Ligi ya Morrison na Simba kwenye suala 'Release letter' imefikia patamu

Timu inaenda kuwa kikundi cha vichaa. Manara+Morisoni + akili za mashaki wake = vichaa fc . Hatari Sana hii !!! Kuna siku timu itaingia uwanjani wakiwa wamevaa chupi tu.
 
hiyo hiyo sheria Morison ndo aliwapiga nayo yanga , Simba hawajakosea mkataba uheshimiwe,nakumbuka wakati Yanga wanachukua wachezaji wa kigeni mwaka jana kuna ambao hawakucheza mechi na River United kwasababu release letters zilichelewa kutolewa na As Vita waliheshimu mkataba.
 
Kwahiyo kaishaitwa kusaini mkataba mpya baada ya awali unaoishia? Mchezaji hajaachwa inakuaje unamtakia heri ktika safari yake mpya ya soka?
wapi kwenye ile barua simba imesema wamemwacha? Soka ni biashara ,mkataba wa mchezaji haujaisha halafu anatakaje release letter ? Simba wameona kwa mda uliobaki kama kuna timu inamtaka kabla ya mda wake kuisha basi ivunje mkataba na walete offer ,mbona simple tu!
 
shida simba wanamkomoa bm kishamba sana
hv kweli unampa mtu barua last day
 
Njaa mbaya sana ulichokiandika hakifanani na Akili uliyonayo.Viposho vya Barbara vimechetua Akili yako.Mtake msitake Morrison atachezea Yanga na atawafunga goli zuri na litawakera sana mpaka mkome kudadadeki zenu.
 
Sioni sababu ya usajili wa Morison kuwa habari kubwa hivi na kuleta malumbano yasiyo ya msingi. Simba walishonyesha kuwa hayuko kwenye mipango yao ya mbeleni kwa maana nyingine hawamuhitaji na ana mkataba wake upo ukingoni. Yanga wameshaonyesha kuwa wanamhitaji. Na kweli ukiangalia winga za Yanga wakina Moloko na Chiko Ushindi ni kweli Morison anahitajika sana sana Yanga. Sasa kwa nini viongozi wa Yanga na Simba wasikae chini tena ndani ya dakika 10 tu wakalimaliza hilo suala ili kuwe na "win win" kila upande ili Simba wasiendelee kumlipa mshahara Morison kwa kipindi kilichobaki na Yanga waendelee pale Simba itakapoishia

Vinginevyo ninachokiona hapa ni utoto na uzamani zaidi kwenye hivi vilabu vyetu viwili badala ya kuleta weledi. Halafu kila siku hivi vilabu vinatamba kuwa vinaendeshwa kwa weledi na vinataka kuwa kama timu kubwa Afrika kama Al haly, Mamelod, n.k. Kwa mtindo huu na uswahili huu katu haiwezejani. Ifike mahali Simba waende Yanga waulize bei ya Fei toto wapewe wakiweza walipe wambebe na Yanga nao waende Simba waulize bei ya Inonga wakiweza walipe wasepe.

Wenzao huko South Afrika Kaizer na Mamelodi, n.k. wameshawapa mkono wa kwa heri wachezaji wote ambao hawapo kwenye mipango yao msimu ujao ili wachezaji wakatafute mapema maisha yao kwenye vilabu vipya ndio maana kuna tetesi kuwa Kambole kashasajiliwa Yanga. Hapa kwetu hawa mapacha wa kariakoo wapo radhi wamuongezee mkataba mchezaji ambaye hayupo kwenye mipango yao msimu ujao hata kama itawagharimu msimu mzima kwa hofu tu kuwa akienda kwa mpinzani wake anaweza akafanya vizuri halafu wao viongozi wakazodolewa na mashabiki na wanachama wao.
 
Kama ameomba kwa maandishi sidhani kama kuna shida yoyote. Hapo kuna kaukanjibay.

Anyway, ni vizuri kuwatreat wachezaji tusiowahitaji vizuri sababu hata wachezaji wengine watajisikia wapo salama hata pale watakapoamua kutokuendelea na sisi.

Imagine wewe ni mchezaji mpya halafu unakutana na mwenzako aliyekuwa kama wewe anaomba release letter akacheze ila ananyimwa wakati hatumiki tena.
 
Hajanyimwa haki ya kusajiliwa na timu nyingine. Kinachotakiwa ni ile timu nyingine kuleta ofa yake kwa simba maana mkataba wa BM bado haujaisha. Hiyo timu inayomtaka inashindwa nini kuwasilisha maombi kwenye klabu ya simba na kuwasilisha ofa yake?
 
Uzuri wachezaji wote wanayajua matatizo ya Bernard Morrison.
 
Reactions: Tsh
Simba hatumuitaji tena, Mor anaweza kuomba kuvunja mkataba awe mchezaji huru na tukampa taratibu ila hatutaki kwa sababu tunajua anaenda kuwachezea kandambili. Tรนnamkomoa tu na kuna kaukanjibay, Kama ushafanya kazi na wahindi utaelewa.
 
Morison ana shida mingi sana ya kimaadili, no wonder sauzi hawamtaki kabisa.
 
Hajanyimwa haki ya kusajiliwa na timu nyingine. Kinachotakiwa ni ile timu nyingine kuleta ofa yake kwa simba maana mkataba wa BM bado haujaisha. Hiyo timu inayomtaka inashindwa nini kuwasilisha maombi kwenye klabu ya simba na kuwasilisha ofa yake?
Uto wakituletea maombi tutawapiga na kitu kizito hilo lipo wazi. Njia rahisi ni kwa mchezaji kuomba avunje mkataba kisheria.
 
Haya sasa. Hana hata haja ya kuomba tena kuvunja mkataba. Tunalipa mshahara wa bure.
 
Yanga kama wanamtaka kwa haraka wampe pesa BM ili anunue sehemu ya mkataba uliobaki pale Simba! Sasa wanabaki wanapiga makelele tu na kulalamika bila kuchukua hatua. Katika ulimwengu wa soka pesa ndiyo huzungumza! hata kama mchezaji ana mkataba wa miaka mitano bado pesa inaweza kumng'oa!! Ila kuhama bila pesa hilo jambo halipo kwenye ulimwengu wa soka. Inabidi asubiri mkataba ubaki na siku sifuri ili aondoke kwa bei ya sifuri, kinyume cha hapo ni kupoteza muda tu!
 
Reactions: Tsh
Sababu ya kumtaka kwa haraka si ndo hiyo imesogezwa mbele? Watamsubiri tu huku sisi tunampa mshahara.
 
Kwa ulichoandika hapa hujioni Kama wewe ndio mjinga na akili fupi? Unawatazama wenzako namna hiyo wakati unadhihirisha ujinga wako kwenye maandishi yako.
 
Mjadala walisha ufunga CAF Kwa taarifa Yao ya kusogezwa mbele dirisha la usajili.
Maana yake Yanga watampata Morrison. Freee bila kutumia nguvu yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ