Linasubiriwa tukio lolote litokee nchini Iran ili liunganishwe na shambulizi la Israel


Mkuu kifo ni kifo tu, alisikika mama yetu mmoja akituasa:

Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

Ukweli mchungu hii ni vita ya Marekani na Iran, hapo Israel ni kikaragosi tu:

Palestina ni wahanga, Iran na Israel hawachekani, ila Marekani wapewe maua yao

Kwamba Iran atapigwa pigo moja kali, litakalomwacha mfu au kilema asiweze kurusha ngumi moja punde baada ya hapo? Mbona itakuwa ni kujaribu kupaka rangi hewa kutotaka kulijua hilo?

Kwamba kuna mwenye shauku na eti popote alipo anashangazwa na chelewa chelewa ipi?



Kwani hujui kulikuwa na kimbunga Milton huko kwa mwenye vita vyake, ewe ndugu unayedhani vita ni kabumbu?
 
Umeandika gazeti, ila inashangaza kuona unaona ajabu nchi kushirikiana na washirika wake kuipiga nyingine. Kwani Iran imekatazwa kushirikiana na Marekani?
Iran inajiamini sana, ndomaana haina muda wa kushirikiana na nchi nyingine kuitwanga Israel. Mwenye nguvu huwa hashirikiani na mtu yoyote kumchapa mnyonge.

Lakini mnyonge ni kawaida kushirikiana na watu wengine kumchangia mwenye nguvu.
 
Mkuu umenena yani kwa sasa hata ikitokea ajali ya basi kupinduka utasikia MOSSAD HAO!!
Hiki kimbunga kinachotokea Marekani sasa hivi, kama kingetokea Iran saa hizi wangesema kuwa MOSSAD wapo kazini. Au ungesikia kuwa Mungu wa yakobo anaiadhibu Iran kwa sababu ya kushambulia Israel πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Anajifanya mbabe sasa tunataka kuona huo ubabe wake.
Kama kawaida yake akipigwa na mwenye nguvu hasira zake huzimalizia kwa kina mama na watoto huko Gaza na Lebanon πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ujinga mtupu,

Huoni ajabu kwamba, adui za Israel huwa wanauliwa hata wakiwa Ikulu ya Iran

Huo uwezo anao Israel pekee hapo middle

Na unaposema Israel alipize, kati ya Iran na Israel ni yupi ambaye huwa anaishia kulipiza
Hili unaliongea wewe mke wa Netanyahu, lakini Israel yenyewe haijawahi kusema hivyo. Kama una ushahidi wa Israel ikisema kuwa ilimuua mtu Iran basi tuwekee hapa tuone. Yenyewe huwa inatangaza iliowaua Lebanon na Gaza.

Lakini pia mbona umeshindwa kuzungumzia uwezo wa Hamas kuingia Israel mchana kweupee kuuwa wanajeshi kambini, kuteka maelfu ya watu na kutoka nao Israel hadi Gaza bila MOSSAD, Netanyahu na wapumbavu wengine kujua!! Kile kilichofanyika October 7 kinaonesha kuwa hapo Israel hakuna mtu ambae anaweza kuwa salama kama Iran ikimtaka. Fikiria watu wanaingia nchini, wanauwa mamia ya raia na makumi ya wanajeshi na pia kutoka na maelfu ya mateka bila kushtukiwa kitu ambacho hata hapo Rwanda kisingewezekana halaf wewe unakuja kusifia ujinga hapa.
 
nahisi wanachofanya israel ni kutengeneza mifumo ya kujilinda zaidi kupunguza adhari za vita kwao..na ili kuweza kupigana na iran inabidi uwanja wa vita uwe iran au jirani na iran...wanatafuta uwanja huo uwe lebanon rejea ramani ya middle east...vita hapigani nyumbani kwake israel anakufuata huko ulipo sawa na amrekani..kwa hio akishaikamata lebanoni kama ilivyo gaza leo..lazima akiwashe na iran...na iran kama anataa vita salama kwake aingie ajiunge na hezbula kwenye uwanja wa vita hapo lebanon..
 
Nilishasema NUCLEAR RODS zitakuwa overheated na kusababisha mlipuko mkubwa sana kwenye vinu vya kinyuklia. Serikali ya IRAN itajitokeza na kusema ni ajali ya kawaida kumbe ndani yake kuna jasusi la mossad linafanya kazi hapo hapo. Hence mission accomplished.


Namba 2. Sumu ya BOTOX au CYANIDE itatumika anywhere any point for massive caussalties in TEHRAN

Mind yu hapo BEIRUT kemikali ya AMMONIUM NITRATE iliyokuwa imetunzwa kwenye mapipa ya MELI iliyosajiriwa PANAMA ilimaliza mamia ya watu.

MOSSAD have ten thousand ways of reacting
 
Hiki kimbunga kinachotokea Marekani sasa hivi, kama kingetokea Iran saa hizi wangesema kuwa MOSSAD wapo kazini. Au ungesikia kuwa Mungu wa yakobo anaiadhibu Iran kwa sababu ya kushambulia Israel πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hii coment kwa heshima na taadhima naomba ifunguliwe uzi kabisa
 
Kushabikia vita ni upuuzi uliopindukia, Hivi huwa mnapata faida gani watu wasio na hatia wanapouwawa?

Kila nikiangalia kinachoendelea Gaza na Lebanon naona kabisa hakukuwa na haja ya kufanya mashambulizi ambayo yangesababisha maangamizi ya miji as outcome yaje.

Muda wetu wa kuishi hapa Duniani ni mfupi sana na hakuna kitu kitamu na chenye thamani kama uhai, Watoto na kina mama wanauwa kwa upuuzi wa watu wachache tu.

Ifike kipindi aya yote yaishe na Dunia iwe sehemu salama kwa kuishi kwa binadamu wote.

Najua wengi wa Watanzania tunashabikia huu upuuzi kwakuwa tupo kwenye Nchi ambayo tuna amani.
 
Israel ni nchi ya hovyo isiyokuwa na jeshi, silaha wala serikali imara. Kila kitu wanategemea wazungu, kuanzia jeshi, silaha na uongozi wa nchi.
 
Wayahudi wa uliyankulu hawalijui hilo. Wao wanajua kuwa hata hawa wazungu kina Netanyahu na genge lake ni wayahudi wenzao πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hao ndio wayahudi halisi, wewe hao unaowajua wako wapi.
 
Umeandika kishabiki sana, yaani Iran iwe na uwezo wa kuipiga Israel? Ni Marekani au UK ndo walimuua Ismael Haniyeh ndani ya Iran? Ni Marekani ndo waliua viongozi wote wa Hezbollah?
Acha kujidanganya wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…