Lindi: Zitto Kabwe na Sulemani Bungara (Bwege) wakamatwa na Polisi

Lindi: Zitto Kabwe na Sulemani Bungara (Bwege) wakamatwa na Polisi



Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo kupitia mtandao wa Twitter, Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe na Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Sulemani Bungara (Bwege) wamekamatwa

Chama hicho kimeeleza kuwa Polisi wamewasili kwenye mkutano wao wa ndani Wilayani Kilwa ambapo shughuli za kuwapokea Madiwani 8 wa CUF zilikuwa zinaendelea

Aidha, kimebainisha kuwa kitatoa taarifa zaidi baadaye kwani sasa Viongozi wa chama hicho mkoni humo pamoja na Wanachama wanaelekea Kituoni


CCM sasa inaamini polisi, kubambikia kesi na kutesa watu. chama cha wakulima na wafanyakazi kilicho asisiwa na Baba Mwalimu Nyerere sasa hakina hoja kabisa ndio maana kinatumia polisi.
 
Hao wahuni kina zito wakamatwe tu hatutaki siasa chafu
Semeni ukweli. Membe anawatesa mno. Bado hajaamua anagombea kupitia chama gani yewezekana ikawa ccm lkn ninyi mnaweweseka na kuhangaika na kina Zitto mkifikiri walikuwa wanafanya maandalizi ya kumpokea Membe.

Lengo la kuanzisha Act Wazalendo ilikuwa ni kupunguza kura za Upinzani. Sasa kama nyoka mlimfuga wenyewe chumbani keshakuwa mkubwa na hawezi kutoka tena mle chumbani. Kila atakaegusa mlango lazima ajeruhiwe.
 
ati Tunakwenda kuwa na uchaguzi HURU na HAKI - viashiria ndiyo hivi vishaanza kwamba hata mikutano ya ndani hairuhusiwi kwa sasa.
 
.
1592575.jpg
 
Back
Top Bottom