni Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, sio samia.
Amandla...
Hao wote ni satanic syndicate. Wasubiri malipo yao hapa Duniani na ahera. Mmoja wa washauri wake wa siri, ameuawa jana. Maisha ya Duniani ni mafupi sana, jitahidi utende wema. Unakuja wakati utaomba ungerudi kwenye nafasi uliyokuwepo ili ukafute uovu wako, lakini hutaupata.ni bola hajaongea nao kwanza,maana Kama angeongea nao,halafu inakuja kugundulika mwejekiti wao ni gaidi suspect,nadhani ingeleta taswira ya sintofahamu zaidi.nadhani wadukuzi walimtonya mama asikutane nao Kuna Mambo wameyadukua kwa Mr hai si shwari kukutana nao kwa Sasa!
Nani huyo?Hao wote ni satanic syndicate. Wasubiri malipo yao hapa Duniani na ahera. Mmoja wa washauri wake wa siri, ameuawa jana. Maisha ya Duniani ni mafupi sana, jitahidi utende wema. Unakuja wakati utaomba ungerudi kwenye nafasi uliyokuwepo ili ukafute uovu wako, lakini hutaupata.
Umeishia darasa la ngapi? Siku hizi JF imekuwa kokoro. Limekusanya hata watu ambao hawajui kuandika vizuri. Ile JF ya Home of great minds inazidi kupotea.ni bola hajaongea nao kwanza,maana Kama angeongea nao,halafu inakuja kugundulika mwejekiti wao ni gaidi suspect,nadhani ingeleta taswira ya sintofahamu zaidi.nadhani wadukuzi walimtonya mama asikutane nao Kuna Mambo wameyadukua kwa Mr hai si shwari kukutana nao kwa Sasa!
Laana kubwa ya Taifa hili, ni kukosa viongozi wenye uwezo. Kwenye uongozi wapo low minds ambao hawawezi kuipeleka nchi mbele.Hivi kweli kwa akili za Hawa viongozi tutapata maendeleo kweli,siasa za kishamba zinalingamiza Taifa.
Leta hoja ujibiwe, sio unajiumauma. CHADEMA wameweka mambo yao wazi. Wanakamatwa, wanauwawa, wanapotezwa, wanateswa, wamekomaa kwenye reli. Hawana kichaka cha kujificha, wala hawana haja wala mpango. Sasa Serikali mara oohh, tutakutana na wapinzani. Mara oooh, chokochoko zimeanza, wananchi wapuuzeni hao, wana pa kukimbilia na wana hela za kujitibia tukiwajeruhi. Mara ooohhh, tulitaka kukutana nao, ratiba ilibana. Ni nani hasa anayejificha vichakani? Siyo CHADEMA , ni Samia na serikali yakeVichaka vya kujificha mtavipata vingi tu-
UtanzaniaU-Tanzania
Mkuu, kwelikweli kuna haja ya kuwa na msamiati huu, Utanzania ukimaanisha uzezeta wa kukubali kila kitu. Mie naona ndivyo tulivyo WatanzaniaUtanzania
Wanauddhi sana Mkuu, wanaudhi hasa. Kwa nini usitoe sababu ambazo zina mshiko kama unataka kudanganya?Hakuna emoji inayofaa Ku-express emotions zangu, uneandika vizuri kabisa asante!
Basi ni bora hata aseme wazi, sina mpango wa kukutana na mtu yeyote. Lakini wanapokuja na utumbo wa maelezo kama huu wanatuletea harufu mbaya tu, hata kama sisi sio watu wa upinzani. Waelewe kwamba haya ni masuala yanahusu nchi yetu, hawa Wapinzani ni Watanzania pia, sio wapinzani wa kutoka Burundi wanakotaka twende. Wapinzani wakichachamaa tunaoathirika ni Watanzania wote.Samia aendelee kuonea wapinzani kwa sababu kashika Bunduki na Mabomu,wala siye hatuna shida ya kukutana na Samia,hana faida yoyote kwa Taifa aende zake huko
😅😅Angalia hizi kauli!Serikali ya Tanzania huwa inaamini kuwa wananchi ni wajinga kupindukia.
View attachment 1880889
Hahaha umeongea ukweliBasi ni bora hata aseme wazi, sina mpango wa kukutana na mtu yeyote. Lakini wanapokuja na utumbo wa maelezo kama huu wanatuletea harufu mbaya tu, hata kama sisi sio watu wa upinzani. Waelewe kwamba haya ni masuala yanahusu nchi yetu, hawa Wapinzani ni Watanzania pia, sio wapinzani wa kutoka Burundi wanakotaka twende. Wapinzani wakichachamaa tunaoathirika ni Watanzania wote.
Mie sidhani kama amezungukwa na watu wajanja kiasi hicho. Hata kama waliomzunguka ni wajanja kwa kiasi fulani, inawezekana kabisa tatizo basi ni yeye kutotambua ujanja wa watu waliomzunguka. Sasa tuna neno linalosema mtu wa namna hiyo ni nani.Wanaofaidika na hizi distractions ni wengi mkuu.
Ufalme ni gharama sana, Natamani Rais Samia angejua hilo. Amezungukwa na watu wajanja sana.
Blessed country [emoji17][emoji17]Tanzania