Lindi: Zitto Kabwe na Sulemani Bungara (Bwege) wakamatwa na Polisi

Niimeangalia clip ikionyesha kukamatwa kwa Kabwe na 'Bwege'. Clip haisemi kwa nini wamekamatwa, lakini wachangiaji wametoa kauli zao kana kwamba wanafahamu kwa nini wamekamatwa.

Mmoja anasema CCM wameisha anza kampeni na hawakamatwi. Kauli hii inamaanisha mchangiaji huyu anahisi wamekamatwa kwa kuanza kampeni kabla ya wakati(?)

Mwingine anasema nongwa ipo: kwa nini wakamatwe katika mkutano wa ndani? Huyu anamaanisha kosa walilofanya ni kufanya mkutano (japo walichukua tahadhari kufanyia ndani).

Mwingine anauliza "CCM uoga wa nini kukamata wapinzani?" Huyu anaelekeza mashambulizi kwa CCM, ambao anawatuhumu kuwaogopa upinzani kiasi kwamba wanaanza kuchukua tahadhari kuhakikisha wanaibuka washindi katika uchaguzi ujao.

Vivyo hivyo kwa michango mingine yote iliyotolewa: inajenga hoja kwa hisia tu na kutoa mtazamo kutokana na hisia hizo. Kwa nini ujenge hoja kwa hisia tu badala ya kupeleleza ukapata uhakika wa suala husika na hapo ndipo utoe msimamo wako ukiwa na uhakika wa uyasemayo? Polisi ana wajibu wa kukueleza kwa nini anakushika, na wewe mshikwaji una haki ya kuuliza kwa nini unashikwa. Sijui kwa nini clip iliyotolewa inakatwa hiyo sehemu ya maelezo wanayotuhumiwa nayo walioshikwa? Kama sehemu hiyo ingekuwepo, wachangiaji wangekuwa wanatoa maoni yao baada ya kuwa na uhakika wa jambo wanalolizungumzia. Sijui mtoa mada alikuwa na haraka gani ya kutoa hiyo clip kabla ya kuhakikisha kulikoni? Jambo la pili ni kuhusu kuelekeza lawama kwa CCM. Polisi ndio waliowashika watuhumiwa, na polisi ni chombo cha Serikali. Hivi kweli CCM (Chamwino au Lumumba) walikuwa wanafahamu kinachoendelea huko Lindi, au wachangiaji wanawabambikizia tu lawama?

Kufanya michanggo yetu iwe na maana, ipo haja tuchangie pale tu tunapokuwa na uhakika wa suala tunalotaka kuchangia na tuelekeze lawama au pongezi mahali husika.
 
Huyo zitto kutwa kujipendekeza kwa mabalozi kuichafua Nchi yetu

Akamatwe akae huko ajifunze
Nchi yetu ipi imechafuliwa? au ni Nchi yako mwenyewe? Zito kusema ukweli ni kuichafua Nchi?
 
Bunge lilishavunjwa, Bwege si Mbunge tena wa Kilwa Kaskazini
 
Jiwe alisema watakaoleta fujo na matusi watashughulikiwa, serikali haijalala. Sasa kumbe fujo zenyewe ndiyo hivyo vikao vya ndani? Au polisi hawakuelewa?
I wish I could be IGP!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…