Khanji kapoor
JF-Expert Member
- Oct 19, 2024
- 3,861
- 9,909
Nyeghe..!!Habari zenu ndugu zangu ,
Habari za Mfungo wa Ramadhan &Kwaresma!
Swali hili nimekuwa nikijiuliza na kupata maono ya watu wengi hasa wazungu : Ni kipi kinafanya watu kuletana kwenye dunia yenye matatizo lukuki.
Wazungu wengi wanaonekana wanapinga huu mfumo kwa kuhofia uelekeo wa dunia ni kuja kuwatesa watoto.
Kiuhalisia mimi mambo nisiyoyapenda sipendi mwingine yamtokee never katika maisha , uzoefu wa maisha yangu ni kwamba maisha ni ya hovyo; hayana furaha muda wote hata upate vitu vyote ,umaskini ,magonjwa ,upweke ,shida na mihangaiko,kejeli ,ulemavu , utapeli ,mauaji , utapeli ,unyonyaji.
Yote hayo bado binadamu tunapambana kuzaa tena kwa kuwa na furaha kabisa kuzaa watoto...Je, huu ni ubinafsi au laah.
Binafsi Mtu akijiua naona kafanya jambo la maana sana ,utawezaje kuvumilia vitu vinavyokutesa huku ukipewa motives za kinafiki..Mifumo inayotaka watu wazaliane ni mifumo inayotaka kupata faida; serikali (kupata kodi na kuendeleza taifa) , wazazi(kupata watumwa kama wasaidizi wa kuwasumbua wakiwa wazee) , matajiri (kupata cheap labor na wateja wa bidhaa zao?
Je , mtoto unayemzaa ataweza kuvumilia yote hayo ? Na kwa nini kusiwe na chaguo la mtu kuzaliwa?
Ila sii mnyama CcmKila mnyama anayo akili kwenye zone yake
Ataweza vizuri tu.Je , mtoto unayemzaa ataweza kuvumilia yote hayo?
Inaonekana kuna jamii ya siri inategemea sana uzao wa wanadamu ili kusavaivu 😁Pyramid scheme proved ,ukitaka kujiua unapewa vitisho kibao ,mwishoe utakufa tu ...wastage of time kwa kweli.
Wabinafsi sana ; mtu anazaa watoto wanakuja kuishi maisha ya ajabu ,yeye furaha yake kuwaona maana ni kama watumwa wake .Wengine hawajitambui,na wanadanganyika katika imani walipo kuwa mpo kuongezeka na kuijaza dunia bila kuangalie uwezo wa kuihudumia dunia iliyojazwa.
Nini faida ya kizazi cha binadamu kuendelea kuwepo miaka yote hapa ulimwenguni?Ataweza vizuri tu.
Kuzaliana ni lazima iwe kizazi cha binadamu ukiendelee kuwepo hayo mengine yanatatulika vizuri sana.
😂😂😂Unasikia ''Nina watoto watatu bado wawili wafike 5 '' kama ni jambo lina ulazima fulani hiviNilipata watoto kipindi sijajitambua... Ungekuta ndio kipindi hiki hata iweje nisingekubali kaleta wapendwa wangu kwenye huu ulimwengu wenye kila aina ya hatari... Alafu hiki kitu sio kwamba watu hawajui sema ndio hivyo wanafarijiana upumbavu wakati ni kitu kipo wazi kabisa kwamba kukubali kuzaa au kuzalisha ni kama kujikuta gerezani alafu ufanye juu chini umlete mpendwa wako aje kuishi humohumo gerezani
Tule ugali halafu tufe mkuu, inawezekana hata hatupo ni illusion tu🤣Nini faida ya kizazi cha binadamu kuendelea kuwepo miaka yote hapa ulimwenguni?
Ni kwamba baadaye maisha yatakuwa magumu mara mbili ya sasa ; kuingia mifumo AI ,ongezeko la watu kuliko rasilimali ,kutoweka mifumo wa kifamilia (kuishi kwa ndoa).Ataweza vizuri tu.
Kuzaliana ni lazima iwe kizazi cha binadamu ukiendelee kuwepo hayo mengine yanatatulika vizuri sana.
Faida za kizazi cha binadamu kuendelea kuwepo ulimwenguni ni nyingi, na zinahusiana na maendeleo, ustawi wa maisha, na hatima ya sayari yetu. Baadhi ya faida hizo ni:Nini faida ya kizazi cha binadamu kuendelea kuwepo miaka yote hapa ulimwenguni?
Ingekua ni lazima, basi kila mwanadamu angekua amezaa kabla ya kufaAtaweza vizuri tu.
Kuzaliana ni lazima iwe kizazi cha binadamu ukiendelee kuwepo hayo mengine yanatatulika vizuri sana.
Inasikitisha sana😂😂😂Unasikia ''Nina watoto watatu bado wawili wafike 5 '' kama ni jambo lina ulazima fulani hivi
Kwa sababu hata dhana nzima ya akili ni binadamu tu ndie alieitolea tafsiriHakuna mnyama mwenye akili kumzidi binadamu.
Sio wote wanaojaliwa hiloIngekua ni lazima, basi kila mwanadamu angekua amezaa kabla ya kufa
Achana na mtizamo ya AI, wewe kama wewe kwa mtizamo wako binafsi zipi faida za binadamu kuendelea kuwepo ulimwenguni wakati wote?Faida za kizazi cha binadamu kuendelea kuwepo ulimwenguni ni nyingi, na zinahusiana na maendeleo, ustawi wa maisha, na hatima ya sayari yetu. Baadhi ya faida hizo ni:
1. Kuendeleza Maarifa na Teknolojia
Kizazi baada ya kizazi, binadamu wamekuwa wakigundua na kuendeleza teknolojia mpya, sayansi, na falsafa. Bila kizazi kipya, maendeleo haya yangesimama, na ulimwengu ungebaki katika hali duni.
2. Kuendeleza Ustaarabu na Utamaduni
Binadamu hujenga na kurithisha tamaduni, sanaa, lugha, na historia kwa vizazi vijavyo. Ustaarabu unakua kupitia elimu, fasihi, muziki, na mila, ambazo haziwezi kudumu bila kizazi kipya.
3. Kudumisha Maisha Duniani
Binadamu huchangia mazingira kwa njia tofauti, kama vile kutunza misitu, kuhifadhi wanyama, na kuendeleza kilimo endelevu. Bila binadamu, mfumo wa ikolojia unaweza kubadilika kwa njia isiyoeleweka.
4. Ugunduzi na Utafiti wa Maisha Nje ya Dunia
Binadamu wanaendelea kuchunguza uwezekano wa maisha katika sayari nyingine. Ikiwa kizazi cha binadamu kitaendelea kuwepo, kuna nafasi kubwa ya kugundua makazi mapya nje ya dunia.
5. Uendelevu wa Familia na Jamii
Familia na jamii zinategemea kizazi kipya kwa ajili ya kuendeleza mahusiano ya kijamii, kusaidiana, na kujenga mustakabali bora. Bila vizazi vipya, jamii zingeanguka na kupoteza mshikamano wake.
6. Kukabiliana na Changamoto Mpya
Binadamu hukumbana na changamoto kama vile mabadiliko ya tabianchi, magonjwa, na migogoro ya kijamii. Kizazi kipya huleta mawazo mapya na suluhisho za kukabiliana na changamoto hizi.
Kwa kifupi, kizazi cha binadamu kuendelea kuwepo ni muhimu kwa maendeleo, uendelevu wa jamii, na mustakabali wa sayari na ulimwengu mzima.
(Chatgpt)