Lijue tatizo jipya la kisaikolojia ambapo mtu aliyepata "mafanikio" kwenye maisha yake huamini kwamba watu wake wa karibu wanamchukia

WhatsApp kulikuwa na group la familia sasa ikapita donation kila mtu lazima achangie 30k ya msiba wa bibi,ukichangia lazima group admin atoe mkeka wa watu waliotoa pesa.
Sasa watu wengi walikuwa wanalega lega sana kutoa na mambo mengi pale msibani yalikuwa hayaendi vizuri,nikasema ngoja niokoe jahazi tusijepata aibu bure nikachangia laki 9 badala ya elfu 30,kama kawaida group admin akafanya yake akaweka mkeka kuwa bwana mdogo David ametoa laki 9.....ebaana eeh nilipigwa vijembe sio vya dunia..utasikia watu wengine kwa kupenda sifa ameambiwa atoe elfu 30 yeye ametoa laki 9,mwingine anakuja quotes ule ujumbe anasema watoto wa siku hizi wana dharau sana...daaah
 
Mzee Likud umeonyesha tu unamchukia kaka yako. Mengine uliyoandika ni kama kusindikiza tu hii habari ya kumchukia kaka yako. Kama kujenga ukweni na kusomesha ndugu wa mke ni ABOMINATION basi watu wengi sana wameshafanya hilo kosa. Hata mimi kama nitaoa familia fukara nitawasaidia ninachoweza. Wewe LIKUD bado ni mtu maskini na hela huna. Umekuwa ukitetea shule za Kayumba kwamba ni bora kuliko za binafsi kwa kua umepigika. Kutoka nje ya Afrika sio ishu kabisa. Ni suala la kawaida mno. Punguza chuki kwa ndugu yako.
 
Amewajengea wakwe zake au amejijengea ya kwake ukweni?
 
Hao ndugu zako ni "wachawi", ingawa siwamaamishi wale wachawi "wengine".

Endelea na moyo huo hata katika mambo mengine. Bora uchukiwe kwa kutenda mema kuliko kusengenywa kwa sababu umetenda mabaya.
 
ur a poor judge of character
 
Duh pole sana mkuu
 
Familia yenu imejaa malimbukeni wengi sana

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi kabisa mkuu
 
Mafanikio yanaonyesha tabia yako halisi ambayo inafichwa na dhiki/shida.
 
True masikini mara nyingi tunajishtukia sana
 
Yaani kukosa pesa ndio chanzo cha matatizo ya afya ya akili
 
Mimi Sina maneno mengi ila wahenga wetu hawakukosea.

Mchumia ukweni, urudi na deni.

Hivyo kaka hizo Nyumba mbili sio za kwake Wala watoto wake.

Wakiachana leo na mkewe, yeye atapata thamani ya Nusu Nyumba ya mjini wakati automatic mkewe atakuwa na Nyumba mbili na Nusu.

Kuhusu elimu ni ukweli unamwonea kijicho
Na hili lipo wazi.
 
Ulivyoandika tu inaonesha dhahili unamchukia, sasa wewe Hadi kutembea unampangia atembee vipi? Acheni makasiriko na maisha ya watu...! Na hapo ulipo unaomba muda wowote limkute baya ili upate la kusema......si tulisema? Kiko wapi??
 
We na kaka yako acheni utoto
 
Kwanini kujenga ukweni ni vibaya mkuu? Mimi nina mpango huo siku za mbeleni maana kwetu mambo 'safi kiaina' ila mke wangu akienda kwao mpaka najisikia vibaya wanapolala watoto wangu maana ni nyumba mbavu za mbwa. Kuna ubaya gani nilijenga nyumba ndogo ya 15m Kwa mfano. Maana kwao hakuna mwenye uwezo wa kufanya hivyo....
 
Naskia ukifanikiwa unakua unadhani watu hawakuthamini tena, wanaishi na wewe kinafki ili wafaidi pesa zako.

Ndo maana wanasema 'It's lonely at the top'
Kuwa na fedha mfukoni ni kitu kingine kabisa. Kwa wanaume ni rahisi zaidi kujua hili. Ukiwa na fedha mfukoni unaweza kuwa na confidence ya kufa mtu na ukamwa-approch demu mkali sana. Au kwenye kikao unaweza kuwa na ujasiri wa kuwa mzungumza mkuu. Ukikosa fedha sasa... demu yule yule utamuona kama anadharau na hutathubutu hata kutoa salaam. Kikao ndiyo kabisa mtu anajificha na anaona aibu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…