Ligi ya Morrison na Simba kwenye suala 'Release letter' imefikia patamu

Ligi ya Morrison na Simba kwenye suala 'Release letter' imefikia patamu

Timu inaenda kuwa kikundi cha vichaa. Manara+Morisoni + akili za mashaki wake = vichaa fc . Hatari Sana hii !!! Kuna siku timu itaingia uwanjani wakiwa wamevaa chupi tu.
 
Kumbe kusimamia sheria sikuhizi ni uswahili? Basi uswahili hautakaa uishe duniani hapa.

Hakuna upumbavu kufanya mambo kwa hisia wakati mwanzoni yalifanyika kisheria, kibyovyote vile Simba Sc ni lazima wahakikishe hakuna mlango wa kuja kusurubiwa na BM3 kama jinsi ambayo aliwafanya Yanga Sc.

Ili uone uzito wa hili swala, basi unapozungumzia hii issue, usisahau uhusiano mbovu uliopo kati ya Simba sc na yanga , lakini pia zingatia tabia husika ya mlengwa.
hiyo hiyo sheria Morison ndo aliwapiga nayo yanga , Simba hawajakosea mkataba uheshimiwe,nakumbuka wakati Yanga wanachukua wachezaji wa kigeni mwaka jana kuna ambao hawakucheza mechi na River United kwasababu release letters zilichelewa kutolewa na As Vita waliheshimu mkataba.
 
Kwahiyo kaishaitwa kusaini mkataba mpya baada ya awali unaoishia? Mchezaji hajaachwa inakuaje unamtakia heri ktika safari yake mpya ya soka?
wapi kwenye ile barua simba imesema wamemwacha? Soka ni biashara ,mkataba wa mchezaji haujaisha halafu anatakaje release letter ? Simba wameona kwa mda uliobaki kama kuna timu inamtaka kabla ya mda wake kuisha basi ivunje mkataba na walete offer ,mbona simple tu!
 
shida simba wanamkomoa bm kishamba sana
hv kweli unampa mtu barua last day
 
Mwisho wa kutuma Majina CAF ni tarehe 14 August 2022 na Yeye Mkataba wake na Simba SC unaisha tarehe 16 August 2022 hivyo asiwe na Wasiwasi huko Yanga SC anakotaka kwenda ataenda Kuchezea ile ya Vijana ambayo inaweza baadae ikashiriki Ndondo Cup au ataenda Kukaa mpaka Dirisha Dogo la January 2023 ndipo aende huko Yanga SC.

Na Mwambieni Tanzania nzima hakuna Timu inayojua Kumroga Mchezaji na Kumfunika kabisa asifanikiwe Kokote aendako kama akiondoka vibaya kama Simba SC na Simba SC huwa haiishii hapo tu bali ukifanya nayo Masihara unaweza hata hii dunia ukaiaga kama walivyoiaga Wanafiki akina Ngumi Jiwe barabarani.

Na Simba SC haina tu 'Mafia' na Watoto wa Mjini ( wa Kihuni ) bali pia ina Watu Wasomi na Walewa wa Masuala mno.
Njaa mbaya sana ulichokiandika hakifanani na Akili uliyonayo.Viposho vya Barbara vimechetua Akili yako.Mtake msitake Morrison atachezea Yanga na atawafunga goli zuri na litawakera sana mpaka mkome kudadadeki zenu.
 
Sioni sababu ya usajili wa Morison kuwa habari kubwa hivi na kuleta malumbano yasiyo ya msingi. Simba walishonyesha kuwa hayuko kwenye mipango yao ya mbeleni kwa maana nyingine hawamuhitaji na ana mkataba wake upo ukingoni. Yanga wameshaonyesha kuwa wanamhitaji. Na kweli ukiangalia winga za Yanga wakina Moloko na Chiko Ushindi ni kweli Morison anahitajika sana sana Yanga. Sasa kwa nini viongozi wa Yanga na Simba wasikae chini tena ndani ya dakika 10 tu wakalimaliza hilo suala ili kuwe na "win win" kila upande ili Simba wasiendelee kumlipa mshahara Morison kwa kipindi kilichobaki na Yanga waendelee pale Simba itakapoishia

Vinginevyo ninachokiona hapa ni utoto na uzamani zaidi kwenye hivi vilabu vyetu viwili badala ya kuleta weledi. Halafu kila siku hivi vilabu vinatamba kuwa vinaendeshwa kwa weledi na vinataka kuwa kama timu kubwa Afrika kama Al haly, Mamelod, n.k. Kwa mtindo huu na uswahili huu katu haiwezejani. Ifike mahali Simba waende Yanga waulize bei ya Fei toto wapewe wakiweza walipe wambebe na Yanga nao waende Simba waulize bei ya Inonga wakiweza walipe wasepe.

Wenzao huko South Afrika Kaizer na Mamelodi, n.k. wameshawapa mkono wa kwa heri wachezaji wote ambao hawapo kwenye mipango yao msimu ujao ili wachezaji wakatafute mapema maisha yao kwenye vilabu vipya ndio maana kuna tetesi kuwa Kambole kashasajiliwa Yanga. Hapa kwetu hawa mapacha wa kariakoo wapo radhi wamuongezee mkataba mchezaji ambaye hayupo kwenye mipango yao msimu ujao hata kama itawagharimu msimu mzima kwa hofu tu kuwa akienda kwa mpinzani wake anaweza akafanya vizuri halafu wao viongozi wakazodolewa na mashabiki na wanachama wao.
 
Ndio shida ya kukurupuka km huku ,Simba sio mafala kukomalia Sheria ifuatwe hawataki Kona Kona ili baadae yaje yawapate km watani zao.
Jamaa mwenyew mhuni mhuni haeleweki kwa usalma zaidi ni heri kanuni izingatiwe waachane kikanuni km walivyokutana kikanuni .
Muda mwingine huruma huponza ,baadae yakigeuka wote tutaanza kuwalaumu viongozi.
Ogopa Sana kitu kinachoitwa mkataba
Kama ameomba kwa maandishi sidhani kama kuna shida yoyote. Hapo kuna kaukanjibay.

Anyway, ni vizuri kuwatreat wachezaji tusiowahitaji vizuri sababu hata wachezaji wengine watajisikia wapo salama hata pale watakapoamua kutokuendelea na sisi.

Imagine wewe ni mchezaji mpya halafu unakutana na mwenzako aliyekuwa kama wewe anaomba release letter akacheze ila ananyimwa wakati hatumiki tena.
 
Kujua kuwa mchezaji umetangaza kuwa mmemsimamisha mpaka mwisho wa msimu na kutakia heri katika maisha yake mapya ya soka halafu unamnyima haki ya kusajiliwa na timu zingine kisa tu muda bado wa mkataba ni uswahili zaidi. Dirisha la CAF linafunguliwa tarehe 30 kwahiyo mpaka hapo Simba wanamkomoa Morrison asisajiliwe abakie hana timu
Hajanyimwa haki ya kusajiliwa na timu nyingine. Kinachotakiwa ni ile timu nyingine kuleta ofa yake kwa simba maana mkataba wa BM bado haujaisha. Hiyo timu inayomtaka inashindwa nini kuwasilisha maombi kwenye klabu ya simba na kuwasilisha ofa yake?
 
Kama ameomba kwa maandishi sidhani kama kuna shida yoyote. Hapo kuna kaukanjibay.

Anyway, ni vizuri kuwatreat wachezaji tusiowahitaji vizuri sababu hata wachezaji wengine watajisikia wapo salama hata pale watakapoamua kutokuendelea na sisi.

Imagine wewe ni mchezaji mpya halafu unakutana na mwenzako aliyekuwa kama wewe anaomba release letter akacheze ila ananyimwa wakati hatumiki tena.
Uzuri wachezaji wote wanayajua matatizo ya Bernard Morrison.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
HAKUNA mwenye Shida na Hilo Hata leo Simba wametoa taarifa Kwamba Morrison Ni mchezaji halali wa Simba na analipwa mshahara km kawaida.

Kama unamtaka kwa Sasa angali ktk mkataba Halali lazima uje MEZANI Biashara ifanyikie. Kinyume na hapo usubiri mkataba wake uishe umchukue akiwa huru. Kitu rahisi tu, HAKUNA njia ya mkato. Morrison na Yanga wanajua hilo. Wanataka tu kutingisha kiberiti. Ni ushamba Yanga na Morrison wanafanya.
Simba hatumuitaji tena, Mor anaweza kuomba kuvunja mkataba awe mchezaji huru na tukampa taratibu ila hatutaki kwa sababu tunajua anaenda kuwachezea kandambili. Tùnamkomoa tu na kuna kaukanjibay, Kama ushafanya kazi na wahindi utaelewa.
 
Simba wako sahihi kukausha hadi mkataba wa Morson utapoisha.

Kikanuni, Mchezaji anaetaka kuondoka hana haki ya kuomba Release Letter.

Club mpya inayomtaka mchezaji ndio inayotakiwa kutoa taarifa ya nia ya kumuhitaji mchezaji, kisha iombe release letter. (Yanga haina mahusiano mema na Simba ndio maana inapata ugumu)
Morison ana shida mingi sana ya kimaadili, no wonder sauzi hawamtaki kabisa.
 
Hajanyimwa haki ya kusajiliwa na timu nyingine. Kinachotakiwa ni ile timu nyingine kuleta ofa yake kwa simba maana mkataba wa BM bado haujaisha. Hiyo timu inayomtaka inashindwa nini kuwasilisha maombi kwenye klabu ya simba na kuwasilisha ofa yake?
Uto wakituletea maombi tutawapiga na kitu kizito hilo lipo wazi. Njia rahisi ni kwa mchezaji kuomba avunje mkataba kisheria.
 
CAF YATUMA BARUA YANGA SC 🔖

Kocha msaidizi wa Yanga SC Cedric Kaze 🇧🇮 akiongea na wanahabari leo amethibitisha kuwa klabu ya Yanga SC 🇹🇿 imepokea barua kutoka (CAF) ikiwataarifu kuwa wamesogeza mbele michuano ya (CAF) na dirisha la usajili Kuelekea msimu ujao (2022/23)

Amesema (CAF) wamesogeza mbele kwa mwezi mmoja michuano ya klabu bingwa Africa na kombe la Shirikisho.

Michuano hiyo itaanza September 9 hadi 11/2022 badala ya August 12/2022 kama ilivyokuwa imetangazwa awali.

Mabadiliko hayo yamepelekea kusogezwa mbele pia kwa DIRISHA LA USAJILI ambalo sasa litafunguliwa August 1/2022 hadi August 15/2022 kwa timu kusajili pasipo kupigwa faini yoyote na (CAF)

Ni ruksa sasa kuanza kusajili Wachezaji kuanzia July 1 hadi August 15/2022.

Baada ya August (15/2022) klabu zitalazimika kulipa faini ya USD $ 5,000 kwa kila mchezaji ili kuingiza majina kwenye mfumo wa CAF ndani ya siku (10)

Cedric Kaze amesema (CAF) wameisaidia Yanga SC kujiandaa vizuri kwa kuhakikisha wanasajili Wachezaji bila shinikizo kuelekea michuano ya klabu bingwa Africa.
Haya sasa. Hana hata haja ya kuomba tena kuvunja mkataba. Tunalipa mshahara wa bure.
 
Yanga kama wanamtaka kwa haraka wampe pesa BM ili anunue sehemu ya mkataba uliobaki pale Simba! Sasa wanabaki wanapiga makelele tu na kulalamika bila kuchukua hatua. Katika ulimwengu wa soka pesa ndiyo huzungumza! hata kama mchezaji ana mkataba wa miaka mitano bado pesa inaweza kumng'oa!! Ila kuhama bila pesa hilo jambo halipo kwenye ulimwengu wa soka. Inabidi asubiri mkataba ubaki na siku sifuri ili aondoke kwa bei ya sifuri, kinyume cha hapo ni kupoteza muda tu!
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Yanga kama wanamtaka kwa haraka wampe pesa BM ili anunue sehemu ya mkataba uliobaki pale Simba! Sasa wanabaki wanapiga makelele tu na kulalamika bila kuchukua hatua. Katika ulimwengu wa soka pesa ndiyo huzungumza! hata kama mchezaji ana mkataba wa miaka mitano bado pesa inaweza kumng'oa!! Ila kuhama bila pesa hilo jambo halipo kwenye ulimwengu wa soka. Inabidi asubiri mkataba ubaki na siku sifuri ili aondoke kwa bei ya sifuri, kinyume cha hapo ni kupoteza muda tu!
Sababu ya kumtaka kwa haraka si ndo hiyo imesogezwa mbele? Watamsubiri tu huku sisi tunampa mshahara.
 
nyie Makolo wapumbavu sana tena wapuuzi wa mwisho, hata hamjui sheria za CAF zinasemaje, kwa taarifa yenu YANGA na Morrison wanawacheka tu. Kasomeni sheria za CAF wajinga nyie, "ukimsajiri mchezaj ambaye mkataba wake umebaki mwezi mmoja kuisha na mchezaj hatak tena kuendelea na hiyo club, Team inayotaka kumsajiri itatozwa Faini ya Million 11 na CAF na mchezaj huyo atakubaliwa usajiri wake mpya." Na makolo mlivyo wapumbavu zaid mkatoa hadi Public Notice 😂 kuwa mmemalizana na Morrison na mnamtakia maisha mema... Sasa kwa akili zenu fupi mnadhan Yanga itashindwa kulipa faini ya million 11..?😅😂 Mnajua GSM, Eng Hersi, Suma..?
Kwa ulichoandika hapa hujioni Kama wewe ndio mjinga na akili fupi? Unawatazama wenzako namna hiyo wakati unadhihirisha ujinga wako kwenye maandishi yako.
 
Mjadala walisha ufunga CAF Kwa taarifa Yao ya kusogezwa mbele dirisha la usajili.
Maana yake Yanga watampata Morrison. Freee bila kutumia nguvu yoyote.
 
Back
Top Bottom