Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #21
Anajichanganya yeye mwenyewe.
1. Anafukuza wamachinga bila kuwa na sehemu za kutosha kuwaweka, anataka wakale wapi?
2. Anafukuza wamasai ili kufurahisha mwarabu
3. Anafanya teuzi za ajabu ajabu. Sasa mtu kama Kingai alifaa kuwa na nafasi ile?
4. Anakumbatia wabunge 19 walioko bungeni kinyume cha katiba
5. Hana ubunifu wa vyanzo vya mapato, yeye kutwa kucha anakopa tu anakopa tu
6. Anatuwekea tozo na kodi za ajabu ajabu, Tozo kwenye miamala ya simu, tozo tukitoa pesa zetu benki, anatulipisha kodi ya jengo la mwenye nyumba pindi tukinunua LUKU
7. Anatangaza kutuongezea mishahara kwa 23.3% halafu anaenda kutuongezea buku kumikumi, kisha anaichukua juu kwa juu tukitoa pesa benki.
8. Sisi tunataka katiba mpya, yeye anajifanya kuunda tume mpya ya Mukandala wakati Jaji Warioba alishamaliza kazi!
Sasa mtu kama huyu tutaanzia wapi kumuelewa kwa mfano?
1. Wamachinga hawajafukuzwa isipokuwa waliambiwa wasizonge hifadhi za barabara.
2. Hajafukuza Wamasai isipokuwa wamepunguzwa na kuhamishwa waliokaribu au ndani ya hifadhi ya ngorongoro.
3. Kwenye Teuzi hapo sina chakuchangia, kwani ni ishu ya mtazamo wa mtu na mtu. Kwako anaweza kuwa mzuri Kwa mwingine akawa Mbaya.
Kuhusu kufuata sheria Kama ameteua waliopindisha sheria basi amekosea.
4. Wabunge 19 wapo chini ya mhimili wa Bunge na sio serikali.
5. 😂😂 Vyanzo vya mapato alivyobuni ikiwemo Tozo umeona Watanzania wakipiga mayowe. Akibuni vingine zaidi watu watajiua walahi😂
6. Tozo ndio ubunifu aliouona unaweza fanyika Kwa urahisi na Kwa watu wengi yaani kila mtu ni rahisi kuchangia nchi kupitia tozo Kama tuu atatumia Simu, Luku, bank n.k
7. 😀😀😀 Hapo sina chakumtetea.
8. Pia kwenye Katiba mpya sina cha kumtetea.