Lipi ni sawa, kumfukuza kijana wako hapo kwako ili akaanze maisha yake au kumwacha azeekee hapo kwako?

Lipi ni sawa, kumfukuza kijana wako hapo kwako ili akaanze maisha yake au kumwacha azeekee hapo kwako?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Kwa jamii nyingi kijana akishapata umri basi anaonekana ameshakuwa mkubwa na hastahili tena kuwepo hapo kwako mzazi na mara ingine kama ataendelea kuwepo, basi atakereshwa almradi aondoke akaanze kujitegemea na s'tyms haya yanafanyika bila hata kujali kama mhusika ana ajira au la.

Wengi wanadai kumwondoa kijana kunaichangamsha akili yake kumfanya kijana ajitambue zaidi aache kujibweteka aongeze juhudi za kupambania maisha n.k.

Hii ni tofauti kwa jamii zingine hasa za kimwambao. Wao kijana hakui kwa mzazi. Mandhari mzazi yu hai basi mtoto atabaki kuwa mtoto tu, maisha yake yote. Huko kijana anaweza kuishi na wazazi hadi akapata wajukuu na pengine hata kuzeekea na hata kufia akiwa
hapohapo kwa wazazi.

Haya mambo wakuu yamekaaje?

Je, ungependa kumwona kijana wako katika taswira ipi kati ya izo mbili hapo juu?
 
Kwa maisha magumu na heka heka za kutokua na kazi maalum niliopitia baada ya kufukuzwa ,na Mzee kwangu nitakua tofauti sana, mwanangu wa kiume akae tu home hata akipata na vitukuu hapa sawa
Maisha ya kujitegemea bila kua na msaada au support yeyote kwa ndg mabaya sana unaweza kujikuta kibaka bila kupenda

Napenda sana mfumo wanaoutumia baadhi ya kabila kama wairaq kwao mtoto wa kiume akifikisha umri wa kuoa anakatiwa ngombe za kutosha then anaenda kujitafuta
 
Mjenge nyumba mfungulie miradi kisha mfukuze nyumban akajitegemee ili kupunguza wimbi la wezi katika taifa
😆mkuu unaongelea kujenga nyumba utafikiri ni kupanga maboksi ya viberiti,,,ujenzi wa nyumba kwa wengi wetu ni lifetime investment hlf uweze kumjengea dogo?,,,pamoja lakini 👍
 
Kwa maisha magumu na heka heka za kutokua na kazi maalum niliopitia baada ya kufukuzwa ,na Mzee kwangu nitakua tofauti sana, mwanangu wa kiume akae tu home hata akipata na vitukuu hapa sawa
Maisha ya kujitegemea bila kua na msaada au support yeyote kwa ndg mabaya sana unaweza kujikuta kibaka bila kupenda

Napenda sana mfumo wanaoutumia baadhi ya kabila kama wairaq kwao mtoto wa kiume akifikisha umri wa kuoa anakatiwa ngombe za kutosha then anaenda kujitafuta
kuna kipindi tulikuwa tunaishi anko na anti yetu. sasa bana maisha yalipobana sana mzazi akaamua kuwatimua wote wawili anko na yule anti wakajitegemee.

daah nakumbuka huu ulikuwa uamuzi mgumu sana na wa kikatili kabisa. lakin ndoivo mzazi hakurudi nyuma ilikuwa lazma anko na anti waondoke. basi bn wakaenda kupanga huko mitaa mingine ila mara kibao nliona anko alikuwa anarudi kijanja, anatym ile mida mzazi hayupo home yey ndo anakuja hom anang'ata sembe anapotea zake😆

Sasa bana katika struggle za life bana yule anti akaukwaa ukouko akaumwa sana hadi ikabidi arudi pale home kujiuguza hadi akafariki.

nlichojifunza usimtimue mtu anayekutegemea kama bado hajajipanga vinginevo unaweza kujikuta unaua mtu iviivi.
 
mi sitamtimua maana maisha niliyopitia sitamani mwingine ayapitia,hebu fikilia unakosa pakulala unasontea sehemu yenye kigodoro ndo unaweka kambi, unakosa hela ya kula unamwendea jamaa kistaarabu ili akusaidie hela ya kula ila anakwambia hela ipo ila mpaka nikuf*re..unaamua kujikataa kwenda kuchonga kalai ili upate chakutafuna imagine unashindia mhogo wa kutafuna kutwa nzima
 
Nimehisi mpk njaa.... Pole mkuu jamaa Hana ubinadamu hata kidogo. makutupora upo kijitonyama kwa kimaro au upo na huyu Bolotoba
 
Mfumo wa kufukuza vijana waliutumia zaidi wazee hapo kipindi Cha nyuma lakini kinaweza kuwa na madhara mengi kuliko faida! Na kupelekea vijana kupoteza utu wao, kuwa vibaka, na kila aina ya uhalifu

Kwa Dunia ya sasa Bora umwelekeze ajifunze stadi za kazi mbalimbali ambazo zitakuwa njia ya yeye kujitafuta na kuondoka hapo nyumbani Ila kumfukuza aseeh ni ngumu hiyo situation waliopitia hiyo wana mengi ya kutuambia
 
Back
Top Bottom