Lijue tatizo jipya la kisaikolojia ambapo mtu aliyepata "mafanikio" kwenye maisha yake huamini kwamba watu wake wa karibu wanamchukia

Hapa kuna kosa gani??
Kama amezaa na huyo mwanamke wake huoni kama ni vema sana hayo aliyoyafanya??
Mm nazani ameandaa mazingra mazuri ya watoto wake pindi watakapokuwa wanatembelea babu na bibi yao.

Unajisikiaje mjini mkae sehemu safi lkn kijijin ambako niko kwenye asili yenu kuko ovyo??
Mm binafsi nampongeza jamaa KWa kuweka mazingira rafiki KWa wanawe hapo mbeleni
 
Okay
 
Binafsi sikubaliani na hoja yako!

Na mimi ntatoa tu mfano mmoja kati ya michache niliyonayo...!

Nimezaliwa na kukulia Uswahilini, kama unavyojua Uswahili huwa kuna Vijiwe tofauti tofauti, ambavyo uhusisha watu wanaofahamiana, yani Mtu ataenda Mishe zake, ama mihangaiko yake, na ikifika mida flani unakuta kijiwe kimejaa, hawa wakipiga story hizi hapa, hawa wanaongea kuhusu hili n.k...!

Nilikua miongoni mwa Vijana wadogo kwenye Kijiwe hiki, na wengi wao walikua Ma brother!

Kuna siku anapita Brother akiwa na Usafiri, ndo Usafiri wake wa kwanza, kapaki kijiweni akashuka na kusalimia kila mtu, baadaye akaanza kumwambia Brother mwingine ambaye alikua Best yake sana, kwamba mbona hawatafutani, amtafute basi wapeane michongo, jamaa akamwambia u busy ndo unachangia (Japo hakuwa na issue yoyote, kula kulala).

Brother mwenye gari anamwambia yeye anaenda kumcheki Bi mkubwa wake kama vipi aje home kwao, jamaa akamwambia soon atakuja, basi yule Brother mwenye usafiri akaondoka, Kijiweni wakaanza kumjadiri, kwamba anafanya issue gani mpaka kanunua gari!?

Mwingine akaleta taarifa kijiweni tu kuwa sio gari tu, kanunua na Nyumba Mbezi Beach!

Mmoja akamwambia yule best yake wa muda mrefu kuwa aende home kwao, si kaambiwa kuwa atapewa Mchongo, jamaa akajibu "Aaah, siendi, ataona kama najikomba kwake..!"

Nikashuhudia mara nyingi jamaa akipita kijiweni kwenda kumsalimia Bi. Mkubwa wake lazima asimame ashushe Kioo cha gari asalimie, lakini kuna Mabrother pale kijiweni wengine wanajifanya hawajamuona au kusikia salamu yake, akipita yanaanza maneno, Jamaa atakua anajiskia sana sasa hivi n.k..!

Baada ya yule Brother kugundua kwamba watu pale Maskani ya Mtaa ambao amezaliwa kama vile hawajari hata salamu yake, akawa akipita anapiga tu Hodi... Mwendo.... Baadaye akawa hata Honi hapigi, anapita zake tu kwenda kumcheck Bi. Mkubwa wake...!!

Kuna watu hasa Waswahili mtu wa karibu akipiga hatua, wao ndo wanakua wa kwanza kujiweka mbali nae, halafu huku pembeni wanaanza kuongea maneno yasio na maana!!!

Badala ya kuendelea kuwa karibu nae ili kupata maujanja how come from no where jamaa kapata pesa....!

Na watu ambao wanajiweka mbali nawe, na wewe kaa mbali nao, coz ukilazimisha, wanaweza kukushusha kwa njia zozote zile ili muendelee kuwa level moja...!
 
Mimi nina pinga kichwa cha uzi wako,siyo ugonjwa bali ndio ukweli uko hivyo.
 
Utajiri wa ukubwani huwa una matatizo yake tofauti na ule wa kuukuta na kukua nao. Tajiri wa ukubwani hata ukimsalimia anaona unataka kumuomba hela
 
Sio kila sehemu kuna maeneo ambayo lazima uongee tu...

Sio kila sehemu kuna maeneo ambayo lazima uongee tu...

Mt 20:15 SUV​

Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?

Stori yako haitofautiani na majibu haya ya Yesu.

Mtu kama hafanyi uhalifu wala dhambi katika matumizi yake usimuingilie.
Hata ajenge maelfu ya nyumba Ukweni sio kosa kisheria za dini, nchi na popote pale.

Thamani unayoiona ya mzazi wako sio lazima yeye aione.
 
Hahahahahaha anatembea kama katoka kucheza ndondo....
Hapo kama namuona kwapa kalitanua kidogo kama ana vijipu uchungu vileee kwenye kwapaa
Miguuni kaunda tege flani hivi anadindika kama kangaroo
 
Hii psychology inanisumbua mie mno buy infact I have $250k kwenye akaunti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…