Liberata Mulamula: Rais Samia alipanga kukutana na wapinzani lakini ratiba zikaingiliana



Tulishasema kuna watu wengi walikuwa wananufaika na uhasama. Wametumia mwanya huu kupata pesa za kunua vitu kama teknologia ya kurekodi watu, kununua wapinzani...... wote hawa watakosa kazi
 
Uwe na heshima kwa Mheshimiwa Rais wetu. Ni Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, sio samia.

Amandla...
Heshima haiombwi wala kulazimishwa bali inatengenezwa na matendo yako.

Kwa ukigeugeu wake, maneno yake kuwa tofauti na matendo yake, nani atamheshimu? Hapa ndani atasifiwa na kuheshimiwa na wanafiki, watu wajinga, na wanaojikomba kwake kutafuta teuzi, lakini siyo na watu wenye good free brain. Huko nje amekwishaanza kudharaulika sana, na ataendelea kuwa hivyo.
 
Hao wote ni satanic syndicate. Wasubiri malipo yao hapa Duniani na ahera. Mmoja wa washauri wake wa siri, ameuawa jana. Maisha ya Duniani ni mafupi sana, jitahidi utende wema. Unakuja wakati utaomba ungerudi kwenye nafasi uliyokuwepo ili ukafute uovu wako, lakini hutaupata.
 
J
Nani huyo?
 
Umeishia darasa la ngapi? Siku hizi JF imekuwa kokoro. Limekusanya hata watu ambao hawajui kuandika vizuri. Ile JF ya Home of great minds inazidi kupotea.
 
Hivi kweli kwa akili za Hawa viongozi tutapata maendeleo kweli,siasa za kishamba zinalingamiza Taifa.
Laana kubwa ya Taifa hili, ni kukosa viongozi wenye uwezo. Kwenye uongozi wapo low minds ambao hawawezi kuipeleka nchi mbele.
 
Vichaka vya kujificha mtavipata vingi tu-
Leta hoja ujibiwe, sio unajiumauma. CHADEMA wameweka mambo yao wazi. Wanakamatwa, wanauwawa, wanapotezwa, wanateswa, wamekomaa kwenye reli. Hawana kichaka cha kujificha, wala hawana haja wala mpango. Sasa Serikali mara oohh, tutakutana na wapinzani. Mara oooh, chokochoko zimeanza, wananchi wapuuzeni hao, wana pa kukimbilia na wana hela za kujitibia tukiwajeruhi. Mara ooohhh, tulitaka kukutana nao, ratiba ilibana. Ni nani hasa anayejificha vichakani? Siyo CHADEMA , ni Samia na serikali yake
 
Kuna mawili. Kwanza, kwa bahati mbaya tumejenga jamii ambayo wanaofika kwenye ngazi za juu za uongozi sio ambao ni bora zaidi baina yetu kiuwezo na kifikra. Hata pale wanaporuhusu wenye fikra sahihi kufikia nafasi za uongozi, wananyimwa uhuru wa kufanya kazi kwa ubora na uwezo wao. Ni tokenism, wanawekwa huko ili watumikie maslahi ya wanaowaweka.
Pili, kwa muda sasa, wanaotuongoza hawatuheshimu. Mkataba wa viongozi na wanaoongozwa, na mahusiano baina ya pande hizo mbili sio mahusiano respectful. Kiongozi anapozungumza na umma, kichwani kwake anamuona mtu duni kwake kifikra. Kwa namna moja wanaweza kuwa sahihi kwa sababu kiwastani, uwezo wa kufikiri wa average Tanzanian uko chini ukilinganishwa na ule wa average kiongozi. Matokeo yake ni kauli unazozizungumzia za polisi na wanasiasa. Kwa namna fulani, hii state of affairs inaakisi kukosa kwao uwezo wa kuongoza na pengine ni hali ambayo wanai encourage kwa sababu inawanufaisha. Isingekuwa hivyo, ungeona sauti za wenzetu wenye fikra sahihi na uwezo wa kufanya mijadala inayohoji hizi kauli za viongozi zikipewa nafasi zaidi kwenye vyombo vyetu habari ili hata wale wasio na uwezo wajifunze. Na pia ubora wa elimu wanayopewa watoto wetu usingekuwa ulipo.
 

Pichani, Mzalendo akiwa Mazungumzoni na Beberu .

Hivi wenzetu ni kwamba wanatuoni ujinga wetu lakin wanatupotezea na kutucheka sana.
 
Samia aendelee kuonea wapinzani kwa sababu kashika Bunduki na Mabomu,wala siye hatuna shida ya kukutana na Samia,hana faida yoyote kwa Taifa aende zake huko
Basi ni bora hata aseme wazi, sina mpango wa kukutana na mtu yeyote. Lakini wanapokuja na utumbo wa maelezo kama huu wanatuletea harufu mbaya tu, hata kama sisi sio watu wa upinzani. Waelewe kwamba haya ni masuala yanahusu nchi yetu, hawa Wapinzani ni Watanzania pia, sio wapinzani wa kutoka Burundi wanakotaka twende. Wapinzani wakichachamaa tunaoathirika ni Watanzania wote.
 
Hahaha umeongea ukweli
 
Wanaofaidika na hizi distractions ni wengi mkuu.

Ufalme ni gharama sana, Natamani Rais Samia angejua hilo. Amezungukwa na watu wajanja sana.
Mie sidhani kama amezungukwa na watu wajanja kiasi hicho. Hata kama waliomzunguka ni wajanja kwa kiasi fulani, inawezekana kabisa tatizo basi ni yeye kutotambua ujanja wa watu waliomzunguka. Sasa tuna neno linalosema mtu wa namna hiyo ni nani.
 
Wapinzani nawafananisha na abiria ndani ya boti wotw tupo safarini halafu anatokea abiria mmoja anaanza kutoboa boti mpinzanianaanza kufurahia kama zuzu kana kwamba hajui kitakachokuja kutokea kitawakumba wote........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…